LGE2024 Dar es Salaam: Vyama 14 vya Siasa vyadai kuridhishwa na matokeo ya Uchaguzi

LGE2024 Dar es Salaam: Vyama 14 vya Siasa vyadai kuridhishwa na matokeo ya Uchaguzi

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Dhahiri sadaka ya goli la mama linatafutwa wakimsubiri Abdul
 
VYAMA 14 vya siasa vimesema Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika jana ulikuwa huru na haki.

Aidha vyama hivyo vimeipongeza serikali chini ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, kwa maandalizi mazuri tangu mwanzo wa kupata wagombea, kampeni na upigaji kura.

Vyama hivyo vimetoa tamko hilo mapema leo Dar es Salaam, vilipokuwa vikitoa tathimini ya uchaguzi uliofanyika Novemba 27 mwaka huu.

Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP) Wilaya ya Kinondoni, Bakari Makame, amesema vyama hivyo vimeridhishwa na mwenendo mzima wa uchaguzi huo na matokeo yaliyotangazwa.

"Uchaguzi uliofanyika ulikuwa wa amani, huru na kulikiwa hakuna vurugu. Kwa upande wa Wilaya ya Kinondoni uchaguzi ulikuwa mfano kwa wilaya zote," amesema Makame.

PIA SOMA
- LGE2024 - Tamko la Vyama nane vya siasa rafiki kwa CCM | vyaishambulia CHADEMA
Nchi hii ina TISS Wajinga sana. Hivi unajua haya yote wana yaandaa wao???
 
Hivyo ni vyama vya kinafiki, si vya kisiasa vya upinzani. Havijulikani kwa wapiga kura vinafanya nini. Kazi ya vyama hivyo ni kuisindikiza CCM kushinda, vyama vya upinzani ni dhahiri vinajulikana, ndio hivyo vilivyoona dosari kwa uchaguzi huu.
Haya yalikuwepo hata enzi za ukoloni (divide them n rule)
Anayeandaa maigizo haya akili yake imevia. Huwezi kutumia mbinu za miaka ya 1880s leo
 
Vyama hivyo vilisimamisha wagombea wao kwenye uchaguzi huu na vimepata viti vingapi.Au walikuwa waangalizi kwenye mchakato wa uchaguzi wa Serikali za mitaa.
 
Tulishindwa elimu tukadhani kutunga mtihani rahisi ndio suluhu....
Matokeo ya elimu mbovu ndio tumepata wanasiasa wajinga kama hao WA vyama vya upinzani
 
Back
Top Bottom