TANZIA Dar: Ali Mohamed Kibao, kiongozi wa CHADEMA auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana

Nchi hii chini ya utawala wa chama dola kongwe sasa imekwisha.

Imekuwa ni utawala wa kishetani ambapo mauji, utekaji, kupoteza na kuteswa imekuwa kitu kinachotumiwa serikali kwa kuwa imeshindwa kudhibiti vyombo vyake vya ulinzi na usalama.

Labda serikali waje na taarifa nyingine ya kuridhisha kuwa ni vinginevyo kuwa vyombo vyake havihusiki.

Na serikalu kutuletea ushahidi kuwa kuna magenge ya kigaidi ndani ya nchi ya Tanzania ndiyo yanayo teka raia, na watuambie hao magaidi wanafadhiliwa, wanawezeshwa na kupewa baraka na nani kufanya mauaji, kutesa, kuteka na kupoteza
 
Roho imeniuma zaidi kuona spika alikataa huu mjadala bungeni. Namuombea laana huyu mama
 
Na hapa ndio tulipopotoka kama Taifa na nasikitika hata wananchi tushaingia kwenye huu Upuuzi..., Hakuna vijana wa CHADEMA kuna vijana wa Tanzania na Watanzania..., tutakapoendelea kujigawa kwa mafungu sisi wa huku chini tutaendelea kutumika kama madaraja kwenye Siasa....

Jambo kama hili likemewe sababu sio la kibinadamu no matter aliyeshikwa ni mwanasiasa au teja...., Ama sivyo hizi Divide and Rule zitaendelea kuwanufaisha wachache no matter Chama gani kitakuwa kimeshika Hatamu,... Kwahio yoyote anayefanyiwa ndivyo sivyo kila mtu akemee kwa nguvu zote na wakati wote....
 
Kuna Kila Sababu CCM na Jeshi la Polisi Kuchunguzwa

Katika kipindi cha hivi karibuni, kumekuwa na ongezeko la matukio ya utekaji wa watu nchini Tanzania, hali inayosababisha hofu kubwa miongoni mwa wananchi. Wakati matukio haya yanavyozidi kuibuka, kuna wasiwasi kwamba vyama vya siasa, hususan Chama cha Mapinduzi (CCM), pamoja na Jeshi la Polisi, vinaweza kuwa na uhusiano wa moja kwa moja na matukio haya. Hii ni sababu mojawapo inayopelekea vyombo vya ulinzi na usalama kuchunguza hali hii kwa makini.

Utekelezaji wa Sheria na Ulinzi

Jeshi la Polisi lina jukumu kubwa la kuhakikisha usalama wa raia na mali zao. Hata hivyo, katika baadhi ya matukio, kuna madai kwamba polisi wamekuwa wakishindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo, au pengine wanashirikiana na wahalifu. Hali hii inazua maswali kuhusu uaminifu wa kikosi hicho na uwezo wake wa kukabiliana na uhalifu. Uchunguzi wa kina unahitajika ili kubaini kama kuna ushirikiano wowote kati ya polisi na wahalifu katika matukio ya utekaji.

Tuhuma dhidi ya CCM

Chama cha Mapinduzi, kama chama tawala, kinahusishwa na matukio mengi yanayoleta wasiwasi katika jamii. Kuna tuhuma kwamba baadhi ya viongozi wa CCM wanaweza kuwa na ushirikiano wa kisiasa na wahalifu, kwa sababu ya maslahi yao ya kisiasa. Utekaaji wa watu unaweza kuwa mbinu ya kuwatisha wapinzani au kuzuia sauti za upinzani zisisikike. Hali hii inahitaji uchunguzi wa kina, kwani inahusisha maslahi ya kisiasa na usalama wa wananchi.

Mitandao ya Kijamii na Mlipuko wa Habari

Mitandao ya kijamii imekuwa chombo muhimu katika kutoa taarifa kuhusu matukio ya utekaji. Wananchi wanatumia mitandao hii kufichua matukio ambayo hayapewi kipaumbele na vyombo vya habari vya kawaida. Hata hivyo, kuna hatari ya habari zisizo sahihi kuenea, na hivyo kuchangia kuongezeka kwa hofu katika jamii. Vyombo vya ulinzi na usalama vinahitaji kuchunguza si tu matukio yenyewe, bali pia chanzo cha taarifa hizo na namna zinavyotolewa.

Mhimili wa Haki za Binadamu

Ni muhimu kutambua kwamba matukio ya utekaji yanavunja haki za msingi za binadamu. Wananchi wanapaswa kuwa huru na salama katika nchi yao, na yoyote anayehusika na ukiukaji wa haki hizi lazima achukuliwe hatua. Hali hii inahitaji ushirikiano kati ya vyombo vya ulinzi, mashirika ya haki za binadamu, na jamii kwa ujumla ili kuhakikisha kwamba haki za kila mtu zinaheshimiwa.
Hitimisho

Kwa ujumla, kuna haja ya uchunguzi wa kina kuhusu uhusiano kati ya CCM, Jeshi la Polisi, na matukio ya utekaji nchini Tanzania. Hili ni suala nyeti linalohitaji umakini wa hali ya juu ili kubaini ukweli na kuchukua hatua stahiki. Wakati huu wa mabadiliko, ni muhimu kwa kila mdau kushirikiana na kuhakikisha kwamba usalama wa raia unalindwa, na kwamba haki za binadamu hazikiukwa. Serikali, vyama vya siasa, na jamii kwa ujumla wanapaswa kufanya kazi pamoja ili kuondoa hofu na kuimarisha amani katika nchi.
 
