Dar: DC Gondwe ashindwa kuwalinda waliompa taarifa za Siri, wote waachishwa kazi

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,132
Reaction score
64,416
Salaam Wakuu,

Mkuu wa Wilaya Godwin Gondwe alipokuwa Mkuu wa Wilaya Temeke, kulikuwa na Mgogoro Hospitali ya Dar Group.

Gondwe akaitembelea, na kuwaambia Wafanyakazi na Madaktari wafunguke matatizo yao kwamba atawalinda. Watu wakajiachia.

Leo kahamishwa Wilaya kapewa Jokate. Wote walioongea hivi sasa hawana kazi. Wanaambiwa nendeni kwa Gondwe.

Maboss wa Dar Group wamekuwa Wakali. Wanajitapa balaa.

Je, Gondwe atawasaidia tena? Au ndo basi yaishe?

Thread 'Mgomo wa Madaktari na Wafanyakazi wa hospitali ya Dar group (T.O.H.S) kuanza Februari 14' Mgomo wa Madaktari na Wafanyakazi wa hospitali ya Dar group (T.O.H.S) kuanza Februari 14
 
Kufanya Kazi private sector ni changamoto so waende tena kwake Ili awasaidie kupata stahiki zao kama hawajapata baada ya kuachishwa Kazi.
 
Uongozi ni karama
 
Hao waliotoa siri kama waliambiwa "wafunguke" kama ulivyoandika kwenye uzi wako, nao "wakafunguka" kweli mbele za watu wapewe pole.

Kwangu wangetakiwa watoe hizo taarifa kwa siri, ili kama zikija kuvuja, hapo ndio alaumiwe Gondwe, coz yeye ndie alipewa personally.
 
Kwani nchi haina sheria?

Huyo Gondwe ni Mungu-mtu au mtetezi wa wanyonge?

Ajiri wakili uende kortini ukapambane.
 
Gondwe hana Msaada tena kwa hao Waliofukuzwa
 
Upumbav wao tu, yaaan ufanye kaz tena private sector umseme muajiri wako kwa serikal halafu utegemee ubaki kazini...? Hata ningekua mimi ningewafukuza kazi. Vijana hata ugekua unafanya kazi serikalini ambapo Job Security ni 90% ambapo unaweza kulopoka chochote na usifanywe kitu, kamwe usiingie ktk huo mtego eti funguka nitawalinda...
 
Kwani nchi haina mahakama?
Sasa unafanya kazi binafsi ukiachishwa unaenda mahakamani ili mahakama imlazimishe huyo mtu akuajiri?
Sheria za private sector zinataka mwajiri akulipe mshahara wa mwezi mmoja ambao hujaufanyia kazi, kama walilipwa mahakamani waende kudai nini?
 
Mi huwa sielewi kwanini wewe una kampuni, unapata faida unakuwa mchoyo wa kugawana faida na wenzako, unawafanya wafanye kazi mazingira magumu na unawafanya kama watumwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…