Intelligence Justice
JF-Expert Member
- Oct 23, 2020
- 3,443
- 4,006
Mkuu,Siku hizi ukitembea katika jiji la Dar es salaam, hali imekuwa si hali ni makelele mtindo mmoja. Hakuna utulivu kabisa.
Ukienda masokoni kila mwenye kibanda chake ana spika na rerding inayoita biashara yake non-stop kuanzia asubuhi saa mbili hadi usiku au jioni mida ya kufunga kazi.
Wakati huohuo kuna magari yanapita mabarabarani yanapiga muziki kwa sauti kubwa ajabu eti yanapromote makampuni fulanifulani. Wakati mwingine yanaweka kambi masokoni au sehemu yenye mkusanyiko mkubwa wa watu na kufungulia maspika yake ya muziki. Yaani ni makelele tupu mijini.
Kwa sasa ukiwa jijini Dar es salaam, unafanya mishe zako hakuna utulivu, huwezi kuconcentrate.
Ukiacha hilo, utakutana na bodaboda nao wamefunga mziki mzito, wanapiga singeli mtindo mmoja.
Hapo sijazungumzia Bar zinazofungulia muziki non stop katika makazi ya watu.
Noise pollution Dar ni kubwa mno imesababisha watu waumwe vichwa, uwezo wa kusikia kupungua, msongo wa mawazo, Quality of life imeshuka mno na sababu mojawapo ni Makelele mtindo mmoja.
Serikali haina budi kufanya yafuatayo.
1. Kuzuia kila mwenye biashara yake masokoni kuwa na kimtambo cha kupiga kelele kuita wateja. Hivi vispeaker vinafanya maisha ya ufanyaji shughuli masokoni kuwa headache
2. Serikali ipige marufuku kwa bodaboda kufunga speaker kwenye mabodaboda yao, kwanza haya mamiziki wanayofungulia ni hatari kwa usalama barabarani.
3. Serikali ithibiti haya matangazo ya magari ambayo huzunguuka mitaani huku wamefungulia muzik kwa staili ya Disco.
4. Miziki kwenye mabar iangaliwe upya, limit ya kiwango cha sauti (decibels) kiwekwe ili kupunguzia wananchi adha.
Wewe ni mkongwe, kwanini usiwasilishe lalamiko lako na sheria ichukue mkondo wake?
SHERIA NA KANUNII.
"..Sheria ya Mazingira, 2004 Kifungu 106(5) (5) Si ruhusa kwa mtu yeyote kupiga kelele aukusababisha kelele kuzidi kiwangokilichoainishwa au kitakachobainishwakuhusiana na upigaji kelele. (6) Litakuwa ni kosa kwa mtu yeyote kumwagauchafu au kupiga kelele bila kuzingatia njiailiyobainishwa kuwa ni bora katika Kanunizinazoweza kutungwa na Waziri.II. Kanuni za Usimamizi wa Mazingira zaViwango vya Udhibiti wa Kelele na Mitetemoza mwaka 2015Katika kudhibiti kelele na mitetemo, Waziri mwenyedhamana ya mazingira kupitia Kifungu cha230(2)(s) cha Sheria ya Usimamizi wa MazingiraSura 191, mwaka 2015 alitunga Kanuni zaUsimamizi wa Mazingira za Viwango vya Udhibitiwa Kelele na Mitetemo za mwaka 2015 (Tangazo laSerikali Na. 32 la mwaka 2015).."