DAR: DART kuondoa tiketi vituo vya Mwendokasi, malipo ya kadi kurejea

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Kampuni ya Emirates National Group kutoka Falme za Kiarabu iliyopata zabuni ya kuendesha mradi wa Mabasi hayo itaanza utaratibu huo Novemba 2022.

Pia, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Usafirishaji wa DART, Fanuel Karugendo amesema wameipa miezi 6 kampuni hiyo kuingiza mabasi mapya na kwa kuanza itaingiza mabasi 177.

Amesema "Majaribio yalifanywa na wataalamu wetu kwa kushirikiana na wataalamu wa mifumo kutoka Colombia na baada ya mwendeshaji mpya kuanza kazi, abiria sasa watatumia kadi, sio tiketi tena".

==========

Wakati njia ya Mbagala ikitarajiwa kuwa na mabasi 750 yatakayosafirisha kati ya abiria 600,000 mpaka 700,000 kwa siku, awamu ya kwanza ya usafiri wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam (Udart), imepata mwekezaji mwingine atakayeboresha huduma katika njia iliyopo sasa hivi.

Kampuni hiyo mpya ya Emirates National Group kutoka Falme za Kiarabu itaingia mkataba na Wakala wa Mabasi Yaendayo haraka (Dart) wiki ijayo, ili kuanza kutoa huduma ikiingiza mabasi mapya 177 yatakayosaidiana na yaliyopo tangu kuzinduliwa kwa mradi huo mwaka 2016.

Tovuti ya kampuni hiyo iliyoanzishwa mwaka 1990 inaonyesha imekuwa ikijishughulisha na kukodisha magari na utoaji wa huduma za usafiri wa umma na binafsi, huku makao makuu yake yapo Abu Dhabi, Falme za Kiarabu.

Ujio wa mabasi hayo 177, Dart imesema kutaongeza uwezo wa kuwahudumia abiria kutoka 200,000 wa sasa hadi abiria 500,000 wanaohudumiwa kila siku na usafiri huo ambao kwa miezi ya hivi karibuni umekuwa ukisuasua kutokana na uchache wa mabasi unaosababisha abiria kukaa vituo kwa muda mrefu.

Juzi, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Usafirishaji wa Dart, Fanuel Karugendo alisema baada ya kutangazwa kwa zabuni, kampuni hiyo ya Kiarabu iliibuka mshindi baada ya kukidhi vigezo vyote.

Ikumbukwe mwendeshaji wa kwanza Udart alikuwa katika majaribio ya mradi huo kwa awamu ya kwanza na kumekuwepo na danadana za muda mrefu za kampata mzabuni mpya kwa takribani miaka mitano sasa.

Akifafanua zaidi hilo, Karugendo alisema mchakato wa kumpata mzabuni huyo ulikuwa wa wazi kupitia Ushirika wa Serikali na Sekta Binafsi (PPP) na baada ya kusaini mkataba huo wiki ijayo atapewa miezi sita kuyaingiza mabasi hayo nchini.

“Ni uamuzi wake, anaweza kuyaleta nusu baada ya kumaliza kusaini mkataba na mengine kuyamalizia ndani ya miezi sita ilimradi tu asivuke muda kama mkataba unavyotaka,” alisema Karugendo.

Utaratibu wa matumizi ya kadi kulipia usafiri huo alisema unarejea baada ya mashine ya majaribio kituo cha Morocco kuwa na ufanisi.

“Majaribio yalifanywa na wataalamu wetu kwa kushirikiana na wataalamu wa mifumo kutoka Colombia na baada ya mwendeshaji mpya kuanza kazi, abiria sasa watatumia kadi, sio tiketi tena. Mfumo huo mpya wa kielektroniki wa kukusanya nauli umetengenezwa na wataalamu wazawa na hivi sasa ndio unatumika kukatia tiketi wakati huu tunaendelea kuleta kadi,” alisema Karugendo.

Shukuru Othuman, mkazi wa jijini hapa alisema wamepata adha ya kutosha, hivyo ujio wa kampuni hiyo unaweza kuboresha huduma.

Eva Thomas naye alisema “tunaomba Mungu mabasi hayo yafike salama, nina imani mambo yatakuwa safi katika huduma.”

Kwa upande wake, Ashura Ngaiza alisema ni “matarajio yangu huduma itakuwa ya kutukuka kuliko ilivyo sasa ambapo watu wanabanana kwenye mabasi kutokana na kutokuwapo usafiri mwingine rahisi na wa haraka katika njia hii baada ya kuondolewa kwa daladala.”

Kicheko Mbagala

Katika hatua nyingine, mradi wa Dart njia ya Mbagala, Karugendo alisema umeshakamilika kwa asilimia 78 na vitu vilivyobaki ni vidogo, vikiwamo vivuko vya Uhasibu, Mbagala Rangi Tatu na Kigogo.

Baada ya kuanza kazi kwa barabara hiyo, alisema mabasi 750 yanatarajiwa kuingia barabarani kusafirisha abiria 600,000 hadi 700,000 kwa siku.

“Idadi hiyo ya mabasi itakuwa ikihudumia barabara zote, zikiwamo zile za mlisho za kuwafikisha abiria vituo vikuu na baadaye kama kutakuwa na uhitaji zaidi tutaongeza,” alisema Karugendo.

MWANANCHI
 
Huu mradi unasaidia sana..tatizo hapo kwenye uendeshaji! Watu wanawaza upigaji na sio kutoa huduma,ngoja tuone huyo muwekezaji mpya.
 
Hapa sasa pesa itaonekana, maana upigaji ulizidi, pesa inaishia mifukoni mwa watu.
Lakini, Hivi kwani kuna uhusiano kati dini ya Rais na dini ya watu wanaopewa zabuni zabuni awamu hii hasa waarabu?
Na je, kampuni hii mpya itayanunua mabasi ya zamani toka kwa kampuni ya zamani?
 
Wenye daladala wajipange serekali inataka kuingilia kila kitu sas biashara za daldalz zitakuwaje ,embu wafikiriewe jmn Ni Bora mngewapa tu hyo njia watumie siyo kila kitu serekal ifanye
 
Muda wa Kulipa Fadhila umefika sasa. Ivi mnafikiri ni jambo Rahisi Rahisi Rangi za Bendera ya Tanzania kuonekana kwenye Jengo kubwa la kibiashara Duniani lililopo Dubai, tena Muda mfupi tu baada ya Chifu Hanganya kutoka huko?
 
Mimi pia huwa nafikiria sana,Kenya wenzetu wanajali sekta binafsi sisi tumegubikwa na fikra za Kikomunisti.
Tunapenda michongo , kila mmoja mjanja nafikiri ndio tulivyolelewa tangu enzi za mchonga, yaani ni michongo kwenda mbele,
Ukimpambanisha kidogo tu chini ila kwa kuchonga tu aaaaah kuanzia maneno mpaka vitendo
 
Hongera sana serikali kwa kuwaweka hao waarabu. Na uhakika kutakuwa na ufanisi na pande zote mbili kufaidika Serikali na mwekezaji. Mmatumbi ukimchekeachekea anakupanda hadi mabegani. Emirates hawana upuuz
 
Hapa sasa pesa itaonekana, maana upigaji ulizidi, pesa inaishia mifukoni mwa watu.
Lakini, Hivi kwani kuna uhusiano kati dini ya Rais na dini ya watu wanaopewa zabuni zabuni awamu hii hasa waarabu?
Na je, kampuni hii mpya itayanunua mabasi ya zamani toka kwa kampuni ya zamani?
Zile paid trip kwenye ME si za kawaida ati
 
Back
Top Bottom