Dar es salaam limegeuka jiji la makelele, Serikali imelala?

Dar es salaam limegeuka jiji la makelele, Serikali imelala?

Ili Uishi vizuri kwenye haya Maisha haitakiwi kuwa Kompliketa! Wote wanaosababisha hizo ambazo Kwako ni kero ni watu wenye Akili timamu na wanachofanya ndio kichocheo cha kuwapatia Riziki.

Hata Miaka ya zamani Sehemu za mikusanyiko ya watu kama masokoni au Sehemu za kupata usafiri ( maeneo ya stand) hua kuna kelele yani kabla ya hivi vispika unavyosema.

Kama Hapa Dar baadhi ya maeneo kulivyo Busy na Biashara nyingi, Nadhani ikiwa unahitaji utulivu inabidi ubadili ZONE... Labda ukafanye Mishe zako maeneo ya Pembezoni Huko ambapo bado hakuna population kubwa au kwenda baadhi ya Mikoa ambayo ndio kwanza inajitafuta ila kwa Hapa Dar! Ukishuka Mbezi tu UBUSY na kelele zinakuchangamsha ili ujue Uko wapi sasa.
Kila mtu akiamua kufanya chochote anachojisikia in the name of kutafuta ridhiki, Mzee hapatakalika.
 
I think wageni kutoka nchi zilizoendelea wakija nchini mwetu wakatuona tunavyoishi na kufanya mambo yetu kama watu wasi na akili wanatushangaa sana.

Kuna story kwamba MJ alipotua Dar aliziba pua muda wote, sina hakika kama ni kweli ila Dar inanuka kweli sio utani. Ukifika tu pale airport unasikia harufu moja ya ajabu.
 
Nilishangaa sana Hadi Mama Lishe anakipaza sauti Dah!,alafu ile sauti ipo recorded inajiludia Automatic Akiwasha Asubuhi ni mpaka jioni, tuwekeni utaratibu wa kujali na haki za wengine sio kila Mtu anapenda Kelele kiasi kwamba ukipigiwa simu hamuwezi kusikilizana
Nikikuta sehemu ya kula kuna kispika huwa napita kando. Sijazoea kabisa kula na makelele.
 
Nchi ya kipumbavu sana hii. Hakuna utawala wa sheria hata kidogo.

Bajaji zinaweka honi na ving'ora kama polisi. Kila siku usiku ni xmas kwa jinsi zinavyomulika.

Majengo yanajengwa kiholela kila kona hakuna residential area tena hasa DSM. Unajenga nyumba hapa jirani yako mtu anajenga bar, sheli na nyumba ya ibada.

Leo nimeona video mtu kasimamisha gari barabarini kabisa ili aingie msikitini pale coco beach. Kwanza kujenga msikiti, clubs, restaurants coco beach ni uzwazwa wa hali ya juu.

Nchi ya kipumbavu sana hii.
Tukisema tuwe wakweli, Dar imejengeka sehemu chache sana ambazo unaweza ukasimama with confidence ukasema yes hili ni jiji. Sehemu nyingi mpangilio ni wa hovyo wanazidiwa hadi na maskani kwetu Lizaboni.

Miaka sio mingi hili jiji halitakua jiji tena bali pango la walanguzi.
 
Siku hizi ukitembea katika jiji la Dar es salaam, hali imekuwa si hali ni makelele mtindo mmoja. Hakuna utulivu kabisa.

Ukienda masokoni kila mwenye kibanda chake ana spika na rerding inayoita biashara yake non-stop kuanzia asubuhi saa mbili hadi usiku au jioni mida ya kufunga kazi.

Wakati huohuo kuna magari yanapita mabarabarani yanapiga muziki kwa sauti kubwa ajabu eti yanapromote makampuni fulanifulani. Wakati mwingine yanaweka kambi masokoni au sehemu yenye mkusanyiko mkubwa wa watu na kufungulia maspika yake ya muziki. Yaani ni makelele tupu mijini.

Kwa sasa ukiwa jijini Dar es salaam, unafanya mishe zako hakuna utulivu, huwezi kuconcentrate.

Ukiacha hilo, utakutana na bodaboda nao wamefunga mziki mzito, wanapiga singeli mtindo mmoja.

Hapo sijazungumzia Bar zinazofungulia muziki non stop katika makazi ya watu.

Noise pollution Dar ni kubwa mno imesababisha watu waumwe vichwa, uwezo wa kusikia kupungua, msongo wa mawazo, Quality of life imeshuka mno na sababu mojawapo ni Makelele mtindo mmoja.

Serikali haina budi kufanya yafuatayo.

