TANZIA Dar: Ali Mohamed Kibao, kiongozi wa CHADEMA auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana

TANZIA Dar: Ali Mohamed Kibao, kiongozi wa CHADEMA auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana

Imefika wakati sasa wananchi Wana kila sababu na haki kuchukua hatua mkononi kwa usalama wao na familia zao kwanza kugoma kuchukuliwa na mtu yeyote anayeitwa polisi awe amevaa uniform au hajavaa maana tulipofika huwezi kuwa na imani na jeshi hili la polisi Tanzania.maana kuna wengine wanakuja na uniform na vitambulisho at the end of the day inakujasemekana sio polisi ni mambo ya ajabu sana ndani ya nchi hii.
Yes..

Tunapaswa kujilinda.....

Tunapaswa kuomba ulinzi wa Mungu na atufundishe namna ya kukabiliana na shetani hawa wanapotujia kutudhuru....

Usikubali kwenda kufa kizembe. Bora ufe ukipambana nao iwe AMA ZAO, AMA ZANGU.....
 
Amir Jeshi atumie nguvu na madaraka yake kudhibiti vyombo vyake vya dola.
 
Kuna watu huwa wanawasema sana wanyaruwanda, wahutu na watusi kama watu walio na roho mbaya sana, mtu fulani anapofanya jambo baya sana la kikatili kwa mwenzake utasikia kauli kwamba "huyu hawezi kuwa Mtanzania", "arudishwe kwao Burundi", "Watanzania hatuko hivyo"na kauli nyingine za kibaguzi kama hizo.

Sasa ni dhahiri kwamba Watanzania nao ni binadamu sawa na binadamu wengine wote wanaoutuzunga nchi za jirani linapokuja suala la ukatili na kinachoitwa roho mbaya, hatuna tofauti nao, lilikuwa ni suala la kutufautiana nyakati na muda tu.
 
Raia Samia hajatoa kauli thabiti dhidi ya kundi hili la kigaidi linaloendelea kufanya uhalifu wa kuteka na kuua raia wasio na hatua....

Aidha polisi wameendelea kutoa kauli tata, zilizobeba mizaha, kutojali na zinazoonesha "zero responsibility" kwa Jeshi la Police kinyume kabisa na wajibu wao wa kisheria na kikatiba.......

Kwa niaba ya raia wenzangu, naomba serikali kwa ujumla (Rais Samia Suluhu Hassan) na specific Jeshi la police wajibu maswali haya muhimu ya wananchi:

1. Kazi na jukumu la msingi la Jeshi la Police ni kulinda Usalama wa raia na Mali zao. Kazi yenu polisi pia hutekekezwa kutumia intellejensia ya kunusa uhalifu, kisha kuchunguza, kudhibiti na kukamata wahalifu na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria. Kama hizi ndizo kazi zenu, ni kwanini mauaji haya yanaendelea na ninyi mkiwa mpo kimya tu....?

2. Circumstantial evidence inaonesha wazi kuwa polisi kwa upande wa pili ni nyie mnahusika. Mmeunda genge la utekaji na uuaji wa kuteka na kutesa watu mnaoambiwa na viongozi wenu muwaue. Haina shaka kuwa mnafadhiliwa na wanasiasa vigogo ndani ya CCM na serikalini lengo likiwa ni kulinda madaraka na influence yao ya kisiasa. Polisi mmezikana tuhuma hizi. Mmesema hamhusiki. Kama ndiyo hivi, ni nani wanahusika....?

3. Genge hili la ugaidi linaloendesha shughuli zake mchana kweupe, kila linapomlenga mtu fulani na likimfikia hujitambulisha kuwa ni "police" wakitumia magari ya kifahari sana na wakati mwingine ya Jeshi polisi kwa sura na usajili wa namba zao. Swali muhimu ni hili, kwamba, inakuwaje genge hili la kihalifu linalojitambulisha kama "police" pale linapotenda uhalifu wake mchana kweupe na nyie polisi halisi hamfanyi kuchukua hatua zozote kuwatia mikononi mwenu wauaji hawa...?

4. Serikali (Rais Samia Suluhu Hassan), TANPOL na Waziri wa mapolisi ndugu Masauni, Je mmeshindwa kulinda uhai wa raia? Mnafanya nini kwenye ofisi zetu za umma kama genge hili la ugaidi limewashinda nguvu kiasi cha kujiona lenyewe ndiyo serikali? Kwanini mnadhani mnastahili kuaminika ktk mazingira haya?

##Rais Samia Suluhu Hassan toka mafichoni, acha kuwa chura kiziwi wa Kizimkazi waambie raia kuwa wewe na serikali yako mmeshashindwa kazi, mmeshindwa kutumia vyombo vya ulinzi kutulinda uhai wa watu ili kila mtu achukue hatua binafsi za kujilinda muone kama tutashindwa....!

======================================
UPDATES:

Hatimaye Rais Samia Suluhu Hassan (Chura Kiziwi) kafunguka masikio, amesikia na kutoka huko alikojificha na kutoa kauli.....

