Miaka ya 2004 kushuka chini kulikuwa na watu wa kawaida sana waliotamba kwa umaarufu pamoja na majina yao.
Nakumbuka wachache ila mtaweza kuongeza.
Mimi na mkumbuka Baba Rama mwenye mikokoteni iliyokuwa na jina lake.
Ili kuwa maeneo ya kuanzia urafiki,manzese,kagera,tandale na mabibo.
Mwengine alikuwa bingwa wa kuandika ukutani sijui mda alikuwa anatoa wapi 😄.
Huyu sehemu za ukuta anaandika jina lake "Rama kapita" kwa wale mliokuwa mnaishi mabibo sio wageni.
Kuna mwengine alikuwa maarufu za kwa kutuma salamu redioni anaanza "Niambrieeeeeeeeeeee" .
Mwengine chesko mzee wa matunda kipindi hicho clouds hipo moto.