Dar: David Jairo anadaiwa kupora na kujimilikisha ardhi kinyemela huko Mabwepande

Kadodo1

Member
Joined
Apr 18, 2024
Posts
44
Reaction score
33
ALIYEKUWA Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini katika serikali ya Rais Jakaya Kikwete, David Jairo anadaiwa kupora na kujimilikisha ardhi kinyemela.

Jairo ambaye pia amewahi kuwa Katibu wa rais Kikwete anadaiwa kujimilikisha ardhi kiwanja Namba 1 mpaka 30 kitalu R, ndani ya shamba No.3650 Mtaa wa Mji Mpya Mabwepande, Manispaa ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam.

Kiongozi huyo mstaafu amekiri kumiliki ardhi hiyo na tayari amekwishakabidhiwa hati na Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Mkoa wa Dar es Salaam.

Eneo linalodaiwa kuporwa na Jairo linahusisha eneo lililokuwa likimilkiwa na Jonathan Kaihura, ambalo lilikuwa likipakana naye.

Akizungumza na Pambazuko kwa simu, Kaihura anadai kumiliki eneo hilo tangu mwaka 2004 kutoka iliyokuwa serikali ya kijiji Mabwepande, Kata ya Bunju baada ya serikali kutoa waraka wa kugawa yaliyokuwa mashamba pori ya Dar es Salaam.

Kaihura alisema baada ya kukamilisha ramani yake, mwaka 2015 alifanya utaratibu wa kupata hati miliki ambapo aliandika barua kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni kupitia Serikali ya Mtaa wa Mji Mpya, Kata ya Mabwepande kwa ajili ya kuomba kumilikishwa viwanja vyake.

Alisema baada ya mkurugenzi kujiridhisha alimwandalia rasimu za hati Na 26, 24, 6, 5, 4, 9, 1, 3, 20, 25, 22, 18, 19, 21, 23, 15, 16, 17, 11, na 8 zote za kitalu ‘R’ Mabwepande na alikamilisha malipo ya hati hizo na kugongwa muhuri baada ya kusainiwa na aliyekuwa Ofisa Ardhi Mteule, Jacob Ngowi Mei 19, 2015.

Kwa mujibu wa taratibu za umiliki wa ardhi, rasimu hizo ni nyaraka za awali kwenda kwa Kamishna wa Ardhi kwa ajili ya kuandaliwa hati miliki.

“Ardhi hii niliipata pamoja na mke wangu, Ramla Moshi mwaka 2004 kupitia ugawaji wa ardhi uliofanywa na iliyokuwa serikali ya Kijiji Mabwepande Kata ya Bunju, ambapo tuligawiwa jumla ya ekari tatu na nusu na baadaye nilijenga nyumba na kumweka mlinzi kwenye eneo langu lililopakana na jirani yangu, David Jairo upande wa mashariki ambaye anamiliki zaidi ya ekari 80.

“Mapema mwaka 2015 tulikubaliana na jirani yangu (Jairo) kupima maeneo yetu tukimtumia mpimaji mmoja baada ya Manispaa ya Kinondoni kuendesha zoezi la fidia kwa wamiliki wa mashamba katika eneo hilo na kuandaa mchoro wa mipango miji Na.DSM/KND257/072014 ambao ulikuwa niwa eneo letu lote.

IMG-20250325-WA0290.jpg

Mzee Girian Bukori anayedai kuporwa ardhi na rafikiye David Jairo.

“Aidha mpimaji wetu alikamilisha kazi yake ambapo kila mmoja alilipa gharama zake na mimi nilikabidhiwa ramani yangu Na. El/333/186 kwa usajili No.79626,” alisema Kaihura.

Kaihura alisema akiwa anasubiri kukabidhiwa hati zake, alishtuka kuambiwa kuwa eneo hilo tayari limekwishamilikishwa kwa Jairo kupitia Wizara ya Ardhi bila Manispaa ya Kinondoni kushirikishwa.

Jairo anena haya

Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Jairo alisema taarifa za masuala yote ya umiliki wa ardhi zipo Wizara ya Ardhi, hivyo ni vema wanaotaka kujua zaidi kuhusu suala hilo waende huko.

