DAR: DART kuondoa tiketi vituo vya Mwendokasi, malipo ya kadi kurejea

DAR: DART kuondoa tiketi vituo vya Mwendokasi, malipo ya kadi kurejea

Yale mabasi ambayo yaliwekewa guarantee na serikali, mwendeshaji wa sasa alishamalizana na serikali kulipa ule mkopo wa NMB!?
Yale ni mabasi ya mradi...
Mwendeshaji atayatumia huku akiilipa serikali na NMB
 
Wenye daladala wajipange serekali inataka kuingilia kila kitu sas biashara za daldalz zitakuwaje ,embu wafikiriewe jmn Ni Bora mngewapa tu hyo njia watumie siyo kila kitu serekal ifanye
Mwendokasi wana barabara zao maalumu
 
Hapa sasa pesa itaonekana, maana upigaji ulizidi, pesa inaishia mifukoni mwa watu.
Lakini, Hivi kwani kuna uhusiano kati dini ya Rais na dini ya watu wanaopewa zabuni zabuni awamu hii hasa waarabu?
Na je, kampuni hii mpya itayanunua mabasi ya zamani toka kwa kampuni ya

Hapa sasa pesa itaonekana, maana upigaji ulizidi, pesa inaishia mifukoni mwa watu.
Lakini, Hivi kwani kuna uhusiano kati dini ya Rais na dini ya watu wanaopewa zabuni zabuni awamu hii hasa waarabu?
Na je, kampuni hii mpya itayanunua mabasi ya zamani toka kwa kampuni ya zamani?
Kwaio umemaind kuona mchongo umeenda kwa muarabu
 
Yale ni mabasi ya mradi...
Mwendeshaji atayatumia huku akiilipa serikali na NMB
Kama mabasi ni ya mradi , nani atakuwa na uchungu nayo!? Maana mwendeshaji anaweza asiyape matunzo ipasavyo, kwani hana hasara nayo. Hii haiwezi kuwa kweli.
 
Hawa waarabu ni mijitu ya hovyo ajabu inapewa tenda kubwa hivi

Tutegemee kifo chw mende
 
Hawa waarabu ni mijitu ya hovyo ajabu inapewa tenda kubwa hivi

Tutegemee kifo chw mende
Kampuni iko pale uae, ila unaweza kuta wamiliki na waendeshaji ni wazungu au hata wahindi, uchumi wa pale umeshikwa na wageni wenyeji wapo wapo tu
 
Wenye daladala wajipange serekali inataka kuingilia kila kitu sas biashara za daldalz zitakuwaje ,embu wafikiriewe jmn Ni Bora mngewapa tu hyo njia watumie siyo kila kitu serekal ifanye
Waende route za pembezoni mwa Jiji, huduma zao ni mbovu mabasi ni machafu, lugha chafu, wanakata muda mrefu vituoni nk. Hata hivyo Wana nafasi ya kuboresha huduma zao, wajifunze kwa wakenya.

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Kama mabasi ni ya mradi , nani atakuwa na uchungu nayo!? Maana mwendeshaji anaweza asiyape matunzo ipasavyo, kwani hana hasara nayo. Hii haiwezi kuwa kweli.
Yeye ndiye operator, yakiharibika atashindwa safirisha watu atafukuzwa
 
Wenye daladala wajipange serekali inataka kuingilia kila kitu sas biashara za daldalz zitakuwaje ,embu wafikiriewe jmn Ni Bora mngewapa tu hyo njia watumie siyo kila kitu serekal ifanye
BRT system ipo ili kuondoa mfumo wa hovyo wa madaladala, wajipange kwenda kutoa huduma nje ya mji, jiji la dar es salaam haliitaji tena ma dala dala
 
Hapa sasa safi naipa heko serikali
Siipendi CCM, simkubali aliyepita na tuliyenaye, lakini panapobidi kusifia tunasifia. Kampuni ipo vema nimeifuatilia binafsi.
Kwa hili heko kwa serikali 👏
 
Waarabu wamepewa waendeshe huu mradi??
 
Waanze kwanza na kuwa na kadi janja vinginevyo kule mbagala ndio watapigwa mpaka watajua hawajui, waswahili uswahili mwingi sana ndiomaana biashara zetu hazifanikiwi
 
Kampuni ya Emirates National Group kutoka Falme za Kiarabu iliyopata zabuni ya kuendesha mradi wa Mabasi hayo itaanza utaratibu huo Novemba 2022.

Pia, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Usafirishaji wa DART, Fanuel Karugendo amesema wameipa miezi 6 kampuni hiyo kuingiza mabasi mapya na kwa kuanza itaingiza mabasi 177.

Amesema "Majaribio yalifanywa na wataalamu wetu kwa kushirikiana na wataalamu wa mifumo kutoka Colombia na baada ya mwendeshaji mpya kuanza kazi, abiria sasa watatumia kadi, sio tiketi tena".

