Dar: Emmanuel Kalungwana kortini kwa wizi wa Mita za Maji za DAWASA

Dar: Emmanuel Kalungwana kortini kwa wizi wa Mita za Maji za DAWASA

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Emmanuel Kalungwana mkazi wa Mbezi Africana, amefikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Kinondoni kujibu shtaka la kuingilia miundombinu ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) ambalo ni kosa la uhujumu uchumi

Kalungwana amefikishwa Mahakamani hapo na kusomewa shtaka lake na wakili wa Serikali, Salima Jafari mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Ramadhani Rugemalira.

Wakili wa Serikali alidai kuwa mshtakiwa anadaiwa kuiba dira za maji (Mita 3) eneo la Wazo akiwa na lengo la kuziuza ili kujipatia fedha.

Mshtakiwa huyo anadaiwa kutenda kosa hilo tarehe 2 Agosti,2024.

Mshtakiwa baada ya kusomewa shtaka hilo amerudishwa mahabusu baada ya kushindwa masharti ya dhamana ambayo ni kiasi cha Shilingi laki tano (500,000) na wadhamini wawili.

Upande wa mashtaka umedai kuwa upelelezi bado haujakamilika. Baada ya kusomewa shtaka hilo, hakimu Rugemalila aliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 2,2024.

Hata hivyo, kwa mujibu Sheria ya Maji Namba 5 ya mwaka 2019 Kifungu cha 61 kinaelekeza faini isiyopungua 500,000 na isiyozidi 50,000,000,au Kifungo kuanzia miaka miwili isiyozidi miaka mitano au vyote faini na kifungo kwa pamoja.

Pia soma:

KERO - √ - Wizi wa mita za maji Mbezi Mtaa wa Luis (Upendo)

KERO - Wizi wa mita za maji washamiri Mbweni Teta, DAWASA wapo kimya

DOKEZO - √ - Wizi wa mita za maji, mita hizi zinapelekwa wapi?
 
Dah jamaa karudi mahabusu kwa kukosa wadhamini wawili na laki 5 tu!

Huyu jamaa akitoka kwenye hayo matatizo anatakiwa ajitafakari sana kuhusu ndugu,jamaa na marafiki wanaomzunguka,

Afanye kazi ya halali kwa bidii sana ili ajikwamue atoke kwenye hayo maisha,atambue kua maisha yake ni yake na hakuna mtu wa kumsaidia,

Sometimes hua tunajua thamani ya watu waliotuzunguka pale tu tunapofikwa na matatizo.
 
Tz ukitaka ibaa hela nyingi
Sasa huoni huyo yuko mahakamani kinyonge tena peku

Ova
 
Back
Top Bottom