“Ni nani aliyekwambia huku kuna mgogoro? mimi ni mtu mzima sana, nina miaka 75, ni mstaafu wa serikalini, siwezi kusema kitu ambacho hakipo. Kabla ya kuja kwangu nadhani mngeanzia wizara ya ardhi sio kwangu mimi, wewe kama mwandishi wa habari fanyeni upepelezi wenu msiwe na upande.

“Mwandishi mzuri anakwenda kwenye source (chanzo), na source anayegawa na kutoa hati ni wizara ya ardhi na unajua kabisa custodian (muhifadhi), ni wizara ya ardhi. Lakini pia unaniuliza kitu ambacho kilikwishapita, na hayo maandishi yaliyowekwa kwenye eneo hilo hayajafuata utaratibu wa kisheria,” alisema Jairo.

Baadaye Jairo alimtumia mwandishi nyaraka yenye kumbukumbu Na. LD/327808/16 inayoonyesha inatoka Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Dar es Salaam kwenda kwa Kaihura.

“Baada ya ofisi kupokea barua yako ya tarehe 16 Februari 2022 ukiambatanisha na vielelezo mbalimbali kwenda kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, ikimshauri kusitisha maandalizi ya hati kwenye eneo la viwanja tajwa kwa kuwa kuna uchunguzi wa mgogoro uliokuwa unandelea.

“Baada ya ofisi ya kamishna wa ardhi msaidizi mkoa wa Dar es Salaam kupata barua hiyo yenye Kumb. Na LD/327808/10 ya tarehe 18 Machi 2022 kwenda ofisi ya Takukuru (M) Kinondoni juu ya uchunguzi wa suala hili.

“Kupitia barua yenye Kumb. Na. PCCB/KND/GCR/616/2021 ya April 13, 2022, Ofisi ya Takukuru Mkoa wa Kinondoni iliifahamisha ofisi ya Kamishna wa Ardhi msaidizi mkoa wa Dar es Salaam kuwa uchunguzi uliofanyika juu ya mgogoro wa umiliki wa viwanja husika haukuweza kubaini vitendo vya rushwa kwa mujibu wa sheria ya Takukuru Na.11/2007, hivyo ofisi yake inaendelea kumtambua David Kitundu Jairo kuwa mmiliki halali wa viwanja tajwa,” inasema sehemu ya taarifa hiyo.

Pambazuko lilimtafuta, Kamishna msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Dar es Salaam, Shukrani Kyando ili kutolea ufafanuzi suala hilo. Hata hivyo katibu muhtasi wake alisema yupo nje ya ofisi.

Hata hivyo, mmoja wa makamishna wa ardhi Mkoa wa Dar es Salaam ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa kuwa si msemaji wa suala husika, alisema utaratibu upo wazi kwamba wanatoa hati baada ya kupokea nyaraka kutoka manispaa au halmashauri husika, na endapo kuna hati imetolewa bila kufuata taratibu ikibainika inaweza kubatilishwa.

“Kwa mfano mtu binafsi anapotaka kupima eneo lake kuna fomu ya majirani zake, ofisi ya mtaa, kata na utambuzi huo upo chini ya halmashauri husika kwa kuwa wao ni rahisi kuchunguza na kujua uahalali wa mmiliki wa awali, mauziano yalikuwaje, mwisho wanaandaa nyaraka na kuzileta kwetu kwa ajili ya hati.

“Lakini sheria inaturuhusu endapo ikibainika taratibu hazikufuatwa au kuna mgogoro tunaiondoa hati husika katika daftari la msajili mpaka mgogoro huo uishe, na endapo makosa yanaonekana wazi basi tunaibatilisha moja kwa moja hapo hapo,” alisema.

