Viongozi wa Chama Cha Wamiliki wa Daladala Dar es Salaam (DACOBOA) wamekutana na Viongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) leo 10 Desemba, 2024 kutoka Idara ya Elimu kwa Mlipakodi na Mawasiliano na kufanya nao mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya kikodi kuhusu usafirishaji wa abiria ndani ya Jiji la Dar es Salaam.