Uchaguzi 2020 Dar es Salaam imepatwa na nini? Mbona mpo tuli?

Uchaguzi 2020 Dar es Salaam imepatwa na nini? Mbona mpo tuli?

Juzi Mgombea ubunge Jimbo la Ubungo kwa Tiketi ya CCM alifanya mkutano na wanaCCM katika Ukumbi wa Banora,Mlimani City.Wafuasi wengi walienda wakitegemea kupewa chochote,waliishia kupewa maji ya Mia tatu.Waliouliza mambo ya mshahara walijibiwa Kama mshahara hautoshi acha kazi waajiriwe wengine.WanaCCM Dar mwaka huu wapo baridiiiiiiiiiiii hamna umateumate.Tusubiri tarehe 28/10
 
Kama mji mkuu Tanzania kwa hadhi na historia, jiji la Dar ndio lango la mambo yote, yawe mazuri au mabaya.

Ni kweli Dar ni bandari salama ila sio kwa kupoa huku kwenye vuguvugu hili la mabadiliko.

Sijaona zile vibe za 2010 kipindi cha Dr. Slaa Vs Kikwete. Sijaona vibe za 2015 kipindi cha Mh Edward Lowasa Vs Dr. JPM

Jiji na viunga vyake vyote ilikua mshikemshike nguo kukauka nikuvae, ila this time, watu wako busy na issue zao tu.

Sijui ni hasira zimewajaa mzee wa kaya alivyoziba mirija kwa miaka 5?

Please, tunapoelekea week 4 za mwisho, tunataka kuona mchango wa jiji kubwa katika harakati za kuwa na taifa lenye muelekeo wa kisera na kimifumo ya taasisi za kiutawala, na maendeleo.
watu wa Dar tupo kimya na vichinjio vyetu hatuna shobo!
 
Kwani hukuona ilivyokuwa huko Kawe mshike mshike ulivyokuwa kati ya mmiliki mapepo na huyo bibi? Bibi alipigwa knock out. Huko kwenye majimbo mengine nako walipigwa knock out mapema na hivyo ligi ilishamalizika mapema.
Itakuwa miongoni mwa waliopigwa upofu. Mmiliki mapepo amegeuka kuwa pepo! Huyo sio size ya Halima Mdee. bahati nzuri ni kwamba Kawe hawaishi misukule...
 
Ukichunguza zaidi utagundua kwamba wagombea wa ccm hapo DSM ndio wanaoongoza kwa kuchukiwa na wananchi

1601466490583.png

1601466857081.png

apo vp
 
Hongereni Dar mmejitambua mmeachana na waongo na matapeli wa siasa ya tundu Lisu na mbowe.
 
Kama mji mkuu Tanzania kwa hadhi na historia, jiji la Dar ndio lango la mambo yote, yawe mazuri au mabaya.

Ni kweli Dar ni bandari salama ila sio kwa kupoa huku kwenye vuguvugu hili la mabadiliko.

Sijaona zile vibe za 2010 kipindi cha Dr. Slaa Vs Kikwete. Sijaona vibe za 2015 kipindi cha Mh Edward Lowasa Vs Dr. JPM

Jiji na viunga vyake vyote ilikua mshikemshike nguo kukauka nikuvae, ila this time, watu wako busy na issue zao tu.

Sijui ni hasira zimewajaa mzee wa kaya alivyoziba mirija kwa miaka 5?

Please, tunapoelekea week 4 za mwisho, tunataka kuona mchango wa jiji kubwa katika harakati za kuwa na taifa lenye muelekeo wa kisera na kimifumo ya taasisi za kiutawala, na maendeleo.
Wewe unaishi wapi kwani ni vibe gani unataka ivi umekatisha mitaani huko au upo kwenye mitandao ila ukiotaka kujua dar wapi vizuri subiri Magufuli aje kufanya kampeni dar ndio itakua mjomba wamepita hao watu wa blablaa na hatukustuka wala nn tupate kanda ndugu uone mambo.
 
Back
Top Bottom