Dar es salaam limegeuka jiji la makelele, Serikali imelala?

Unatetea
Ili Uishi vizuri kwenye haya Maisha haitakiwi kuwa Kompliketa! Wote wanaosababisha hizo ambazo Kwako ni kero ni watu wenye Akili timamu na wanachofanya ndio kichocheo cha kuwapatia Riziki.

Hata Miaka ya zamani Sehemu za mikusanyiko ya watu kama masokoni au Sehemu za kupata usafiri ( maeneo ya stand) hua kuna kelele yani kabla ya hivi vispika unavyosema.

Kama Hapa Dar baadhi ya maeneo kulivyo Busy na Biashara nyingi, Nadhani ikiwa unahitaji utulivu inabidi ubadili ZONE... Labda ukafanye Mishe zako maeneo ya Pembezoni Huko ambapo bado hakuna population kubwa au kwenda baadhi ya Mikoa ambayo ndio kwanza inajitafuta ila kwa Hapa Dar! Ukishuka Mbezi tu UBUSY na kelele zinakuchangamsha ili ujue Uko wapi sasa.
Upumbuvu
 
Siku hizi ukitembea katika jiji la Dar es salaam, hali imekuwa si hali ni makelele mtindo mmoja. Hakuna utulivu kabisa.

Ukienda masokoni kila mwenye kibanda chake ana spika na rerding inayoita biashara yake non-stop kuanzia asubuhi saa mbili hadi usiku au jioni mida ya kufunga kazi.

Wakati huohuo kuna magari yanapita mabarabarani yanapiga muziki kwa sauti kubwa ajabu eti yanapromote makampuni fulanifulani. Wakati mwingine yanaweka kambi masokoni au sehemu yenye mkusanyiko mkubwa wa watu na kufungulia maspika yake ya muziki. Yaani ni makelele tupu mijini.

Kwa sasa ukiwa jijini Dar es salaam, unafanya mishe zako hakuna utulivu, huwezi kuconcentrate.

Ukiacha hilo, utakutana na bodaboda nao wamefunga mziki mzito, wanapiga singeli mtindo mmoja.

Hapo sijazungumzia Bar zinazofungulia muziki non stop katika makazi ya watu.

Noise pollution Dar ni kubwa mno imesababisha watu waumwe vichwa, uwezo wa kusikia kupungua, msongo wa mawazo, Quality of life imeshuka mno na sababu mojawapo ni Makelele mtindo mmoja.

Serikali haina budi kufanya yafuatayo.

1. Kuzuia kila mwenye biashara yake masokoni kuwa na kimtambo cha kupiga kelele kuita wateja. Hivi vispeaker vinafanya maisha ya ufanyaji shughuli masokoni kuwa headache

2. Serikali ipige marufuku kwa bodaboda kufunga speaker kwenye mabodaboda yao, kwanza haya mamiziki wanayofungulia ni hatari kwa usalama barabarani.

3. Serikali ithibiti haya matangazo ya magari ambayo huzunguuka mitaani huku wamefungulia muzik kwa staili ya Disco.

4. Miziki kwenye mabar iangaliwe upya, limit ya kiwango cha sauti (decibels) kiwekwe ili kupunguzia wananchi adha.
Ukweli mtupu.
 
Mkuu hujakaa karibu na ile misikiti ya "swalaa, swalaa, kitanda chako ndiyo kaburi, shuka ndiyo sanda yako, swalaa swalaaa" wanakupigia makelele saa nzima sala ya alfajiri, bila kujali una imani gani?

Hizo sauti za swalaa swalaa za Alfajiri nazo inabidi zifanyiwe kazi. Kwanza hazimo katika mafunzo ya Uislamu aliyoacha mtume. Hili ni rahisi tu kwa waislamu kulirekebisha.
 
Mkuu hujakaa karibu na ile misikiti ya "swalaa, swalaa, kitanda chako ndiyo kaburi, shuka ndiyo sanda yako, swalaa swalaaa" wanakupigia makelele saa nzima sala ya alfajiri, bila kujali una imani gani?