1. Kuzuia kila mwenye biashara yake masokoni kuwa na kimtambo cha kupiga kelele kuita wateja. Hivi vispeaker vinafanya maisha ya ufanyaji shughuli masokoni kuwa headache

2. Serikali ipige marufuku kwa bodaboda kufunga speaker kwenye mabodaboda yao, kwanza haya mamiziki wanayofungulia ni hatari kwa usalama barabarani.

3. Serikali ithibiti haya matangazo ya magari ambayo huzunguuka mitaani huku wamefungulia muzik kwa staili ya Disco.

4. Miziki kwenye mabar iangaliwe upya, limit ya kiwango cha sauti (decibels) kiwekwe ili kupunguzia wananchi adha.
Miji yote yenye makanisa na miskiti mingi ni chaka la makelele. Huwa sielewi. Eti wanaitana kwenda kuswali. Mbona kwenye kwenda kazini na kufanya na mambo mengine hawaitani?
 
Siku hizi ukitembea katika jiji la Dar es salaam, hali imekuwa si hali ni makelele mtindo mmoja. Hakuna utulivu kabisa.

Ukienda masokoni kila mwenye kibanda chake ana spika na rerding inayoita biashara yake non-stop kuanzia asubuhi saa mbili hadi usiku au jioni mida ya kufunga kazi.

Wakati huohuo kuna magari yanapita mabarabarani yanapiga muziki kwa sauti kubwa ajabu eti yanapromote makampuni fulanifulani. Wakati mwingine yanaweka kambi masokoni au sehemu yenye mkusanyiko mkubwa wa watu na kufungulia maspika yake ya muziki. Yaani ni makelele tupu mijini.

Kwa sasa ukiwa jijini Dar es salaam, unafanya mishe zako hakuna utulivu, huwezi kuconcentrate.

Ukiacha hilo, utakutana na bodaboda nao wamefunga mziki mzito, wanapiga singeli mtindo mmoja.

Hapo sijazungumzia Bar zinazofungulia muziki non stop katika makazi ya watu.

Noise pollution Dar ni kubwa mno imesababisha watu waumwe vichwa, uwezo wa kusikia kupungua, msongo wa mawazo, Quality of life imeshuka mno na sababu mojawapo ni Makelele mtindo mmoja.

Serikali haina budi kufanya yafuatayo.

1. Kuzuia kila mwenye biashara yake masokoni kuwa na kimtambo cha kupiga kelele kuita wateja. Hivi vispeaker vinafanya maisha ya ufanyaji shughuli masokoni kuwa headache

2. Serikali ipige marufuku kwa bodaboda kufunga speaker kwenye mabodaboda yao, kwanza haya mamiziki wanayofungulia ni hatari kwa usalama barabarani.

3. Serikali ithibiti haya matangazo ya magari ambayo huzunguuka mitaani huku wamefungulia muzik kwa staili ya Disco.

4. Miziki kwenye mabar iangaliwe upya, limit ya kiwango cha sauti (decibels) kiwekwe ili kupunguzia wananchi adha.
Niliwapongeza wathibiti ubora wa viwango vya kelele walipoingia kazini na iile sheria yao mpya.Niliioma Tanzania ya ustaarabu,ila kwa kuwa wanasii hasa ndio mamiliki wa sehemu hizi za makelele wakawapiga nyundo na waowakaona isiwe shida.Matokeo yake ndio haya tunashuhudia hivi sasa.
 
Wenzako wenye hela wamesogea Mbweni.

Hata iliyokuwa mitaa ya kishua Dar zama hizo, watoto wanaweza cheza mpira barabarani siku hizi dała dała zinakatiza.

Ukitaka amani sogea nje, akina sisi tusio na uwezo wa kununua Mbweni, utaratibu ni Kibaha.
Kwa dar hata huko mbweni ni suala la muda tu kelele zitafika. zamani kuna maeneo yalikuwa ya kishua siku hizi vurugu match kama kawaida.
 
Tatizo lipo hapa Tunakuwa na Siasa za kuwahadaa Wananchi, Mamlaka zisema zisimamie haya mambo kwa utaratibu Wanaibuka Wazee wa Siasa kutetea
Tanzania siasa za vyama vingi tumeshindwa kusimamia. waliomadarakani wanaogopa kusimamia mambo yanayotungiwa sheria na kanuni kuogopa kupoteza mvuto, wenyewe wanasema tusiwaudhi wapiga kura. Dar ina kama watu milion 6 lkn jiji limekuwa la hovyo kwa kelele na uchafu kwa kisingizio cha watu wengi. Je hao wenzenu wenye miji yenye idadi ya watu zaidi ya milion 10 na imetulia na niyakistaarabu wanawezaje!
 
Back
Top Bottom