DAR: Akram Aziz akamatwa, afikishwa Mahakama ya Kisutu. Ana makosa 75!

DAR: Akram Aziz akamatwa, afikishwa Mahakama ya Kisutu. Ana makosa 75!

Watanzania tuamke!!! Mazingira haya yametengenezwa tu, kama taarifa ya mwanzo ilivyosema kua "askari wamemkamata akiwa na vibali sahihi, ila wakaamua kuondoka navyo vibali vyote original na kukataa kuacha copy ofisini kwake". Hapa kama kawaida, serekali inatuhamisha toka maswala fulani kutupeleka kwengine. Tumeshafanywa kama watoto wa chekechea sasa!!!

Watanzania lini tutapata akili jamani ya kuchanganua mambo na ukweli????? Tulishuhudia YUSUF MANJI alikamatwa na akafikishwa mahakamani kwa kukutwa na NYARA ZA SEREKALI, MIHURI YA JESHI, VITAMBAA VYA SARE ZA JESHI. Case iliishia wapi?????? Nani anaehoji mpaka sasa kuhusu hio tuhuma zake au case alizoshitakiwa nazo?????? Kama kweli angeachiwa huru????

Inasikitisha sana kuona mtu akitetea uonevu unaofanywa na askari kwa raia, na uongo tunaopewa raia na serekali yetu, kama huu na iliopita.

Na inasikitisha zaidi kuona wafanya biashara wakubwa wakionewa mpaka kufikia hatua wanafunga biashara zao na watanzania wenzetu kibao wanakosa ajira.
 
Kwa wana JF,

Natambua kuwa kuna threads 2 humu; ila taarifa ni kuwa Akram Aziz ambaye ni mdogo wa Mbunge wa zamani wa Igunga, Ndg. Rostam Aziz, ni kweli alikamatwa na Vyombo vya Dola na mchana huu amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu.

Kwa kuanzia, ana makosa takribani 75 ambayo anahusishwa nayo. Kuna utakatishaji fedha/uhujumu uchumi pia katika makosa hayo.

Taarifa zaidi zinakuja.

Kwa Taarifa za awali Soma => Akram Aziz adaiwa kukamatwa na nyara za Serikali... - JamiiForums
hebu fuatilia zaidi
 
HUWEZI FANIKIWA KWA KUMCHUKIA ALIYEKWISHA KUFANIKIWA
nakuunga mkono asilimia mia moja,pana dhana imejengeka kwa sasa kwamba akikamatwa tajiri akapewa mashtaka ya makosa aliyoyafanya na akaadhibiwa kisheria basi maisha ya sisi wananchi wa kawaida ndo yanakuwa mazuri,hilo sio sahihi na najua watu wengi wanaoshangilia haya hawashangilii kwa maana ya mkosefu kaadhibiwa ila wanashangilia kwa kudhani wao baada ya hapo watakuwa na maisha mazuri kitu ambacho si sahihi kabisa ifike mahali watanzania tubadiri mitizamo yetu
 
Back
Top Bottom