Dar es Salaam: Watoto 160 wamezaliwa kwa upandikizaji mimba

Dar es Salaam: Watoto 160 wamezaliwa kwa upandikizaji mimba

Traxtion

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2021
Posts
8,000
Reaction score
16,414
DAR ES SALAAM; KITUO cha kupandikiza mimba cha Kairuki Green IVF (KGIVF) cha Dar es Salaam kimefikisha watoto 160 tangu kuanzishwa kwake miaka mitatu iliyopita.

Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa kituo hicho, Dk Clementina Kairuki wakati akizungumzia maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya IVF ambayo huadhimishwa kila Julai 25.

Alikuwa akizungumza na wasanii wa Juakali waliotembelea kituo hicho kujifunza kinavyofanya shughuli zake za kupandikiza mimba na kusaidia familia zenye changamoto ya uzazi.

Dk Clementina alisema Julai 25 imepangwa kuwa Siku ya IVF Duniani kwa kuwa ndiyo siku ambayo mtoto wa kwanza alipatikana kwa njia ya upandikizaji wa mimba, ambaye kwa sasa ana miaka 47.

“Tunawapongeza watu waliogundua hii IVF kwa sababu haikuwa rahisi, kwani waligundua baada ya kujaribu mara nyingi sana. Walijaribu karibu mara 103 ndipo wakafanikiwa na mtoto wa kwanza akazaliwa.

“Hata magazeti ya wakati ule nchini Uingereza yanaonesha habari zote ziliandika tukio hilo,” alisema.

Alisema tangu kuzaliwa kwa mtoto huyo wa kwanza, teknolojia ya upandikizaji wa mimba imekuwa ikikua siku hadi siku na sasa inafanyika kwa njia za kisasa zaidi kuliko ilivyokuwa miaka ya zamani.
1785211178497.jpg
 
Gharama yake ni kiasi gani ili watu wajipange hili ni tatizo gumu Sana kwenye ndoa.
 
Back
Top Bottom