Aidha Pambazuko lina nakala ya barua yenye Kumb. Na LD/342405 ya Julai 17,2018 ikitoka Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Mkoa wa Dar es Salaam kwenda kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni ikimtaka kufanyia uchunguzi suala la viwanja Na 1 mpaka 27 kitalu R Mabwepande ili kujua uhalali wa umiliki.
jairo1.jpg

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo

Barua hiyo iliyosainiwa na C.S Ntwenya kwa niaba ya Kamishna wa Ardhi mkoa wa Dar es Saaam ilisema: “Ofisi imepokea barua kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu juu ya malalamiko ya ndugu Jonathan Mgisha Kaihura yaliyowasilishwa katika ofisi yake na kuelekezwa kwetu kwa ajili ya utendaji wa suala hilo.

“Kwa kuwa ofisi yako ndiyo yenye mamlaka ya upimaji, upangaji na umilikishaji wa maeneo hayo, ofisi inakutaka ufanyie uchunguzi na utatuzi wa suala la viwanja hivyo kwa haraka na kutuwasilishia kwetu taarifa ili tuweze kuijibu ofisi kuu”.

Septemba 14, 2018 Murugenzi wa Manispaa ya Kinondoni alirudisha majibu yake kwa Kamishna wa Ardhi kwa barua yenye Kumb. Na KMC/LD/64938/13/ES.

Katika majibu ya barua hiyo iliyosainiwa na Geofrey S. Mwamsonjo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni ilisema, kwa mujibu wa nyaraka walizopewa ziliwathibitishia kuwa Kaihura ni mmiliki halali wa eneo hilo na wakati wa upimaji wa viwanja vya Mabwepande watu mbalimbali walilipwa fidia ndani ya shamba Na. 3650 baada ya kufanyiwa utambuzi na kuthibitishwa na uongozi wa serikali ya mtaa.

Barua hiyo inasema, hata hivyo Kaihura hakulipwa fidia na manispaa na kupelekea kupima viwanja vyake akishirikiana na Jairo na kila mmoja alipata ramani kulingana na kipande chake cha ardhi ambapo ramani ya Jairo Na. 79627 ilitoa viwanja 170 na ramani Na. 79626 ya Kaihura ilitoa viwanja 30.

“Tafadhali rejea barua yako yenye Kum. Na.LD/342405/122 ya tarehe 27/7/2018 ambayo uliandika kwetu ukiomba kupatiwa taarifa ya mgogoro uliojitokeza juu ya umiliki wa viwanja hivyo.

“Kwa mujibu wa nyaraka zilizowasilishwa kwetu mwaka 2015 kwa ajili ya maombi ya kumilikishwa viwanja hivyo kutoka kwa ndugu Jonathan M. Kaihura vilikuwa vikimtambulisha kuwa yeye ndiye mmiliki halali baada ya kupewa na halmashauri ya Kijiji cha Mabwepande ili wayaendeleze maeneo hayo ambayo yalijulikana kama mashamba pori.

“Ofisi ilianza taratibu za umilikishwaji wa viwanja hivyo lakini kabla ya zoezi halijakamilika iligundulika viwanja hivyo vimemilikishwa vyote kupitia Ofisi ya Kamishna wa Ardhi kwa ndugu David Jairo wa S.L.P 32156, Dar es Salaam.

“Hivyo ofisi yetu ilisitisha zoezi la kutoa hati miliki kwa ndugu Jonathan Kaihura ili tuweze kujua kwa nini viwanja hivi vipimwe na Jonathan Kaihura na vimilikishwe kwa ndugu David Jairo wakati ndugu Jonathan Kaihura alikwishalipia gharama za umilikishaji,” inasema sehemu ya barua hiyo kwenda kwa Kamishna wa Ardhi Dar es Salaam.

Pabazuko limeona nyaraka kutoka Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Mabwepande, Faki Sultani Mbashiri kwenda kwa mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni yenye Kumb. Na AMK/MBP/VOL29/18, pamoja na mambo mengine ilisema serikali ya mtaa mwaka 2006 waliwahi kusuluhisha mgogoro wa mipaka kati ya Jairo na Kaihura baada ya Jairo kuingia katika eneo la Kaihura mita mbili na kuanza kuweka nguzo za mipaka. Hata hivyo baada ya usuluhishi Jairo aliondoa nguzo hizo na kuziweka sehemu sahihi.

