Unapaswa kuelewa MUNGU aliwapa binadamu karama tofauti tofauti kupitia Roho wake Mtakatifu,Madaktari wamepewa karama ya uponyaji-Ni neema ya MUNGU katika kuendeleza uhai miongoni mwa wanadamu.MUNGU anasema tutumie utashi,akili pamoja na maarifa ili tusiangamie na upumbavu.MUNGU hupenda mwanadamu naye ajisaidie kwa njia mbalimbali na awajibike pia kwa mazingira yake.Swali ni je,Kwann tunaambiwa tumtegemee tu MUNGU kwenye magonjwa lakini kwenye CHAKULA tunaambiwa tumwombe MUNGU na tujitume kufanya kazi kwa bidii? Kwann tusijifungie tu ndani na kumwomba MUNGU ili chakula kishuke? Jibu ni kwamba-Maandiko yanasema asiyefanya kazi na asile,hivyo kutokufanya kazi kwa bidii hudhalisha mzizi wa dhambi-kwa sababu uvivu huweza kupelekea wizi na kifo kutokana na njaa.Rais wetu mpendwa aliyemtegemea MUNGU pasipo kuwajibika kibinafsi kwa mazingira yake leo yukwapi? TB Joshua aliyewaaminisha watu mambo ya uwongo kuhusiana na CORONA yukwapi? Penye Sala,juhudi na uwajibikaji MUNGU huonekana.