Dar: DCEA yakamata Energy drink zenye kemikali ya Bangi

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
459
Reaction score
644
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imebaini na kukamata makopo 122 ya vinywaji vya kuongeza nguvu (energy drinks) vyenye kemikali ya THC, inayopatikana kwenye dawa za kulevya aina ya bangi, katika operesheni iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Vinywaji hivyo vyenye chapa ya TRIP, vyenye ujazo wa mililita 250 kila kopo, sawa na lita 30.5, vilikamatwa baada ya DCEA kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) kufanya ukaguzi katika duka la Village Supermarket.

Akizungumza na waandishi wa habari Julai 02, 2026, Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo, amesema katika operesheni hiyo watuhumiwa wawili, Syed Abdul Bast (43), raia wa Pakistan, na Dhirendra Kumar Gorodhan (45), Mtanzania mwenye asili ya Asia, walikamatwa na hatua za kisheria zinaendelea.

DCEA imeeleza kuwa kemikali ya THC inaweza kusababisha madhara mbalimbali kwa mtumiaji, ikiwemo kuamsha magonjwa ya akili, kubadili utendaji wa mfumo wa fahamu, kuchochea vitendo vya uhalifu na matumizi ya dawa nyingine za kulevya.

Hata hivyo, tukio hilo ni sehemu ya mafanikio ya operesheni zilizofanyika nchini kote kati ya Mei na Juni 2026, ambapo jumla ya tani 22.6 za dawa za kulevya, lita 30.5 na kilogramu 19.94 za dawa tiba zenye asili ya kulevya zilikamatwa.
 
Ubabaishaji,uonevu na fitina za Kibiashara tu.Kwamba kuna kinywaji ukikinywa unapata hamu ya kwenda kufanya uhalifu!!!!????.CCM ni hatari sana.
Watafute Mawakili wazuri ,watashinda kesi.
Kama vina bangi huwa inasemwa mvuta bangi huwa na kujiamini kulikopitiliza so mtu anaweza akakwepa kuvuta bangi akakutana nayo kwenye energy drink akaenda kufanya vitu vya ajabu.

Japo sipingani na wewe ila hivyo vinywaji vipo pia ktk list ya vinywaji vinavyosababisha magonjwa yasiyo ya kuambukiza shinikizo la damu presha etc
 
Chupa 112 zinaweza kuonekana nyingi, lakini bado hatuwezi kujua zilikuwa za matumizi binafsi au za biashara. Inawezekana walizoea kutumia bidhaa hizo walikotoka na walipoingia Tanzania wakajaribu kuziagiza kinyemela. Hata hivyo, hilo ni uwezekano tu; ukweli utategemea matokeo ya uchunguzi wa mamlaka husika.
 
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imebaini na kukamata makopo 122 ya vinywaji vya kuongeza nguvu (energy drinks) vyenye kemikali ya THC, inayopatikana kwenye dawa za kulevya aina ya bangi, katika operesheni iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Vinywaji hivyo vyenye chapa ya TRIP, vyenye ujazo wa mililita 250 kila kopo, sawa na lita 30.5, vilikamatwa baada ya DCEA kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) kufanya ukaguzi katika duka la Village Supermarket.

Akizungumza na waandishi wa habari Julai 02, 2026, Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo, amesema katika operesheni hiyo watuhumiwa wawili, Syed Abdul Bast (43), raia wa Pakistan, na Dhirendra Kumar Gorodhan (45), Mtanzania mwenye asili ya Asia, walikamatwa na hatua za kisheria zinaendelea.

DCEA imeeleza kuwa kemikali ya THC inaweza kusababisha madhara mbalimbali kwa mtumiaji, ikiwemo kuamsha magonjwa ya akili, kubadili utendaji wa mfumo wa fahamu, kuchochea vitendo vya uhalifu na matumizi ya dawa nyingine za kulevya.

Hata hivyo, tukio hilo ni sehemu ya mafanikio ya operesheni zilizofanyika nchini kote kati ya Mei na Juni 2026, ambapo jumla ya tani 22.6 za dawa za kulevya, lita 30.5 na kilogramu 19.94 za dawa tiba zenye asili ya kulevya zilikamatwa.
Tunaomba picha ya "packaging" ya hicho kinywaji muonekano wa chupa nk kama kuna uwezekano wa kuipata.
 
Hata hivyo, tukio hilo ni sehemu ya mafanikio ya operesheni zilizofanyika nchini kote kati ya Mei na Juni 2026, ambapo jumla ya tani 22.6 za dawa za kulevya, lita 30.5 na kilogramu 19.94 za dawa tiba zenye asili ya kulevya zilikamatwa.
Matumizi mabaya ya ''hata hivyo''. Matokeo ya shule za kukariri. Watu wanadhani ukiandika habari ni lazima uweke ''hata hivyo''. Elimu yetu imekuwa janga badala ya ukombozi. Hata vyombo vya habari vikubwa huwa wanafanya hili kosa.
 
Ubabaishaji,uonevu na fitina za Kibiashara tu.Kwamba kuna kinywaji ukikinywa unapata hamu ya kwenda kufanya uhalifu!!!!????.CCM ni hatari sana.
Watafute Mawakili wazuri ,watashinda kesi.
Usifanye kichwa chako kuwa kigumu.
Na DCEA hawako kwaajili ya kukandamiza biashara za watu plus ni mamlaka zaidi ya moja zilizoshirikiana kufanya Hilo zoezi. Na ni zoezi jema kabisa.
#Binadamu hamna shukrani
 
Aliye kuroga ni nani mpaka unaamini kuna jema chini ya CCM hii!!!???Basi hiyo kemikali ya kuchochea uhalifu itakuwa inapatikana CCM pale Lumumba,ndiyo huwa mnawanywesha Polisi-CCM maana ndiyo wahalifu,wanateka watu na kuwaua?.
 
THC, unaifahamu?
 
Back
Top Bottom