“Pia kumbukumbu zinaonyesha eneo alilokuwa anamiliki Jairo lilikuwa na mashaba matatu yaani, 3651, 3652 na 3653 lote likiwa limezunshwa na nguzo za zege”ilisema taarifa hiyo ya mtendaji.

Mmiliki shamba Na.3650 aibuka

Akizungumza na Pambazuko, mmiliki wa shamba Na.3650 kabla ya kuchukuliwa na serikali ya kijiji, Mzee Giriani Bukori alisema alinunua eneo hilo Septemba 1, mwaka 1999 kutoka kwa Mzee Abdalah Malikuliwa (marehemu).

Alisema upande wa wauzaji ulisimamiwa na mwenye shamba mwenyewe, akiwa na shahidi yake Mzee Abdallah Salum Kimbelete na shahidi wa Mzee Bukori alikuwa ni Jairo.

Mzee Bukori ambaye amelazwa hospitalini kutokana na maradhi mbalimbali, alisema eneo lake lilipakana na Jairo upande wa mashariki na upande mwingine alipakana na mtu mwingine anayemkumbuka kwa jina moja la Mushi pamoja na mto.

“Jairo ni rafiki yangu, nilikuwa msimamizi wake wa ndoa na baba wa ubatizo wa mwanawe, sisi na Jairo ni familia, na alikuwa mkuu wangu wa kazi wakati huo tukiwa wizara ya Nishati na Madini, shamba hilo wakati nalinunua lilikadiriwa kuwa na hekari 12.

Thamani ya ardhi

Katika mahojiano na Pambazuko, baadhi ya wakazi wanaomiliki viwanja katika mitaa ya Mabwepande, Mji Mpya na viunga vyake walida bei ya sasa ya kiwanja chenye ukubwa wa Sq 25 kwa 35 kinauzwa kati ya Shilingi milioni 55 hadi 55 kulingana na ukubwa.

Mashahidi wazungumza

Akiwa nyumbani kwake, Bunju Dar es Salaam, aliyekuwa shahidi wa muuzaji wa shamba hilo linalotambulika kama Na. 3650, Mzee Ally Abdallah Kimbelete aliliambia Pambazuko kuwa anamtambua Mzee Bukori kuwa ni mmiliki halali wa shamba hilo kabla ya kuchukuliwa na serikali ya kijiji na kuligawa kwa watu wengine, akiwemo Kaihura.

“Huyu mtu anayeitwa Jairo sisi huku Mabwepande tunamfahamu kwa jina la utani la ‘mapensi’ kwani mara zote alikuwa akija amevaa vazi hilo na wote tukawa tunamwita jina hilo. Walikuwa wakija na Bukori kama wana kijiji wenzetu na tuliwazoea,” alisema Mzee Kimbelete.

Aidha aliyekuwa mjumbe wa serikali ya kijiji cha Mabwepande wakati huo, Mzee Akili Athuman Maliesi alisema walimuidhinisha Kaihura kuwa mmiliki wa ene hilo kupitia mpango wa kuondoa mapori uliopewa baraka na Serikali ya mkoa wa Dar es Salaam chini ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Wakai uo, Yusuph Makamba na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ritha Mlaki.

“Hata ukinipeleka usiku nitakuonyesha mipaka yote ya maeneo hayo, tunashangaa Jairo kapataje eneo hilo kwani analo eneo lake ambalo kila mmoja wetu analifahamu lakini si kwenye shamba Na. 3650,” alisema Mzee Maliesi.

Aliyekuwa mwenyekiti wa ugawaji wa mashamba pori wakati huo, Hemed Said Ngenje alisema mkutano wa kwanza wa ugawaji mashamba pori ulifanyika Madale Mivumoni chini ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Yusuph Makamba na Rita Mlaki akiwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.

Aidha waraka wa serikali Vol.111/150(b) wa Desemba 31, 1998 kwenda kwa maafisa watendaji wa kata Wilaya ya Kinondoni ulisema kuwa mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam katika ziara yake Desemba 27,1998 iliyohitimishwa kwenye mtaa wa Madale Mivumoni alitoa maagizo kadhaa.

