Dar es salaam limegeuka jiji la makelele, Serikali imelala?

Sasa ukutane na daladala zile aina ya Eicher zina honi kali sana ambayo inaweza ikamuua mwenye ugonjwa wa moyo !
Wenyewe hata habari hawana !
Labda nayo hii inaingia kwenye vitu vinavyo husiana na Demokrasia 😳 !
😳😱 !
 
Noise Pollution imekuathiri tayari ... yaani unaona ukimya kama sio sawa vilee ... umezoea kelele na kupishana kwa kupigana vipushi kariakooo mkuu
Kabisa mkuu, yaani ile nafika Dom town naona kama watu wamekatazwa wasitoke maana naona magari ni machache road, watu wachache pia pako kimya sana. Maeneo kama kariakoo siyapendi kabisa maana kule no mama wa kelele dar nzima.
 
Kuishi kwenye kelele ni mojawapo ya indicators za umasikini na ujima!! Kelele nyumbani, kelele barabarani, kelele maofisini, kelele nyumba za ibada.., ili mradi kelele kila mahali!!
 
Siku hizi ukivuka barabara inabidi uchukue tahadhari ya magari, bodaboda na bajaji. Yaani kuvuka barabara imekuwa ngumu kuliko kusolve swali la logarithm
To be honest, hakuna kipindi huwa natukana matusi mengi kama kipindi cha kuvuka barabara baada wajinga wenye magari na pikipiki ni wengi sana...
 
Kabisa mkuu, yaani ile nafika Dom town naona kama watu wamekatazwa wasitoke maana naona magari ni machache road, watu wachache pia pako kimya sana. Maeneo kama kariakoo siyapendi kabisa maana kule no mama wa kelele dar nzima.
Sogea karume pale ukikaa pale masaa 3 njaa haijakuuma kwa yale makelele niite mimi lofa ila mimi nimependa ile ndio inavuta wateja watu hawapendi biashara za kupigana yaan shati hilo hilo wewe unauziwa 15,000 kuna mwenzio anauziwa 2000 kwa hio ikitangazwa 2000 hio inavuta wateja kwamba pale shati zote 2000 zamani walikua hawatangazi kwa hio ukifika pale unauliza bei na haijaandikwa kinachofuata ni kupigwa elfu 2 2 shati elfu 2 2 elfu 2 2 shati elfu 2 2
 
Kabisa mkuu, yaani ile nafika Dom town naona kama watu wamekatazwa wasitoke maana naona magari ni machache road, watu wachache pia pako kimya sana. Maeneo kama kariakoo siyapendi kabisa maana kule no mama wa kelele dar nzima.
For sure Dom ni mji wenye utulivu sana.
Hata machinga kule airport kuko kimya
Hata watu Wana ka utulivu fulani sio ka kariakooo mkuu! Kila mtu ni kama kavurugwa
 
wanaohubiri kwenye vituo vya daldala,asubuhi tuu makelele mtindo mmoja
 
Sidhani kama ishu ya bei ni sababu, watanzania tunapenda tu makelele. Kwa mfano kwenye daladala kuna konda anaita abiria kwa kutaja bei na sehemu gari inaenda halafu kuna mpiga debe naye anafanya kitu kilekile. Huwa najiuliza haya yote sababu ni nini...
 
Aisee hali makelele inatisha,yaani ukienda Kariakoo lazima urudi kichwa kinauma!!Kwa ujumla Dar kwa sasa ni jiji la kelele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…