Dar: Dunstan Daudi Mutajura adaiwa kutekwa eneo la Buza

Dar: Dunstan Daudi Mutajura adaiwa kutekwa eneo la Buza

Poppy Hatonn

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2021
Posts
3,095
Reaction score
4,632
Nimepokea taarifa usiku huu kutoka kijijini Kishanje, Bugabo Bukoba, akitaarifu kutekwa kwa kijana Danstan Daudi Mutajura (pichani juu) anayefanya kazi Jijini Dar es Salaam.

Dastan ametekwa jana majira ya saa 4 asubuhi maeneo ya Sigara, TANESCO, Buza Jijini Dar es Salaam wakati akienda kazini kwake akitokea nyumbani kwake eneo la Kitunda, Jijini Dar es Salaam.

Kupata matukio ya nyuma kuhusu watu wasiyojulikana ingia hapa: Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Dastan ametekwa na WATU WASIOJUKIKANA baada ya gari alilokuwa akiendesha (T.109 DYV) aina ya Mercedes Benz C300 kuzuiwa kwa mbele na gari la watekaji.

Baadaye gari la Danstan liliokotwa na kupelekwa Kituo cha Kidogo cha Polisi cha Buza na kuandikishwa kama MALI YA KUOKOTWA RB NO. BZA/RB/53/2025

Madereva wa bodaboda walioshugudia tukio hilo wamesema Danstan alinyofolewa kutoka kwenye gari lake na kufungwa Kitambaa usoni akilalamika kuwa alikuwa akitekwa.

20250105_105315.jpg
 
Kundii baya sanaa hiloo
..ukute huyu wakili wa Boni Yai au anasaidia CDM huko.....shidaaaa....asingefungua mlango wa gariii
Kama kweli ni Wakili basi naweza kukubaliana na mtazamo wako.
Yawezekana huenda alikuwa anawafanyia mentoring ya kisheria Watu wa vyama vya Upinzani hususani Chadema. Mwanga wa 'MOTIVES' zilizosababisha kutekwa kwake umeanza kuonekana
 
Back
Top Bottom