Dar: Bilioni 44 za Mikopo ya Halmashauri hazijarejeshwa, zimeliwa

Dar: Bilioni 44 za Mikopo ya Halmashauri hazijarejeshwa, zimeliwa

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla, ameagiza kufuatiliwa kwa marejesho ya mikopo ya Halmashauri inayotolewa kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu huku ripoti zikionesha tangu mikopo hiyo ianze kutolewa ni bilioni 18 pekee zimerejeshwa huku bilioni 44 zikiwa hazijarejeshwa.

RC Makalla ameyasema hayo leo Septemba 28, 2022, wakati wa kikao chake na Wakuu wa wilaya, Wakurugenzi, Mameya na wadau wa mikopo hiyo ya Halmashauri huku akihimiza fedha hizo kuwafikia wanufaika waliokusudiwa na serikali.

RC Makalla amesema kuwa, tangu mikopo hiyo ianze kutolewa, mkoa huo katika Halmashauri zake zimekwishatoa zaidi ya bilioni 60.

Chanzo: EastAfrica Tv
pesa zinapotea kwakuwa baadhi ya watumishi wa serikali wanaunda vikundi wanavyoviweka kama daraja la kupiga hela,pia kutoa mikopo kwa uchama hapa ndipo panapoleta hasara.Watumishi wa serikali manispaa wahusikao na mikopo waanze kubanwa.
 
Kumekucha tena !

Screenshot_2024-03-28-15-56-53-1.png
 
Back
Top Bottom