Dar: Dunstan Daudi Mutajura adaiwa kutekwa eneo la Buza

Dar: Dunstan Daudi Mutajura adaiwa kutekwa eneo la Buza

Nimepokea taarifa usiku huu kutoka kijijini Kishanje, Bugabo Bukoba, akitaarifu kutekwa kwa kijana Danstan Daudi Mutajura (pichani juu) anayefanya kazi Jijini Dar es Salaam.

Dastan ametekwa jana majira ya saa 4 asubuhi maeneo ya Sigara, TANESCO, Buza Jijini Dar es Salaam wakati akienda kazini kwake akitokea nyumbani kwake eneo la Kitunda, Jijini Dar es Salaam.

Kupata matukio ya nyuma kuhusu watu wasiyojulikana ingia hapa: Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Dastan ametekwa na WATU WASIOJUKIKANA baada ya gari alilokuwa akiendesha (T.109 DYV) aina ya Mercedes Benz C300 kuzuiwa kwa mbele na gari la watekaji.

Baadaye gari la Danstan liliokotwa na kupelekwa Kituo cha Kidogo cha Polisi cha Buza na kuandikishwa kama MALI YA KUOKOTWA RB NO. BZA/RB/53/2025

Madereva wa bodaboda walioshugudia tukio hilo wamesema Danstan alinyofolewa kutoka kwenye gari lake na kufungwa Kitambaa usoni akilalamika kuwa alikuwa akitekwa.

View attachment 3192960
Wameanza tena 🙌🏿🙌🏿🙌🏿🏃🏿🏃🏿🏃🏿
 
Kutekana kwa ransom au sababu zingine zozote ni aina ya ujambazi unaosambaa kwenye miji mikubwa.Kwa Dar es salaam bado linaonekana jambo geni.
Nairobi imekuwa jambo linalosumbua vyombo vya usalama na mpaka mwishoni wa mwaka 2024 watu 85 wametekwa na baadhi yao kuuwawa.Imekuwa jambo la kawaida wafanyabiashara na watu watu mashuhuri kuwa na, walinzi binafsi.
Johanessburg utekaji na car jacking ni maisha ya kila siku kwa wakazi wa Jiji hilo.
Polisi lazima waanze kufanya kazi ya kuzuia hii hali isiendelee kabla ya kuzoeleka na kuwa sehemu ya maisha.
Kipindi cha nyuma humu nilishawahi kusema,haya mambo ya utekaji yanayofanywa na watu wa mfumo...kuna watu nao wataanza kupita na upepo wake
Nao watatumia njia hizo hizo kuteka

Ova
 
Nimepokea taarifa usiku huu kutoka kijijini Kishanje, Bugabo Bukoba, akitaarifu kutekwa kwa kijana Danstan Daudi Mutajura (pichani juu) anayefanya kazi Jijini Dar es Salaam.

Dastan ametekwa jana majira ya saa 4 asubuhi maeneo ya Sigara, TANESCO, Buza Jijini Dar es Salaam wakati akienda kazini kwake akitokea nyumbani kwake eneo la Kitunda, Jijini Dar es Salaam.

Kupata matukio ya nyuma kuhusu watu wasiyojulikana ingia hapa: Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Dastan ametekwa na WATU WASIOJUKIKANA baada ya gari alilokuwa akiendesha (T.109 DYV) aina ya Mercedes Benz C300 kuzuiwa kwa mbele na gari la watekaji.

Baadaye gari la Danstan liliokotwa na kupelekwa Kituo cha Kidogo cha Polisi cha Buza na kuandikishwa kama MALI YA KUOKOTWA RB NO. BZA/RB/53/2025

Madereva wa bodaboda walioshugudia tukio hilo wamesema Danstan alinyofolewa kutoka kwenye gari lake na kufungwa Kitambaa usoni akilalamika kuwa alikuwa akitekwa.

View attachment 3192960
Taka taka za wanaume wa Dar,pumbafu na nusu ,mtu ametekwa mbele yenu mnaona hata kufuatilia ilo gari mmeshndwa?
 
Suala la Kudhibiti utekaji na Watekaji siyo kazi rahisi hata kidogo kama unavyofikiri, Kumbuka, hao Watekaji ni Watu Wabobevu na Wataalamu wakubwa kwenye kazi hizo za Kuteka Watu, wamesomea darasani na kupata Mafunzo ya Umahiri kuhusiana na shughuli hizo za Utekaji ( Professional Abductors/Kidnappers). Zinahitajika nguvu kubwa sana na za ziada pamoja na Wananchi kuwa tayari kujitolea muhanga ili kupambana na hao Watekaji sambamba na kuvikomesha kabisa vitendo hivyo vya utekaji na Watekaji wenyewe.
Narudia tena kusema, kudhibiti Watekaji siyo kazi rahisi hata kidogo.
Wakamteke ridhiwani tuone kama watachelewa kukamatwa.
 
Dr Ulimboka alitekwa na Magufuli?! Mtalia na Magufuli hadi mwaka 2125.
Maswali sii kuwa nani alitekwa na nani ila kwanini utekaji ni zaidi wakati fululani na katika nyakati fulani na akiwepo fulani au fulani?
 
Back
Top Bottom