Dar es salaam limegeuka jiji la makelele, Serikali imelala?

Dar es salaam limegeuka jiji la makelele, Serikali imelala?

Ili Uishi vizuri kwenye haya Maisha haitakiwi kuwa Kompliketa! Wote wanaosababisha hizo ambazo Kwako ni kero ni watu wenye Akili timamu na wanachofanya ndio kichocheo cha kuwapatia Riziki.

Hata Miaka ya zamani Sehemu za mikusanyiko ya watu kama masokoni au Sehemu za kupata usafiri ( maeneo ya stand) hua kuna kelele yani kabla ya hivi vispika unavyosema.

Kama Hapa Dar baadhi ya maeneo kulivyo Busy na Biashara nyingi, Nadhani ikiwa unahitaji utulivu inabidi ubadili ZONE... Labda ukafanye Mishe zako maeneo ya Pembezoni Huko ambapo bado hakuna population kubwa au kwenda baadhi ya Mikoa ambayo ndio kwanza inajitafuta ila kwa Hapa Dar! Ukishuka Mbezi tu UBUSY na kelele zinakuchangamsha ili ujue Uko wapi sasa.
Kelele zinawapatiaje watu riziki?? Mbona majiji mingine yote hata ya nchi zilizotuzunguka ambazo hatutofautiani sana katika umasikini watu wanapata riziki bila kelele??
 
Pole sana Bro! Inabidi ujitahidi kusogea Pembezoni ambako bado hakuna Makazi ya Watu kwa wingi utaweza kupata unachotaka
ushauri wako haufai. Ina maana huko nako hauna bodaboda au kelele? Nchi imejaa bodaboda na kila aina ya kelele. So huko unakosema wewe ndo kelele hazitakuja?. Acha serikali itakaposhughulikia hii issue utashangaa. Serikali ni sikivu sana na itashughulikia kero hii so muda mrefu.
 
Nilishangaa sana Hadi Mama Lishe anakipaza sauti Dah!,alafu ile sauti ipo recorded inajiludia Automatic Akiwasha Asubuhi ni mpaka jioni, tuwekeni utaratibu wa kujali na haki za wengine sio kila Mtu anapenda Kelele kiasi kwamba ukipigiwa simu hamuwezi kusikilizana
 
Nilishangaa sana Hadi Mama Lishe anakipaza sauti Dah!,alafu ile sauti ipo recorded inajiludia Automatic Akiwasha Asubuhi ni mpaka jioni, tuwekeni utaratibu wa kujali na haki za wengine sio kila Mtu anapenda Kelele kiasi kwamba ukipigiwa simu hamuwezi kusikilizana
Kwa kweli inakera sana.
 
Yaani baada ya muda tutakuwa na watu wasioeleweka kabisa. Pia jiji la dar es salaam linapoelekea si kuzuri. Tunajua kwa sasa ni ngumu kusimamia swala hili kwa sababu kila chama kinataka kura.
Tatizo lipo hapa Tunakuwa na Siasa za kuwahadaa Wananchi, Mamlaka zisema zisimamie haya mambo kwa utaratibu Wanaibuka Wazee wa Siasa kutetea
 
Nchi ya kipumbavu sana hii. Hakuna utawala wa sheria hata kidogo.

Bajaji zinaweka honi na ving'ora kama polisi. Kila siku usiku ni xmas kwa jinsi zinavyowakawaka.

Majengo yanajengwa kiholela kila kona hakuna residential area tena hasa DSM. Unajenga nyumba hapa jirani yako mtu anajenga bar, sheli na nyumba ya ibada.

Leo nimeona video mtu kasimamisha gari barabarini kabisa ili aingie msikitini pale coco beach. Kwanza kujenga msikiti, clubs, restaurants coco beach ni uzwazwa wa hali ya juu.

Nchi ya kipumbavu sana hii.
 
Ni fujo kwa kwenda mbele.Siyo Dar tu hata mikoani hali ni ileile labda uende vijijini na hakuna mtu anajali. Watu wanavuta sigara hadharani hadi bangi hakuna anayejali na sheria zipo wanasubiri hadi Rais atamke ndio wafanye kazi ovyo kabisa
 
Nchi ya kipumbavu sana hii. Hakuna utawala wa sheria hata kidogo.

Bajaji zinaweka honi na ving'ora kama polisi. Kila siku usiku ni xmas kwa jinsi zinavyomulika.

Majengo yanajengwa kiholela kila kona hakuna residential area tena hasa DSM. Unajenga nyumba hapa jirani yako mtu anajenga bar, sheli na nyumba ya ibada.

Leo nimeona video mtu kasimamisha gari barabarini kabisa ili aingie msikitini pale coco beach. Kwanza kujenga msikiti, clubs, restaurants coco beach ni uzwazwa wa hali ya juu.

Nchi ya kipumbavu sana hii.

Na utupaji taka kila sehemu. Siku hizi hata mitaro ya kupitishia maji ya mvua imegeuka madampo yakutupa taka. Chupa za energy, mifuko ya plastic, magunzi, na kila aina ya uchafu
 
Siku hizi ukitembea katika jiji la Dar es salaam, hali imekuwa si hali ni makelele mtindo mmoja. Hakuna utulivu kabisa.

Ukienda masokoni kila mwenye kibanda chake ana spika na rerding inayoita biashara yake non-stop kuanzia asubuhi saa mbili hadi usiku au jioni mida ya kufunga kazi.

Wakati huohuo kuna magari yanapita mabarabarani yanapiga muziki kwa sauti kubwa ajabu eti yanapromote makampuni fulanifulani. Wakati mwingine yanaweka kambi masokoni au sehemu yenye mkusanyiko mkubwa wa watu na kufungulia maspika yake ya muziki. Yaani ni makelele tupu mijini.

Kwa sasa ukiwa jijini Dar es salaam, unafanya mishe zako hakuna utulivu, huwezi kuconcentrate.

Ukiacha hilo, utakutana na bodaboda nao wamefunga mziki mzito, wanapiga singeli mtindo mmoja.

Hapo sijazungumzia Bar zinazofungulia muziki non stop katika makazi ya watu.

Noise pollution Dar ni kubwa mno imesababisha watu waumwe vichwa, uwezo wa kusikia kupungua, msongo wa mawazo, Quality of life imeshuka mno na sababu mojawapo ni Makelele mtindo mmoja.

Serikali haina budi kufanya yafuatayo.

1. Kuzuia kila mwenye biashara yake masokoni kuwa na kimtambo cha kupiga kelele kuita wateja. Hivi vispeaker vinafanya maisha ya ufanyaji shughuli masokoni kuwa headache

2. Serikali ipige marufuku kwa bodaboda kufunga speaker kwenye mabodaboda yao, kwanza haya mamiziki wanayofungulia ni hatari kwa usalama barabarani.

3. Serikali ithibiti haya matangazo ya magari ambayo huzunguuka mitaani huku wamefungulia muzik kwa staili ya Disco.

4. Miziki kwenye mabar iangaliwe upya, limit ya kiwango cha sauti (decibels) kiwekwe ili kupunguzia wananchi adha.
Upo sahihi boda boda wanasumbua sana kwa kelele imekuwa kero
 
Back
Top Bottom