“Maagizo yake ni pamoja na wenye mashamba hayo (mapori) watakiwe kuyalima, nakwa wale wote ambao hawatalima, maeneo yao yagawiwe upya kwa wananchi ambao hawana ardhi ya kulima.

“Barua hii nawaagiza mtekeleze agizo hilo kwa kukagua maneo yote ambayo ni mapori, muyaorodheshe na kuyagawa kwa wananchi wanaohitaji na taarifa ya ukaguzi wa mapori hayo iletwe kwa kumbukumbu ya ofisi. ”ulisema waraka huo wa mku wa Wilaya ya Kinondoni.

Ngenje aliongeza kuwa kupitia gazeti la Mtanzania la Agosti 2002 walitoa muda wa miezi sita kwa wenye mapori kujitokeza na kuyasafisha.

Kupitia gazeti hilo, mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Mabwepande wakati huo, Abdallah Matumla, alisema mashamba yatakayogawiwa ni zaidi ya ekari 150 ili kuitikia wito wa Rais Benjamin Mkapa kuhusu kilimo cha kufa na kupona ambacho pia kilisisitizwa na Bunge ikiwa ni mojawapo ya kupambana na baa la njaa.

Pia aliyepata kuwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mabwepande mwaka 2004 hadi 2019, alisema eneo lenye mgogoro ni sehemu ya shamba Na.3650 ambalo historia yake ya umiliki haina shaka yoyote.

“Kama Jairo anamiliki eneo hilo basi sina hakika kama alishirikisha serikali ya mtaa au hata majirani, hata tulipomuita aje ofisini tuzungumze alikataa, nadhani alituona sisi hatuna hadhi ya kumuuliza chochote”alisema Kunja.

Mkazi mwingine wa eneo hilo, Dustan Gerson alisema eneo lake lilikuwa jirani na Kaihura na alilipwa fidia na Manispaa ya Kinondoni lakini anashangaa mwenzao aliyekataa fidia amenyang’anywa eneo lake.

Pambazuko linaendelea kufuatilia sakata hili kwa kina katika toleo lijalo ambapo Manispaa ya Kinondoni wameahidi kulitolea ufafanuzi suala hilo.
 
Sasa kama wanafuatilia na hawajajua conclusion, iweje habari yao inaonesha kana kwamba Bw Jairo kapora ardhi ya mtu..
 
  • Thanks
Reactions: G4N
Huwa nikitafakari maisha tunayoishi hapa duniana ,halafu unakuta mtu ana ardhi haitumii wala haina chochote ,huwa nasikitika sana kwa kuwa ni liability kwako kama aizalishi chochote then ukifa wanaanza kugawana na kuiuza kama vile wewe uliokota.Kulimikiza ardhi kama sio ya kilimo ni hasara,bora uuze ukiwa na nguvu kanunue bond ule fedha yako taratibu au uanzishe biashara ambayo utawaachia watoto/ndugu wasimalize shule wanatembeza bahasha ya kaki
 
ALIYEKUWA Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini katika serikali ya Rais Jakaya Kikwete, David Jairo anadaiwa kupora na kujimilikisha ardhi kinyemela.

Jairo ambaye pia amewahi kuwa Katibu wa rais Kikwete anadaiwa kujimilikisha ardhi kiwanja Namba 1 mpaka 30 kitalu R, ndani ya shamba No.3650 Mtaa wa Mji Mpya Mabwepande, Manispaa ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam.

Kiongozi huyo mstaafu amekiri kumiliki ardhi hiyo na tayari amekwishakabidhiwa hati na Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Mkoa wa Dar es Salaam.

Eneo linalodaiwa kuporwa na Jairo linahusisha eneo lililokuwa likimilkiwa na Jonathan Kaihura, ambalo lilikuwa likipakana naye.

Akizungumza na Pambazuko kwa simu, Kaihura anadai kumiliki eneo hilo tangu mwaka 2004 kutoka iliyokuwa serikali ya kijiji Mabwepande, Kata ya Bunju baada ya serikali kutoa waraka wa kugawa yaliyokuwa mashamba pori ya Dar es Salaam.

