SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Najua hii mada itawashtua wengi na wengine watapanda munkari ila embu tuelewane kwanza kabla haujajibu kwa jazba.
Kwa tathmini yangu ya muda mrefu ni kuwa mji wa Dar es Salaam umejaa watu wasio na kazi maalumu. Wale wenye ajira rasmi serikalini au katika sekta binafsi ni wachache sana, wengi ni wabangaizaji na wazururaji walio katika mwamvuli wa kujiajiri.
Ukitaka kujua hilo ni kitendo cha asilimia kubwa ya watu kupotea mitaani siku mbili zilizopita kisa wameambiwa barabara zitafungwa. Yaani unaambiwa usiende kutafuta ugali wako halafu hata manung'uniko hamna, watu wametii amri bila shuruti. Hii inakwambia wengi hawakuwa na mitkasi ya maana wakaona fresh tu.
Nadhani kauli mbiu ya mji wa Dar es Salaam inapaswa kuwa "Mtembea bure siyo sawa na mkaa bure".