Maombi hayatambuliki kwa wote katika secular state. Maombi yenu ombeni kanisani kwenu msiwapigie kelele wengine wasioamini kama nyie.
Wewe nae hapa watu wanaongelea non stop noice pollution,
Wewe umekazania kwenye chuki ya udini tu,hiyo kunadi salaa hua haichukui hata dakika 2 au 3

Mapimbi kama nyie kwenye kila mada hua mnalazimisha muingize issue za udini.
 
Mkuu hujakaa karibu na ile misikiti ya "swalaa, swalaa, kitanda chako ndiyo kaburi, shuka ndiyo sanda yako, swalaa swalaaa" wanakupigia makelele saa nzima sala ya alfajiri, bila kujali una imani gani?

Maombi hayatambuliki kwa wote katika secular state. Maombi yenu ombeni kanisani kwenu msiwapigie kelele wengine wasioamini kama nyie.
Wasio amini ni asilimia ngapi?? 0.002 ni wewe Kiranga, Yericko Nyerere na Marehem Kingunge ambaye alimkiri Yesu kabla ya kuzikwa.

Hivyo basi Kwa vile wengi ni waamimi wa Yesu au Mtume let them pray the way they wish, that is the only way for them to heal from their problems.

Watanzania wanamatatizo mengi saana, wanaamini maombi ndio suluhisho
 
This logical fallacy is called argument from popularity.

Argumentum ad populum.

Siku hizi ukitembea katika jiji la Dar es salaam, hali imekuwa si hali ni makelele mtindo mmoja. Hakuna utulivu kabisa.

Ukienda masokoni kila mwenye kibanda chake ana spika na rerding inayoita biashara yake non-stop kuanzia asubuhi saa mbili hadi usiku au jioni mida ya kufunga kazi.

Wakati huohuo kuna magari yanapita mabarabarani yanapiga muziki kwa sauti kubwa ajabu eti yanapromote makampuni fulanifulani. Wakati mwingine yanaweka kambi masokoni au sehemu yenye mkusanyiko mkubwa wa watu na kufungulia maspika yake ya muziki. Yaani ni makelele tupu mijini.

Kwa sasa ukiwa jijini Dar es salaam, unafanya mishe zako hakuna utulivu, huwezi kuconcentrate.

Ukiacha hilo, utakutana na bodaboda nao wamefunga mziki mzito, wanapiga singeli mtindo mmoja.

Hapo sijazungumzia Bar zinazofungulia muziki non stop katika makazi ya watu.

Noise pollution Dar ni kubwa mno imesababisha watu waumwe vichwa, uwezo wa kusikia kupungua, msongo wa mawazo, Quality of life imeshuka mno na sababu mojawapo ni Makelele mtindo mmoja.

Serikali haina budi kufanya yafuatayo.

1. Kuzuia kila mwenye biashara yake masokoni kuwa na kimtambo cha kupiga kelele kuita wateja. Hivi vispeaker vinafanya maisha ya ufanyaji shughuli masokoni kuwa headache

2. Serikali ipige marufuku kwa bodaboda kufunga speaker kwenye mabodaboda yao, kwanza haya mamiziki wanayofungulia ni hatari kwa usalama barabarani.

3. Serikali ithibiti haya matangazo ya magari ambayo huzunguuka mitaani huku wamefungulia muzik kwa staili ya Disco.

4. Miziki kwenye mabar iangaliwe upya, limit ya kiwango cha sauti (decibels) kiwekwe ili kupunguzia wananchi adha.
Rudi kwenu Kasulu kwani lazima ukae Dar
 
Tanzania Ni Kubwa Sana, hamia mikoa yenye utulivu. Waache waliozoea makelele waendelee na biashara zao.
 
Sasa ukutane na daladala zile aina ya Eicher zina honi kali sana ambayo inaweza ikamuua mwenye ugonjwa wa moyo !
Wenyewe hata habari hawana !
Labda nayo hii inaingia kwenye vitu vinavyo husiana na Demokrasia 😳 !
😳😱 !
Hahaaa. Ndiyo ubaya wa demokrasia huo mkuu. Ukitaka kuwagusa machinga unaogopa sababu watakunyima kura. Ukitaka kusema msijenge hapa, bodaboda ziwe na utaratibu huu, bajaji ziwe hivi nk nk huwezi sababu ya kuogopa kunyimwa kura. Ndiyo maana miji ya India haieleweki hata kidogo. Miji yetu nayo inafuata huko.
 
Back
Top Bottom