Kaihura alisema baada ya kukamilisha ramani yake, mwaka 2015 alifanya utaratibu wa kupata hati miliki ambapo aliandika barua kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni kupitia Serikali ya Mtaa wa Mji Mpya, Kata ya Mabwepande kwa ajili ya kuomba kumilikishwa viwanja vyake.

Alisema baada ya mkurugenzi kujiridhisha alimwandalia rasimu za hati Na 26, 24, 6, 5, 4, 9, 1, 3, 20, 25, 22, 18, 19, 21, 23, 15, 16, 17, 11, na 8 zote za kitalu ‘R’ Mabwepande na alikamilisha malipo ya hati hizo na kugongwa muhuri baada ya kusainiwa na aliyekuwa Ofisa Ardhi Mteule, Jacob Ngowi Mei 19, 2015.

Kwa mujibu wa taratibu za umiliki wa ardhi, rasimu hizo ni nyaraka za awali kwenda kwa Kamishna wa Ardhi kwa ajili ya kuandaliwa hati miliki.

“Ardhi hii niliipata pamoja na mke wangu, Ramla Moshi mwaka 2004 kupitia ugawaji wa ardhi uliofanywa na iliyokuwa serikali ya Kijiji Mabwepande Kata ya Bunju, ambapo tuligawiwa jumla ya ekari tatu na nusu na baadaye nilijenga nyumba na kumweka mlinzi kwenye eneo langu lililopakana na jirani yangu, David Jairo upande wa mashariki ambaye anamiliki zaidi ya ekari 80.

“Mapema mwaka 2015 tulikubaliana na jirani yangu (Jairo) kupima maeneo yetu tukimtumia mpimaji mmoja baada ya Manispaa ya Kinondoni kuendesha zoezi la fidia kwa wamiliki wa mashamba katika eneo hilo na kuandaa mchoro wa mipango miji Na.DSM/KND257/072014 ambao ulikuwa niwa eneo letu lote.

View attachment 3282763
Mzee Girian Bukori anayedai kuporwa ardhi na rafikiye David Jairo.

“Aidha mpimaji wetu alikamilisha kazi yake ambapo kila mmoja alilipa gharama zake na mimi nilikabidhiwa ramani yangu Na. El/333/186 kwa usajili No.79626,” alisema Kaihura.

Kaihura alisema akiwa anasubiri kukabidhiwa hati zake, alishtuka kuambiwa kuwa eneo hilo tayari limekwishamilikishwa kwa Jairo kupitia Wizara ya Ardhi bila Manispaa ya Kinondoni kushirikishwa.

Jairo anena haya

Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Jairo alisema taarifa za masuala yote ya umiliki wa ardhi zipo Wizara ya Ardhi, hivyo ni vema wanaotaka kujua zaidi kuhusu suala hilo waende huko.

“Ni nani aliyekwambia huku kuna mgogoro? mimi ni mtu mzima sana, nina miaka 75, ni mstaafu wa serikalini, siwezi kusema kitu ambacho hakipo. Kabla ya kuja kwangu nadhani mngeanzia wizara ya ardhi sio kwangu mimi, wewe kama mwandishi wa habari fanyeni upepelezi wenu msiwe na upande.

“Mwandishi mzuri anakwenda kwenye source (chanzo), na source anayegawa na kutoa hati ni wizara ya ardhi na unajua kabisa custodian (muhifadhi), ni wizara ya ardhi. Lakini pia unaniuliza kitu ambacho kilikwishapita, na hayo maandishi yaliyowekwa kwenye eneo hilo hayajafuata utaratibu wa kisheria,” alisema Jairo.

Baadaye Jairo alimtumia mwandishi nyaraka yenye kumbukumbu Na. LD/327808/16 inayoonyesha inatoka Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Dar es Salaam kwenda kwa Kaihura.

“Baada ya ofisi kupokea barua yako ya tarehe 16 Februari 2022 ukiambatanisha na vielelezo mbalimbali kwenda kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, ikimshauri kusitisha maandalizi ya hati kwenye eneo la viwanja tajwa kwa kuwa kuna uchunguzi wa mgogoro uliokuwa unandelea.

