Dar es salaam limegeuka jiji la makelele, Serikali imelala?

Bodaboda wanafunga honi za Harrier Lexus, yaani ni shida

Pia boda zimekua nyingi sana dar, hivi baada ya 5years hali itakuaje kwa wingi wao
Yaani baada ya muda tutakuwa na watu wasioeleweka kabisa. Pia jiji la dar es salaam linapoelekea si kuzuri. Tunajua kwa sasa ni ngumu kusimamia swala hili kwa sababu kila chama kinataka kura.
 
Mungu akubariki kwa kuleta mada hii. Dar es Salaam ni dampo la kelele.

Naongezea
5. Makelele ya baadhi ya misikiti na makanisa. Mungu hahitaji sauti za maspika makubwa wakati wa ibada ndo atusikie. Ikiwa ni mkutano wa injili au mhadhara hapo sawa. Lakini kuamshana usiku/mchana au saa 11 asubuhi na kelele za maspika wakati kila mtu anajua wajibu wake si poa.
Ngoja black Arab waje uwasikie wakitetea hoja.
 
Hilo Jiji la kutumia pesa huliweza nenda bush huko porini ukapate utulivu huko huwezi kusikia makelele zaidi ya ndege wa anga

Kuna pesa wapi? Wanaotumia pesa nyingi wote wako sehemu sizizo na kelele za ovyo ovyo kama hizi za maspika ya bodaboda. Kabla ya boda boda na mabanda mengi mji haukua hivi.
 
Ili Uishi vizuri kwenye haya Maisha haitakiwi kuwa Kompliketa! Wote wanaosababisha hizo ambazo Kwako ni kero ni watu wenye Akili timamu na wanachofanya ndio kichocheo cha kuwapatia Riziki.

Hata Miaka ya zamani Sehemu za mikusanyiko ya watu kama masokoni au Sehemu za kupata usafiri ( maeneo ya stand) hua kuna kelele yani kabla ya hivi vispika unavyosema.

Kama Hapa Dar baadhi ya maeneo kulivyo Busy na Biashara nyingi, Nadhani ikiwa unahitaji utulivu inabidi ubadili ZONE... Labda ukafanye Mishe zako maeneo ya Pembezoni Huko ambapo bado hakuna population kubwa au kwenda baadhi ya Mikoa ambayo ndio kwanza inajitafuta ila kwa Hapa Dar! Ukishuka Mbezi tu UBUSY na kelele zinakuchangamsha ili ujue Uko wapi sasa.
 
Siku hizi ukitembea katika jiji la Dar es salaam, hali imekuwa si hali ni makelele mtindo mmoja. Hakuna utulivu kabisa.

Ukienda masokoni kila mwenye kibanda chake ana spika na rerding inayoita biashara yake non-stop kuanzia asubuhi saa mbili hadi usiku au jioni mida ya kufunga kazi.

Wakati huohuo kuna magari yanapita mabarabarani yanapiga muziki kwa sauti kubwa ajabu eti yanapromote makampuni fulanifulani. Wakati mwingine yanaweka kambi masokoni au sehemu yenye mkusanyiko mkubwa wa watu na kufungulia maspika yake ya muziki. Yaani ni makelele tupu mijini.

Kwa sasa ukiwa jijini Dar es salaam, unafanya mishe zako hakuna utulivu, huwezi kuconcentrate.

Ukiacha hilo, utakutana na bodaboda nao wamefunga mziki mzito, wanapiga singeli mtindo mmoja.

Hapo sijazungumzia Bar zinazofungulia muziki non stop katika makazi ya watu.

Noise pollution Dar ni kubwa mno imesababisha watu waumwe vichwa, uwezo wa kusikia kupungua, msongo wa mawazo, Quality of life imeshuka mno na sababu mojawapo ni Makelele mtindo mmoja.

Serikali haina budi kufanya yafuatayo.

1. Kuzuia kila mwenye biashara yake masokoni kuwa na kimtambo cha kupiga kelele kuita wateja. Hivi vispeaker vinafanya maisha ya ufanyaji shughuli masokoni kuwa headache

2. Serikali ipige marufuku kwa bodaboda kufunga speaker kwenye mabodaboda yao, kwanza haya mamiziki wanayofungulia ni hatari kwa usalama barabarani.