Si kauli thabiti kivile, yenye mamlaka na kumaanisha, lakini ingalau kasikia kilio cha umma na kusema neno japo inaonekana Kuna lijamaa limemwandikia tu hii statement, likaweka picha yake na kuitoa mitandaoni👇

Si kauli ya kumaanisha na kuonesha u - serous wa tatizo lililopo kwa sababu TANPOL a.k.a Polisi na Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) ndiyo watuhumiwa wa kuhusika na kuendesha genge hili la kigaidi linalo teka na kuua raia bila sababu...

Rais Samia Suluhu Hassan Hassan hayuko serous. Anataka kunufaika kisiasa na damu za watu hawa wanaouwawa....
View attachment 3090590
Lawama mh.raisi hawezi kuzikwepa kwasabab ndy kichwa na sura ya nchi lakin haina uhalali kuwa naye ni muhusika wa vitendo tajwa. Ukubwa jalala kila jambo baya lazma atupiwe yeye mkuu wa nchi. Lakin kwny uhalisia hvi vtu vina mambo na siri nyng ndani yake, badala ya kuoneshan vidole its time kama nchi kuonesh mshikamano na viongoz kupinga haya matukio na kuwapa ushirikian jesh la polisi, hata majambaz wanawez sema wao n polisi kumbe sio, at least tuwe na imani japo kdgo na jeshi , na tunaomb jeshi lisawazishe haya mambo yanaharibu sana uongozi wa samia na taswira ya nchi.
 
Usichukulie mambo kirahisi wewe ungekuwepo mle ungefanya nini au unaandika tu
Hapana, Matrix19 Yuko sahihi...

Sema tu kuwa, watu wengi bado hawana awareness ya uovu na mauaji haya yanayoendelea hapa nchini......

Laiti abiria wa bus lile wote wangekuwa wako aware, hayo magaidi na bunduki zao wasingefanya lolote. Lazima wangekimbia wenyewe.....!!

Aidha wengine wanajua lakini wanafikiri yanawahusu wanasiasa tu hasa CHADEMA lakini ukweli ni kuwa kila mtu anaathiriwa na ujambazi na mauaji haya ya kutengenezwa na watawala...
 
Usichukulie mambo kirahisi wewe ungekuwepo mle ungefanya nini au unaandika tu
Hakuna mahali nimesema rahisi na ndio maana nikasema "kama".

Kiburi huwa ni jadi ya viongozi ila mzaha mzaha , Mubaraka, Gadaffi, Al Bashir waliondolewa madarakani licha ya kujiona hawagusiki.

Nguvu ya umma ikiamua hizo risasi si kitu .
 
Lawama mh.raisi hawezi kuzikwepa kwasabab ndy kichwa na sura ya nchi lakin haina uhalali kuwa naye ni muhusika wa vitendo tajwa. Ukubwa jalala kila jambo baya lazma atupiwe yeye mkuu wa nchi. Lakin kwny uhalisia hvi vtu vina mambo na siri nyng ndani yake, badala ya kuoneshan vidole its time kama nchi kuonesh mshikamano na viongoz kupinga haya matukio na kuwapa ushirikian jesh la polisi, hata majambaz wanawez sema wao n polisi kumbe sio, at least tuwe na imani japo kdgo na jeshi , na tunaomb jeshi lisawazishe haya mambo yanaharibu sana uongozi wa samia na taswira ya nchi.
Angekuwa mtoto wake, mtu wake wa karibu asingechukua hatua?
 
Serikali ina mkono mrefu sana ,tukio kama lile la watu waliojiamini kuteka basi na kuja kumtoa abiria ndani na mitutu kisha wakaondoka naye kwenda kumuua unadhani ni raia wa wakawaida? Unafikiri wangekuwa raia wa kawaida wangefika hata bahari beach bila kukamatwa?
So sad! Yaani mtu anakwenda kuuawa kirahisi kama vile ng'ombe. Dah!
Kutofautiaba itikadi kihalali adhabu ni kifo.
Waliopigania uhuru wakifufuka wataupigania tena
 
Ile Sheria mpya ya usalama wa taifa kuwekewa Kinga ya kutoshitakiwa ifutwe haraka kwani wahuni wa ccm wanajificha humo.
TLS hebu tuelimishane juu ya umuhimu wa Sheria hivyo kwa taifa letu Kama Haina manufaa basi serikali ilazimishwe kuifuta Sheria hivyo haraka!
Ina manufaa kwa watawala tu.
 
Kuna watu huwa wanawasema sana wanyaruwanda, wahutu na watusi kama watu walio na roho mbaya sana, mtu fulani anapofanya jambo baya sana la kikatili kwa mwenzake utasikia kauli kwamba "huyu hawezi kuwa Mtanzania", "arudishwe kwao Burundi", "Watanzania hatuko hivyo"na kauli nyingine za kibaguzi kama hizo.

Sasa ni dhahiri kwamba Watanzania nao ni binadamu sawa na binadamu wengine wote wanaoutuzunga nchi za jirani linapokuja suala la ukatili na kinachoitwa roho mbaya, hatuna tofauti nao, lilikuwa ni suala la kutufautiana nyakati na muda tu.
Huwa nasemaga watanzania wana roho mbaya mnyarwanda
Ana subiri.....
Na kwa matukio haya ya kutoana uhai chuki ndiyo zinazidi kupandikizwa

Ova
 
Back
Top Bottom