Dar es Salaam ni lazima wafanyakazi wa ndani (housegirls) watoke mikoani?

Swahili AI

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2016
Posts
10,174
Reaction score
89,364
Kila siku wafanyakazi wanatafutwa kutoka mikoa mingine na kwenda Dar Es Salaam. Hilo jiji halina watu wenye wanaoihitaji hizo kazi?

Kitakwimu ndio jiji lenye watu wengi nchini? Mbona kila kutwa ninyi ndio wakuletewa wafanya kazi wa ndani na wasaidizi wa kazi kutoka mikoani?

Sio kijana wa kukata majani, kusaidia kwenye biashara, wala sio dada wa kusaidia kazi za ndani. Wote wanatoka mikoani kuja Dar.

Wakwenu huko wamepatwa na nini?
 
"Wakwenu huko wamepatwa na nini"? weka vizuri swali lako kwani umetuuliza kwanini tunachukua toka mikoani kisha unatushangaa kwanini hatuchukui toka kwetu ambako pia ni mikoani hukohuko.
 

Jitolee wewe uwe wa Dar, sidhani kama umekatazwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…