#COVID19 Dar: Askofu Ruwai’chi aagiza mapadri wote kupata chanjo dhidi ya UVIKO-19

#COVID19 Dar: Askofu Ruwai’chi aagiza mapadri wote kupata chanjo dhidi ya UVIKO-19

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
1629801957494.png

PICHA: Askofu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu Yuda Tadheus Ruwai’chi

Askofu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu Yuda Tadheus Ruwai’chi ameagiza mapadri wote wa jimbo hilo kupata chanjo dhidi ya Uviko 19 kwa kuwa ugonjwa huo unaumiza na kuondoa uhai.

Ametoa agizo hilo leo Jumanne Agosti 24, 2021 katika adhimisho la Misa Takatifu ya kumuombea Padri Paul Haule aliyekuwa Paroko Msaidizi katika Parokia ya Mtakatifu Petro na Mkurugenzi wa Tumaini Media.

Ruwai’chi amesema mwaka 2020 wakati wa awamu ya kwanza ya janga la Uviko-19 watu walimuomba Mungu ajaalie kupatikana kwa chanjo, ambayo sasa imepatikana.

“Tulimuomba Mungu ajaalie kupatikana kwa chanjo sasa imepatikana badala ya kutumika watu wameingia katika malumbano ya kusema haya na yale dhidi ya chanjo,” amesema.

“Tusingojee hadi mambo haya yatutinge, tutumie vizuri fursa alizotupa Mungu kujikinga na kujihami na kwa sababu hiyo, sijui ni mapdri wangapi ambao mmeshachanjwa, lakini leo naomba nitoe agizo, kila padre akachanjwe, kila padre akachanjwe, tusifanye utoto, tusifanye lelemama, hii uviko 19 haina mjomba na shemeji na inatuondolea uhai,” amesema Ruwai’chi

Amesema ni utashi wa Mungu kwa watu wawe hai na kuwa na uhai tele hivyo ni vyema kuujali uhai waliopewa.

“Tujihami na tuendelee kumuomba Mungu, atuhurumie na tujihami na atuondolee hili janga,” amesema Ruwai’chi.

Mwananchi
 
Mapadri wote Tanzania nzima?

Hao mapadri hawana uhuru wa kuamua kuhusu matumizi ya miili yao ama ukiwa padri mwili ni wa kanisa ama askofu?

Halafu nimesikia mshikaji akimshambulia Gwajiboy, jumapili Gwajima akimjibu asije kulalamika, amuulize mwenzake Pengo kilichomkuta kutoka kwa Gwajiboy
 
View attachment 1906131
PICHA: Askofu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu Yuda Tadheus Ruwai’chi


Dar es Salaam. Askofu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu Yuda Tadheus Ruwai’chi ameagiza mapadri wote wa jimbo hilo kupata chanjo dhidi ya Uviko 19 kwa kuwa ugonjwa huo unaumiza na kuondoa uhai.
Ubarikiwe sana BABA ASKOFU aaamin aaamin🙏

Hii ndiyo tofauti kubwa iliyopo kitaasisi Kati yenu "WASOMI MAJINIASI" na wale viongozi wa DINI wakuokotezwa......

#ChanjoNiBoraKulikoTiba
#NchiKwanzaKablaYaYeyote
#SiempreJMT
 
Yule "bwana mropokaji" alishawahi KUMSHAMBULIA kwa maneno mabaya mwadhama Askofu msomi....

Sasa tunasubiri tena amshambulie msomi baba Askofu Ruwaichi......

Wenzake wanaitambua kuwa SAYANSI ni moja ya elimu MWENYEZI MUNGU ametupatia , yeye anatambua "CONSPIRACY THEORIES" kuwa ndiyo majibu makubwa zaidi ya SAYANSI.....

#ChanjoNiBoraKulikoTiba
#SiempreJMT
 
View attachment 1906131
PICHA: Askofu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu Yuda Tadheus Ruwai’chi

Askofu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu Yuda Tadheus Ruwai’chi ameagiza mapadri wote wa jimbo hilo kupata chanjo dhidi ya Uviko 19

Amesema ni utashi wa Mungu kwa watu wawe hai na kuwa na uhai tele hivyo ni vyema kuujali uhai waliopewa.

“Tujihami na tuendelee kumuomba Mungu, atuhurumie na tujihami na atuondolee hili janga,” amesema Ruwai’chi.

Mwananchi
👊😍👋👍
 
Askofu anatoa agizo mapadre wote wachanjwe? Hata Papa hajatoa agizo popote! Kiukweli hilo agizo linastua sana! Seems ukichanja unatamani kila mtu achanje na wala si tu kwa nia njema bali kibinadamu tuna hulka hiyo.

Askofu hili haupo sawa. Mapadre watakupinga waziwazi na kuingiza Kanisa kwenye mgogoro ambao hukuutegemea. Kwanza unawaambia waache "utoto" kweli? Unafikiri kwa nafasi yako ya uaskofu maana yake umezidi mapadre wote akili?

Nimesikiliza hiyo hotuba nikawa very disappointed [emoji20] na Askofu wetu huyu.

Chanjo ni hiari, kama serikali inasema ni hiari wewe kiongozi wa dini unasema lazima? Kesho serikali ikiongoza kwa imla utapinga wewe? Very disappointed [emoji20]
 
View attachment 1906131
PICHA: Askofu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu Yuda Tadheus Ruwai’chi

Askofu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu Yuda Tadheus Ruwai’chi ameagiza mapadri wote wa jimbo hilo kupata chanjo dhidi ya Uviko 19 kwa kuwa ugonjwa huo unaumiza na kuondoa uhai.
Kanisa katoriki ni taasisi imara na inayoongozwa kwa weledi wa hali juu. Tuliosoma seminary tunafahamu hilo na ndio chombo pekee kilichoonesha msimamo wakati wa vituko vya awamu ya tano. Tuna shida sana kwenye educational program zetu zinatoa half cooked personnel. Haiwezekani na kituko cha dunia watu kuendeshwa na hisia kiasi kile yaani. It is impossible to move a mountain by say '' mountain go" haiwezi kutokea. Itoshe kusoma kongole kwa baba askofu na taasisi yako
 
Back
Top Bottom