“Baada ya ofisi ya kamishna wa ardhi msaidizi mkoa wa Dar es Salaam kupata barua hiyo yenye Kumb. Na LD/327808/10 ya tarehe 18 Machi 2022 kwenda ofisi ya Takukuru (M) Kinondoni juu ya uchunguzi wa suala hili.

“Kupitia barua yenye Kumb. Na. PCCB/KND/GCR/616/2021 ya April 13, 2022, Ofisi ya Takukuru Mkoa wa Kinondoni iliifahamisha ofisi ya Kamishna wa Ardhi msaidizi mkoa wa Dar es Salaam kuwa uchunguzi uliofanyika juu ya mgogoro wa umiliki wa viwanja husika haukuweza kubaini vitendo vya rushwa kwa mujibu wa sheria ya Takukuru Na.11/2007, hivyo ofisi yake inaendelea kumtambua David Kitundu Jairo kuwa mmiliki halali wa viwanja tajwa,” inasema sehemu ya taarifa hiyo.

Pambazuko lilimtafuta, Kamishna msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Dar es Salaam, Shukrani Kyando ili kutolea ufafanuzi suala hilo. Hata hivyo katibu muhtasi wake alisema yupo nje ya ofisi.

Hata hivyo, mmoja wa makamishna wa ardhi Mkoa wa Dar es Salaam ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa kuwa si msemaji wa suala husika, alisema utaratibu upo wazi kwamba wanatoa hati baada ya kupokea nyaraka kutoka manispaa au halmashauri husika, na endapo kuna hati imetolewa bila kufuata taratibu ikibainika inaweza kubatilishwa.

“Kwa mfano mtu binafsi anapotaka kupima eneo lake kuna fomu ya majirani zake, ofisi ya mtaa, kata na utambuzi huo upo chini ya halmashauri husika kwa kuwa wao ni rahisi kuchunguza na kujua uahalali wa mmiliki wa awali, mauziano yalikuwaje, mwisho wanaandaa nyaraka na kuzileta kwetu kwa ajili ya hati.

“Lakini sheria inaturuhusu endapo ikibainika taratibu hazikufuatwa au kuna mgogoro tunaiondoa hati husika katika daftari la msajili mpaka mgogoro huo uishe, na endapo makosa yanaonekana wazi basi tunaibatilisha moja kwa moja hapo hapo,” alisema.

Aidha Pambazuko lina nakala ya barua yenye Kumb. Na LD/342405 ya Julai 17,2018 ikitoka Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Mkoa wa Dar es Salaam kwenda kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni ikimtaka kufanyia uchunguzi suala la viwanja Na 1 mpaka 27 kitalu R Mabwepande ili kujua uhalali wa umiliki.
View attachment 3282771

Hizi porojo zote kuna mtu anaweza kusoma kwl. Jairo ana hati bado mnaandika amepora, huu ni udhalilishaji tu.
 
Haramu haijawahi kuwa halali,bali itaendelea kuwa haramu tu,mana hati ambayo imepatikana kwa njia za Kinyanganyi lazima itaendelea kuwa batili,,,,,,
YAANI Lazima binadamu uwe na roho ngumu na ujasiri wa kutosha Kumdhurumu MSIMAMIZI WAKO WA NDOA TAKATIFU NA BABA WA KIROHO WA WATOTO WAKO,,,,,
Kweli tamaa ya mali inaua utu wa mwanadamu.
 
Endapo kama Maelezo haya yana Ukweli Kama hivyo yalivyowasilishwa, basi hizo Hati-miliki za Ardhi za huyo Jairo kuhusiana na hivyo Viwanja Na.1 - 30 Kitalu "R" huko Mabwepande zitakuwa zina UBATILI. Upatikanaji wa Miliki za Viwanja hivyo umegubikwa na vitendo vya udanyanyifu na uvunjaji wa Taratibu za Kisheria za Umilikishaji wa Ardhi. Hivyo, miliki za Ardhi za viwanja hivyo ni Batili kwa mujibu wa Sheria, zinapaswa Kutenguliwa (Revoked).

