Huko sio kuchukiwa, huko ni kufuata na kuhukumu sheria alizovunja huyo bwanaako.
Mfanyabiashara mkubwa wa Utalii na uwindaji Akram Azizi ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya Kilombero North Safaris jana mchana alivamiwa na askari wakiwa na maofisa wananyamapori, akituhumiwa kuwa kontena lililosheheni nyara za taifa kinyume cha sheria zikiwamo pembe za ndovu, ngozi za chui na simba.
Baada ya upekuzi huo ulioanzia ofisini kwake na kisha kuhamia nyumbani kwake Masaki, askari hao hawakukuta kontena hilo wala ngozi za simba na chui kama walivyodai kutonywa.
Saa 20 baada ya kufanyika kwa kazi hiyo ambayo iliendeshwa huku watu wakizuiwa kuingia au kutoka katika maeneo hayo mawili, kumeanza kusambazwa picha mitandaoni zikiambatana na maelezo ya kumhusisha Mfanyabishara huyo wa Utalii wa Uwindaji (Akram Azizi) na tuhuma za ujangili zinaonekana kulenga kutia doa kazi halali na ya kisheria anayofanya, sambamba na kuilenga familia yake na watu wengine wenye undungu naye.
Picha hizo zimepigwa nje ya ofisi yake inayoitwa Kilombero Hunting Safaris na si nyumbani kwa Akram kama inavyoelezwa katika taarifa zinazosambazwa.
Bunduki zinazoonekana kupangwa katika picha hizo, zote ni za kampuni hiyo ya uwindani na utalii ambayo yeye Akram mkurugenzi wake na si za mtu binafsi na zote zimekutwa zikiwa na vibali vyote halali.
Katika upekuzi huo zimekutwa pembe sita za ndovu ambazo zina mihuli na vibali vyote vya serikali na pembe zote zina ‘serial numbers’ zikionyesha zilipatikana mwaka 2014. Hii ni kwa mujibu wa sheria.
Kisheria watu au makampuni yanayotaka kununua pembe za ndovu wanatakiwa kupata vibali serikalini na kwenda kununua ktk kampuni halali na zenye usajili kama hiyo ya Akram.
Upekuzi uliofanyika nyumbani kwake haujakuta kitu chochote tofauti kabisa na inavyotaka kuonekana katika taarifa za awali mitandaoni.
Hakuna anayepinga au kuhoji mamlaka halali za serikali kuhoji mtu kisheria, kinacholeta shida ni hatua ya watu wasiojulikana kusambaza kwa makusudi picha ambazo zinaambatanishwa na taarifa potofu ambazo kwa hakika malengo yake hadi sasa hayajawa bayana.
Wanasheria wa Akram wanashtushwa na bado wanaendelea kufuatilia ili kujua maana hasa ya hatua ya askari waliofanya ukaguzi huo kuondoka na hati zote halisi ‘originals’ na vibali vya umiliki wa silaha na hizo pembe za ndovu.
Askari hao ambao wanatokea Idara ya Maliasili na Polisi walipofika ofisini kwa Akram jana walidai kwamba, taarifa walizoambiwa ni kuwa kuna ngozi za simba, chui na nyara nyingine za serikali vitu ambavyo baada ya upekuzi mkali wa kushtukiza hawakuvikuta.
Kitendo cha kuondoka na vibali halali vyote na kuvizuia na kukataa kuacha nakala za nyaraka hizo na kitendo cha kuanza kusambaza taarifa mitandaoni kwa taswira ya upotoshaji kumetafsiriwa na wanasheria wa Akram na wa kampuni ya Kilombero North Safaris kuwa yenye nia ya kuandaa mazingira ya kutenda dhuluma.
Ahsante
Kilombero North Safaris
Dar es Salaam
31st October 2018