==========

Wakati njia ya Mbagala ikitarajiwa kuwa na mabasi 750 yatakayosafirisha kati ya abiria 600,000 mpaka 700,000 kwa siku, awamu ya kwanza ya usafiri wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam (Udart), imepata mwekezaji mwingine atakayeboresha huduma katika njia iliyopo sasa hivi.

Kampuni hiyo mpya ya Emirates National Group kutoka Falme za Kiarabu itaingia mkataba na Wakala wa Mabasi Yaendayo haraka (Dart) wiki ijayo, ili kuanza kutoa huduma ikiingiza mabasi mapya 177 yatakayosaidiana na yaliyopo tangu kuzinduliwa kwa mradi huo mwaka 2016.

Tovuti ya kampuni hiyo iliyoanzishwa mwaka 1990 inaonyesha imekuwa ikijishughulisha na kukodisha magari na utoaji wa huduma za usafiri wa umma na binafsi, huku makao makuu yake yapo Abu Dhabi, Falme za Kiarabu.

Ujio wa mabasi hayo 177, Dart imesema kutaongeza uwezo wa kuwahudumia abiria kutoka 200,000 wa sasa hadi abiria 500,000 wanaohudumiwa kila siku na usafiri huo ambao kwa miezi ya hivi karibuni umekuwa ukisuasua kutokana na uchache wa mabasi unaosababisha abiria kukaa vituo kwa muda mrefu.

Juzi, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Usafirishaji wa Dart, Fanuel Karugendo alisema baada ya kutangazwa kwa zabuni, kampuni hiyo ya Kiarabu iliibuka mshindi baada ya kukidhi vigezo vyote.

Ikumbukwe mwendeshaji wa kwanza Udart alikuwa katika majaribio ya mradi huo kwa awamu ya kwanza na kumekuwepo na danadana za muda mrefu za kampata mzabuni mpya kwa takribani miaka mitano sasa.

Akifafanua zaidi hilo, Karugendo alisema mchakato wa kumpata mzabuni huyo ulikuwa wa wazi kupitia Ushirika wa Serikali na Sekta Binafsi (PPP) na baada ya kusaini mkataba huo wiki ijayo atapewa miezi sita kuyaingiza mabasi hayo nchini.

“Ni uamuzi wake, anaweza kuyaleta nusu baada ya kumaliza kusaini mkataba na mengine kuyamalizia ndani ya miezi sita ilimradi tu asivuke muda kama mkataba unavyotaka,” alisema Karugendo.

Utaratibu wa matumizi ya kadi kulipia usafiri huo alisema unarejea baada ya mashine ya majaribio kituo cha Morocco kuwa na ufanisi.

“Majaribio yalifanywa na wataalamu wetu kwa kushirikiana na wataalamu wa mifumo kutoka Colombia na baada ya mwendeshaji mpya kuanza kazi, abiria sasa watatumia kadi, sio tiketi tena. Mfumo huo mpya wa kielektroniki wa kukusanya nauli umetengenezwa na wataalamu wazawa na hivi sasa ndio unatumika kukatia tiketi wakati huu tunaendelea kuleta kadi,” alisema Karugendo.

Shukuru Othuman, mkazi wa jijini hapa alisema wamepata adha ya kutosha, hivyo ujio wa kampuni hiyo unaweza kuboresha huduma.

Eva Thomas naye alisema “tunaomba Mungu mabasi hayo yafike salama, nina imani mambo yatakuwa safi katika huduma.”

Kwa upande wake, Ashura Ngaiza alisema ni “matarajio yangu huduma itakuwa ya kutukuka kuliko ilivyo sasa ambapo watu wanabanana kwenye mabasi kutokana na kutokuwapo usafiri mwingine rahisi na wa haraka katika njia hii baada ya kuondolewa kwa daladala.”

Kicheko Mbagala

Katika hatua nyingine, mradi wa Dart njia ya Mbagala, Karugendo alisema umeshakamilika kwa asilimia 78 na vitu vilivyobaki ni vidogo, vikiwamo vivuko vya Uhasibu, Mbagala Rangi Tatu na Kigogo.

Baada ya kuanza kazi kwa barabara hiyo, alisema mabasi 750 yanatarajiwa kuingia barabarani kusafirisha abiria 600,000 hadi 700,000 kwa siku.

“Idadi hiyo ya mabasi itakuwa ikihudumia barabara zote, zikiwamo zile za mlisho za kuwafikisha abiria vituo vikuu na baadaye kama kutakuwa na uhitaji zaidi tutaongeza,” alisema Karugendo.

MWANANCHI
Hivi serikali ndo imeshindwa kufanya biashara yenyewe kama yenyewe mpaka ipate mzabuni?
 
Alaaaa, lakini naona hao watanzania weupe ndio mahodari kwa michongo🤣
Hao waTz weupe hiyo michongo wanayopiga inafanikishwa na sisi waswahili. Kwa kuwa wanaujua udhaifu wetu. Wengi wao wanafaidika kutokana na kuwakumbatia viongozi wanaokula nao.
 
Back
Top Bottom