Aidha, Wizara ya Ardhi haikupaswa kutoa Hati-miliki za Viwanja hivyo bila ya kuwasiliana kwanza na Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ambako Ardhi husika ilipo. Inavyoonekana hizo miliki za Ardhi zilizotolewa kwa huyo Jairo kuwa ni MILIKI PANDIKIZI (Double Allocations), hivyo ni batili kwa ujumla wake tangu Siku zilipotolewa, null and void ab initial!

Njiia iliyo rahisi zaidi ili kutatua Mgogoro huo ni kwa Afisa Ardhi Mteule au Kamishina wa Ardhi kumtumia HATI YA MASHITAKA huyo Jairo kumtaka AJIELEZE KWA MAANDISHI, kwamba ni Kwa Nini Hati-miliki za Viwanja hivyo ZISITENGULIWE baada ya Mmiliki huyo kumilikishwa kwa njia za Udanganyifu???
Ni kwamba Viwanja hivyo vilimilikishwa kwake baada ya yeye Jairo kufanya vitendo vya Udanganyifu, kughushi Nyaraka pamoja na kushiriki vitendo vingine viovu kinyume na Sherria, Kanuni na Taratibu za Umilikishaji wa Ardhi ili kujipatia Miliki za Ardhi kwa viwanja hivyo tajwa.
 
Huyo aliyeporwa ardhi aende Ngende au Mlingotini. Anakubalije kuporwa ardhi yake kirahisirahisi hivyo?
 
Africa mtu anaingia kwenye system ya ajira serikalini hili akavune utajiri na sio vinginevyo.
 
Mheshimiwa Jairo ndiye mmiliki ardhi husika kihalali kwa mujibu wa sheria za Ardhi

Endapo kama kweli Maelezo haya yana Ukweli, Basi umiliki wa Ardhi hiyo kwa huyo Jairo una walakini mkubwa sana, kuna chembechembe za UBATILI ndani yake. Umiliki wake utakuwa siyo halali, unless Maelezo haya yasiwe na Ukweli ndani yake.
 
Hizi porojo zote kuna mtu anaweza kusoma kwl. Jairo ana hati bado mnaandika amepora, huu ni udhalilishaji tu.

Unaweza ukawa una Hati-miliki ya Ardhi lakini Hati hiyo inaweza kuwa siyo Halali kwa mujibu wa Sheria kutokana na sababu mbalimbali.
Aidha, yawezekana Hati hiyo umeipata kwa njia zisizo Halali au Hati hiyo ni ya kughushi, n.k. Yote haya yanaweza kusababisha Hati ya umiliki wa Ardhi kuwa batili. Illegalities katika Hati-miliki za Ardhi zipo nyingi sana kutokana na sababu mbalimbali.

Kila jambo lina Taratibu zake!

Mathalani, ili Mwanamke aweze kujifungua Mtoto ni lazima kwanza Mwanamke huyo abebe ujauzito, endapo kama itatokea ghafla tu from nowhere Mwanamke akawa ana mtoto lakini muda mfupi hapo kabla hakuwahi kubeba ujauzito, Basi kwa vyovyote vile itakavyokuwa Mwanamke huyo lazima atakuwa ana Hoja ya Kujibu. Mwanamke huyo ni LAZIMA AELEZE huyo Mtoto amempata wapi i-hali kwamba hakuwahi kubeba ujauzito!??
 
Haramu haijawahi kuwa halali,bali itaendelea kuwa haramu tu,mana hati ambayo imepatikana kwa njia za Kinyanganyi lazima itaendelea kuwa batili,,,,,,
YAANI Lazima binadamu uwe na roho ngumu na ujasiri wa kutosha Kumdhurumu MSIMAMIZI WAKO WA NDOA TAKATIFU NA BABA WA KIROHO WA WATOTO WAKO,,,,,
Kweli tamaa ya mali inaua utu wa mwanadamu.
Absolutely!

Once illegal is always illegal!
 
Kama kuna DHAHABU atuambie, sasa ardhi yote hiyo mtu mmoja anataka kuifanyia nini? Akiiba changu atavimba tumbo.
 
Back
Top Bottom