Mabasi ya kisasa yana camera, waliomteka wote wamerekodiwa, ni suala la polisi kuwataja baaasi
CCTV footage za area D wahuni waliingia nazo mitini.

CCTV footage za Clouds TV Bashite alipovamia zipo ila wahuni wenye nazo wakakaa kimya.

CCTV footage za Sabaya akiwa anatishia mtu benki zipo , walipoomba ushahidi mahakamani wakasema zisiletwe.

Hizo CCTV footage wala hazitoletwa.

Bashite, Sabaya na majambazi wengine mnatamba nao uraiani tu huko.

Wauaji hawawezi kujichunguza.

Poleni wafiwa.
 
Tukiendekea kuiacha CCM madarakani na Serikali yake kwa ufupi tusahau mabadiliko yoyote yale na tunavyo zidi kua mashujaa wa nyuma ya keyboard ni kuendelea kupoteza muda.

hakuna hatua madhubuti, hakuna mabadiliko.
 
Jeshi la Polisi na wizara yake mama, Watoke wafanye uchunguzi wa haraka na kutoa mrejesho kwa umma na familia ya marehemu. Maana sasa semina elekezi imebainisha wameongezewa bajeti kwa zaidi ya asilimia 900%, ndiyo asilimia Mia tisa kuwezesha jeshi la polisi kutekeleza majukumu yake ya ulinzi wa raia na mali zao.

06 September 2024​

SEMINA ELEKEZI KWA VIONGOZI WAANDAMIZI WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI 2024​


View: https://m.youtube.com/watch?v=jsMEnkMCoc4
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka maafisa waandamizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Tanzania na viongozi wa vyombo vya usalama wa Wizara hiyo kutekeleza kwa vitendo na kuiishi falsafa ya R NNE (4R) ya Rais Dk. Samia S. Hassan ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.


Amesema hayo leo Septemba 06, 2024 wakati alipofungua Semina elekezi kwa viongozi waandamizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Weruweru River Lodge, mkoani Kilimanjaro, Tanzania.

Amesema kuwa ni muhimu kuifahamu vyema falsafa hiyo ya Rais Dkt. Samia Hassan na kuitekeleza kwa vitendo. “Nina imani kubwa kwamba uongozi wa juu wa Wizara umeielewa vizuri falsafa hiyo, na semina hii elekezi ni ushahidi tosha wa kuitekeleza kwa vitendo”.


“Falsafa hii inajikita katika masuala ya Maridhiano (Reconciliation), Ustahamilivu (Resilience), Mageuzi (Reforms), na Kujenga upya Taifa (Rebuilding).

Hivyo, nitoe wito kwa washiriki ambao ni Maafisa Waandamizi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi pamoja na Menejimenti ya Wizara na Taasisi zake kuendelea kushiriki na kuishi kikamilifu falsafa hii,”amesema.


Ameongeza kuwa semina elekezi hiyo ni sehemu muhimu kwa maendeleo ya kitaaluma na kitaasisi kwa maafisa waandamizi wa vyombo vya usalama, na husaidia katika kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kwa kufuata viwango vya kitaaluma na kisheria.

“Semina elekezi hutoa fursa kwa maafisa waandamizi kujifunza mbinu na taratibu mpya katika utendaji wa majukumu yao. Hii inajumuisha teknolojia mpya, mbinu bora za ulinzi na usalama, na mbinu za kisasa za kupambana na uhalifu,”.

Kwa Upande wake Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, engineer Hamad Masauni amemshukuru Rais Dk. Samia Hassan juu ya nia yake ya dhati kwa kufanya maboresho ya Wizara hiyo na vyombo vyake ikiwemo Jeshi la Polisi, Magereza, Uhamiaji na Zimamoto pamoja na Taasisi ya NIDA.

“Maboresho haya yanahusisha upandishaji vyeo wa kihistoria wa Maafisa, Wakaguzi na Askari wapatao 50,971 pia kuongeza Bajeti ya Miradi ya Maendeleo kutoka mwaka 2021/22 hadi 2024/25 ni Shilingi 262.2 ambayo ni sawa na asilimia 954.59 ya ongezeko la Bajeti ya Miradi ya Maendeleo,”amesema.

Amesema kuwa Ongezeko hilo la bajeti limesaidia kwa kiasi kikubwa kupatikana kwa vitendea kazi ikiwemo magari, mitambo, boti, vifaa vya TEHAMA na kadhalika
 
Ila pia mimi naamini Magufuli licha ya kuwa kutiliwa mashaka ya kuhusika na shambulio la Lisu ila haya mengine si amini sana kwa kuwa haya mambo yamekuwepo muda sasa na wash ukiwa ni vyombo vya ulinzi na usalama!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…