3. Serikali ithibiti haya matangazo ya magari ambayo huzunguuka mitaani huku wamefungulia muzik kwa staili ya Disco.

4. Miziki kwenye mabar iangaliwe upya, limit ya kiwango cha sauti (decibels) kiwekwe ili kupunguzia wananchi adha.
Hivi ni makelele au makerere? Maana nyie wazaramo mnatuhalalishia ujinga wenu mkidhami wote ni wehu kama ninyi
 
Unajua watu wengi jawajuhi maana ya afya ya akili. Wanadhani kelele si sababisho kubwa mojawapo. Kutaka utulivu haina maana kwamba watu wanabagua wengine. Sheria zenyewe za mazingira haziruhusu makelele ya kijinga kama haya ya sasa. Zamani jiji la dar es salaam halikuwa hivi. Pia inawezekana kufanya shughuli za boda boda bila kelele. Kama vipi bodaboda zipunguzwe!!!
 
Usiishi zamani BRO... Ishi Sasa! Kila kitu tukianza kulalamika "zamani haikua hivi, zamani ilikuwa vile" unadhani hata majukumu yako binafsi utapata muda wa kuyatatua kweli???

Maisha yanabadilika na ISIKARIRI! Hata TIGO sasa ni YAS na hatulalamiki
 
Ni hivi, hatuwezi kuishi na makelele kiaai hiki. POLLUTION itokanayo na kelele ni nyingi mno. Tusifanye kama sheria hazipo wakati NEMC ina sheria zote zinazozuia makelele kama hayo. Watu wawe wastaarabu na wasipotaka kuwa waataarabu walazimishwe kutii sheria....si picha nzuri kwa wageni na wenyeji. Mimi kwa upande wangu sipendi jiji zuri kama hili liwe na sifa mbaya.
 
Siku hizi ukitembea katika jiji la Dar es salaam, hali imekuwa si hali ni makelele mtindo mmoja. Hakuna utulivu kabisa.

Ukienda masokoni kila mwenye kibanda chake ana spika na rerding inayoita biashara yake non-stop kuanzia asubuhi saa mbili hadi usiku au jioni mida ya kufunga kazi.

Wakati huohuo kuna magari yanapita mabarabarani yanapiga muziki kwa sauti kubwa ajabu eti yanapromote makampuni fulanifulani. Wakati mwingine yanaweka kambi masokoni au sehemu yenye mkusanyiko mkubwa wa watu na kufungulia maspika yake ya muziki. Yaani ni makelele tupu mijini.

Kwa sasa ukiwa jijini Dar es salaam, unafanya mishe zako hakuna utulivu, huwezi kuconcentrate.

Ukiacha hilo, utakutana na bodaboda nao wamefunga mziki mzito, wanapiga singeli mtindo mmoja.

Hapo sijazungumzia Bar zinazofungulia muziki non stop katika makazi ya watu.

Noise pollution Dar ni kubwa mno imesababisha watu waumwe vichwa, uwezo wa kusikia kupungua, msongo wa mawazo, Quality of life imeshuka mno na sababu mojawapo ni Makelele mtindo mmoja.

Serikali haina budi kufanya yafuatayo.

1. Kuzuia kila mwenye biashara yake masokoni kuwa na kimtambo cha kupiga kelele kuita wateja. Hivi vispeaker vinafanya maisha ya ufanyaji shughuli masokoni kuwa headache

2. Serikali ipige marufuku kwa bodaboda kufunga speaker kwenye mabodaboda yao, kwanza haya mamiziki wanayofungulia ni hatari kwa usalama barabarani.

3. Serikali ithibiti haya matangazo ya magari ambayo huzunguuka mitaani huku wamefungulia muzik kwa staili ya Disco.

4. Miziki kwenye mabar iangaliwe upya, limit ya kiwango cha sauti (decibels) kiwekwe ili kupunguzia wananchi adha.
Unategemea nini kama mkuu wa mkoa mwenyewe ni mpiga makelele? Ubunifu zero, anashangaa makonda anafanikishaje mambo yy tupo huku kwenye matajir wa kila aina lkn mambo hayaendi!!
 
Ni hivi, hatuwezi kuishi na makelele kiaai hiki. POLLUTION itokanayo na kelele ni nyingi mno. Tusifanye kama sheria hazipo wakati NEMC ina sheria zote zinazozuia makelele kama hayo. Watu wawe wastaarabu na wasipotaka kuwa waataarabu walazimishwe kutii sheria....si picha nzuri kwa wageni na wenyeji. Mimi kwa upande wangu sipendi jiji zuri kama hili liwe na sifa mbaya.
Samahani Bro! Kwani umefikia sehemu gani?
 
Back
Top Bottom