#COVID19 Dar: Askofu Ruwai’chi aagiza mapadri wote kupata chanjo dhidi ya UVIKO-19

#COVID19 Dar: Askofu Ruwai’chi aagiza mapadri wote kupata chanjo dhidi ya UVIKO-19

Askofu anatoa agizo mapadre wote wachanjwe? Hata Papa hajatoa agizo popote! Kiukweli hilo agizo linastua sana! Seems ukichanja unatamani kila mtu achanje na wala si tu kwa nia njema bali kibinadamu tuna hulka hiyo...
Wewe kafiri askofu wako Yupi?

Hiari wewe na mumeo ila ktk himaya yake ametoa agizo.

Sasa tuone atakayenyanyua mdomo.

Kwanza ujue katoliki hawana ujinga kama wenu, hata wakichukia wataupiga kimya na ndivyo walivyofunzwa.
 
Tulimwomba Mungu awajalie utashi wanasayansi ili chanjo ipatikane mapema. Tumepata mapema, tena tunaanza kuhoji.

Wana wa Mungu, tumshukuru Mungu kwa kuwa amesikia sala na maombi yetu, tukachanjwe..

Nilichanjwa wiki 3 zilizopita. Nilikiuka masharti kidogo, baada ya kuchanjwa sikusubiri dakika 30 kama wanavyoshauri. Kwa sababu nilikuwa safarini, nilchanjwa na kuingia kwenye gari, nikaendesha umbali wa kilometa 600 kwa masaa 8. Nimeendelea na kazi zangu kama kawaida. Bega kidogo lilinisumbua kwa maumivu siku ya pili na ya tatu. Na siku moja nilisikia homa kidogo, otherwise I am perfect 100%.
 
Kwa maneno mengine, chanjo sasa inakwenda kuwa ya lazima. Ni suala la muda tu
 
Chanjo ni hiari ya mtu, mbona anataka kuingilia maamuzi ya Mapadre ? Ingekuwa busara angewaomba.
Anajua anayemtumikia, naye hanaga hiari bali lazima...neno linasema, ataonekana kama kondoo lakini anaongea kama joka...
 
Hata Papa angetamka hilo hadharani Wakatoliki wangempinga hadharani! Askofu nae ni vizuri akakumbushwa mipaka yake. Kwanza kuwaambia mapadre waache utoto ni matusi!

Anawatafuta nini mapadre kama si kulazimisha mgogoro sababu tu ya chanjo? Chanjo imelipasua baraza la maaskofu Calfonia, akasome hiyo habari ili aongozwe kwa hekima.
Hutasikia mgogoro ndani ya wakatoliki.
Mtabwata ninyi makafiri kama gwajima.
Wakatoliki ni level nyingine
 
Bro experience ya ant vaccine protest inayo. Kama mtu unafuatilia juzi Papa aliwaasa watu kuwa chanjo ni salama na ishara ya upendo utesema Papa katoa msimamo wake binafsi au amekuwa manipulated na watu wachache...
Ndio nasema hamjui Ukatoliki ndio maana wengi hutukana wasichojua. Kama msimamo wa papa si msimamo wa Kanisa Katoliki itakuwa Askofu? Unafikiri Papa anaweza kusema ushoga ni halali alafu useme ni msimamo wa Kanisa Katoliki?

Hao ni viongozi na msingi wa maelekezo yao inapaswa yasipingane na mafundisho ya Kanisa. Swala la chanjo ni hiari na haliko chini ya mamlaka yake.
 
Hata Papa angetamka hilo hadharani Wakatoliki wangempinga hadharani! Askofu nae ni vizuri akakumbushwa mipaka yake. Kwanza kuwaambia mapadre waache utoto ni matusi....
Wachungaji wa mshahara wanajulikana...Anadhani ana mamlaka zaidi ya Mungu mwenyewe...
 
Usichanganye Ukatoliki na agizo la Askofu labda hujui Ukatoliki ni nini! Hilo ni agizo lake binafsi kwa muono wake.

He is very wrong bora angekaa kimya na wengine tulifikiri ukimya wao una ujumbe au pengine kuna utafiti wanafanya maana nyenzo wanazo.

