TANZIA Dar: Ali Mohamed Kibao, kiongozi wa CHADEMA auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana

Mbowe na genge lake walimsema sana Dkt Magufuli ndiye anaagiza waty wafe, walifanya sherehe hahaha, ngoja sasa ngoma inogile. Dkt Magufuli alikuwa mkarimu sana
Magufuli ndio muasisi wa huu uhayawani. Na wanaofanya haya ni wale aliokuwa anawatumia yeye.
 
Sasa roho zao zimefurahi nafsi zao zimeridhika kukuona ukiwa mwili mtupu usio na pumzi,Hujawahi kuwatendea baya lolote,kosa lako ni kuwa mwanachama wa CHADEMA.

Tutakutana tena Mbinguni Kamanda.😭😭😭
 
Alishasema utekaji ni drama.

Sijajua kama anamaanisha alichokosema maana haishi drama
 
Usichukulie mambo kirahisi wewe ungekuwepo mle ungefanya nini au unaandika tu
 
Inawezekana serikali INAHUJUMIWA....

Iko siku hili litathibitika....

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Nakataa kabisa kwamba serikali inahujumiwa kwa sababu imekua mstari wa mbele kupinga uwepo wa matukio hayo kuanzia Rais Mwenyewe aliyesema ni drama, Speaker kuondosha swala hilo lisijadiliwe na wabunge na kuitenga polisi na kadhia hiyo. Huku viongozi waandamizi wa chama wakitamka maneno yanayoashiria uhusiono wa moja kwa moja na matukio hayo. Wakati huo huo Jeshi la polisi halijamkamata mtuhumiwa yoyote anayehisiwa au aliyehusika kwenye tukkio hata moja la utekaji ama kwa kupanga au kutekekeza moja kwa moja ili tuone kwamna serikali inahujumiwa. Then serikali inayokubali kuhujumiwa kwa damu za watu ni serikali dhaifu kabisa na haipaswi kuwepo kwani itakua imeshidwa kutimiza wajibu wake wa kulinda raia na mali zao. Leo Polisi walikua wanatumia nguvu kuzuia Wakili wa CHADEMA chama alichokua akikitumia marehemu kushiriki katika uchunguzi (postmeterm) wa maiti. Hii inafikirisha na inatoa majibu yenye mashaka kidogo kuwa serikali inahusika.
 
Hata ukianzishwa wewe, mi nipo tayari kuandamana mkuu.

Leo Mzee Ally, kesho hatujui ni zamu ya nani? Inawezekana ni zamu yako au Yangu. Ukiandamana au usipoandamana wakiamua kukuua wanakuua tu kama walivyomuua mzee wetu kikatili.
Shida Legal system ya nchi iko corrupt, unafanyiwa unyama na kesi inaisha kienyeji tu kwa maelekezo. Tuombe tu mwisho mwema
 
Imefika wakati sasa wananchi Wana kila sababu na haki kuchukua hatua mkononi kwa usalama wao na familia zao kwanza kugoma kuchukuliwa na mtu yeyote anayeitwa polisi awe amevaa uniform au hajavaa maana tulipofika huwezi kuwa na imani na jeshi hili la polisi Tanzania.maana kuna wengine wanakuja na uniform na vitambulisho at the end of the day inakujasemekana sio polisi ni mambo ya ajabu sana ndani ya nchi hii.
 
Hili kundi liki chini ya Rais na linalatibiwa na Rais. Akitaka kulifuta na dakika sifuri.
 
Hili kundi liki chini ya Rais na linalatibiwa na Rais. Akitaka kulifuta na dakika sifuri.
Absolutely, Yes...

Hata statement yake ya leo (Kama kweli yeye) haioneshi kuguswa kwa chochote...

Ni usanii tu wa kupooza mambo, baada ya hapo "business as usual"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…