TANZIA Dar: Ali Mohamed Kibao, kiongozi wa CHADEMA auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana

Hii kitu inamchafua sana Mh. Rasi Mama Samia, asipofanya maamuzi mazito kukemea haya yanayoendelea hii nchi itamfia mikononi mwake.

Very sad new indeed.
 
Hii kitu inamchafua sana Mh. Rasi Mama Samia, asipofanya maamuzi mazito kukemea haya yanayoendelea hii nchi itamfia mikononi mwake.

Very sad new indeed.
Hili siyo la CHADEMA, bali wananchi wanapaswa kuja na utaratibu huu, hiyo ndiyo namna ya kujilinda
 
Hadi kuzuia basi inaonekana kulikuwa na shutuma nzito ikizingatiwa bwana huyu amewahi kuwa mtumishi wa umma(Askari) kule unalishwa viapo vya kutunza Siri.

Pole yake na ndugu zake
 
Chadema tena!?ndio wanao tumia ma defender ya police!?mbona kama unaleta masihara kwenye matukio magumu!?
Uchunguzi ufanyike, dereva na abiria waitwe.

Sio kulishwa matango pori na watu wenye agenda zao.

Ni rahisi sana kufanya dhambi Tanzania kwa sababu ya ushabiki,

Sioni motive ya serikali kwenye hiko kifo.
 
kwa masikitiko makubwa natoa pole na rambirambi zangu kwa ndugu, jamaa na marafiki wa ALI MOHAMED KIBAO ambae ametangulia mbele ya haki.

nawaombea wafiwa wote moyo wa ustahimilivu na subra katika kipindi hiki kigumu.
kifo ni fumbo, kifo hakizoeleki.

Mwenyezi Mungu aileze roho ya marehemu ALI MOHAMED KIBAO mahali anapostahili, Aimen.
 
Mods wacheni tutoe ushauri na tahadhari ili kama wana masiko, basi na wasikie.

Wiki kama mbili zilizopita, yule dada maarufu anaeshi nchini marekani, aliandika katika mtandao wa X makala ndefu ila yenye maneno makali na matusi mazito juu ya kiongozi fulani kiasi yanayoendelea hapa nchini.

Nilikuwa nasoma na kusisimka, ila kwa tukio hili la leo, siwezi kusisimka tena hata aandike nini.

Nimalizie kwa kusema , kwa haya yanayoendelea, huyu dada sitashangaa akaja na makala nyingine mbaya zaidi na akapata uungwaji mkono mkubwa zaidi.

Washauri, mna uhakiki hii itasaidia na zaid mnaona mnamsaidia Bosi wenu au ndio mnazidi kumuharibia?

Kwa nature ya binadamu, mimi naona matukio haya yatawafanya watu wawe majasili zaidi na sasa waone hawana tena cha kupoteza.

Mtambue kuwa, kadri wengi wanavyoumizwa, ndio wengi zaidi huona na wao sasa hawana cha kupoteza na wanazidi kujawa na hasira. Hivyo, hii mbinu mnayotumia, ni sawa na kumwaga petrol kwenye moto ulionza kuwaka.

Pia, kwa haya yanayoendelea, hata mkiomba serikali ya huko aliko imrudishe nchini, inaweza kumuona kama ni mtetezi wa watu badala ya mhalifu.

Anyway, Mungu ana makusudi na kila jambo.
 
Hata kama ni CHADEMA, Serikali na Taasisi husika inabidi zichukue hatua na kukomesha huu upuuzi na upumbavu..., mmoja wetu akifa (mwananchi / nguvu kazi) lazima vyombo husika vifuatilie na kuwahoji watuhumiwa no matter their political stance....
 
Rais amebariki Utekaji na umeuita jina zuri la Drama, msihamishe magoli
 
Ukute hii Nchi inaongozwa na majitu mwitu (nephil ) maana haya majitu yana roho za kutu zilizopitiliza ,
Ccm ni cancer , haya majitu hayafai kuishi , rot in hell .
Scambags
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…