Mimi binafsi sikubaliani nae! Kwa ufupi hili agizo na namna alivyolitoa kama umesikiliza mapadre watampinga... Mark my word.
Wewe ndo utampinga ukiwa chumbani na mkeo, mapadri syo wacheza ngoma za kizaramo
 
Chanjo ni hiari ya mtu, mbona anataka kuingilia maamuzi ya Mapadre ? Ingekuwa busara angewaomba.
Agizo la jumla la Serikali ni watu kuwa na uhuru wa kuchanjwa, lakini maelekezo ya taasisi mbalimbali, yapo chini ya taasisi zenyewe.

Mathalani, mtu una uhuru wa kuoa wanawake idadi yote upendavyo, lakini kufanya kazi kwenye taasisi za Kanisa kama Katoliki, unaweza kuambiwa kuwa ni lazima usiwe ja mke zaidi ya mmoja na uwe unashiriki ibada ya sala. Hutaki acha, ukautumie uhuru wako nje ya Kanisa.
 
Hutasikia mgogoro ndani ya wakatoliki.
Mtabwata ninyi makafiri kama gwajima.
Wakatoliki ni level nyingine
Hutasikia mgogoro kama agizo lake litaishia huko alipotamka lakini akilazimisha tutarudi hapa kujadiliana...Mark my word
 
Askofu anatoa agizo mapadre wote wachanjwe? Hata Papa hajatoa agizo popote! Kiukweli hilo agizo linastua sana! Seems ukichanja unatamani kila mtu achanje na wala si tu kwa nia njema bali kibinadamu tuna hulka hiyo...
Soma, sikiliza ili uelewe. Kuna mahali Askofu amesema mapadre waache utoto.

Askofu ameiambia hadhara aliyokuwa akiihubiria, 'tuache utoto'. Askofu ni mwalimu, ni mzazi, ni kuhani, ni mpatanishi na ni mchungaji. Ana mamlaka ya kufundisha, kuelekeza, kuonya na kukaripia.

Yesu mwenyewe alikaripia ilipobidi, Paulo alionya na kukaripia, kwa nini Askofu akikaripia iwe shida? Au huyajui maandiko kabisa?
 
Uko disappointed wewe mwenyewe. Ruwaichi msimamo wake dhidhi ya Corona aliuweka wazi, Mpaka JPM akamnanga Kiaina.. Jamaa alishahimiza sana Tahadhari dhidhi ya covid kitambo.. Huu ni muendelezo
Kwani wapi nimesema "we" vipi wewe?
 
Hata Papa angetamka hilo hadharani Wakatoliki wangempinga hadharani! Askofu nae ni vizuri akakumbushwa mipaka yake. Kwanza kuwaambia mapadre waache utoto ni matusi...
Bro uwe unafuatilia mbona Papa kashazungumza on behalf kuwa watu wachanje kwani chanjo ni salama na ishara ya upendo. I wish you could be informed
 
bro uwe unafuatilia mbona Papa kashazungumza on behalf kuwa watu wachanje kwani chanjo ni salama na ishara ya upendo. I wish you could be informed
Mzee mimi nalala na kuamkia kwenye habari za Kanisa. Tofautisha ushauri na agizo, Papa ameshauri hajatoa agizo! Agizo maana yake ni lazima na Padre ambaye hatochanja maana yake hamtii askofu wake! Akitoka kwa mapadre atatoa agizo kwa waamini wote! Kitu gani hiki?
 
Ni mapadre wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, hao ndio wapo chini ya mamlaka yake. Ingekuwa ni agizo la TEC hapo ndio ingekuwa mapadre wote nchini
Kumbuka huyu ni rais wa Tec
 
Kumbuka huyu ni rais wa Tec
Nani amekwambia ni Rais TEC? Alafu agizo ili liwe ni la TEC lazima liwe limeridhiwa na maaskofu wote na kutolewa kama tamko la baraza. Hili ni tamko kwa mapadre wa jimbo lake
 
Kumbuka huyu ni rais wa Tec
Hapana mkuu! Wewe ni Mkatoliki? Ulipaswa kumjua Rais wa TEC kama ni kweli, vinginevyo utakuwa sio. Rais wa TEC ni Askofu Mkuu Gervas Nyaisonga wa Jimbo la Mbeya
 
Back
Top Bottom