Mke wangu kanipigia simu yuko njiani kuelekea Dar akitokea Arusha...Kaondoka na Dar Express ya saa 4 kamili lakini anasema " Dad nimehuzunika sana kwani katika ticket wameandika saa 4 kamili, ila basi limeondoka saa tano na robo" huu ni ujumbe wa kweli na na akaendelea" Dad unajua nitafika Dar usiku, nampigia Vanessa aje kunichukua pale Ubungo. Gari lenyewe chafu, Lugha ya yule dada pale ofisini pia ilikuwa harsh imeniondolea mood". Nikampigia na kumtakia safari njema yenye uvumilivu na amani na maneno kidogo ya kimapenzi ili afarijike zaidi.... Kwa meseji hii ya leo kweli Dar Exp hawako vizuri. Ila nikalaumu rohoni kidogo...."kwanini asichague gari zuri, kwanini hakufanya online booking ya precision air ili asichoke sana...kuona tu wakwe?....atarudi lini? atakuwa salama? hajapoteza passport yake (hati ya kusafiria).........ni hii story ya usafiri kafiri na kwa kuwa imetokea kwa "my other half".