Afisa Mteule Drj 2
JF-Expert Member
- Mar 21, 2017
- 3,865
- 4,506
picha zako ulupigia nokia ya tochi?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
picha zako ulupigia nokia ya tochi?
Unaijua flyover wewe?
Tulikotoka
Ujenzi wa daraja hilo lililopewa jina la Mfugale ulioanza miaka miwili iliyopita umegharimu Sh bilioni 92 hadi kukamilika kwake, huku Serikali ya Japan kupitia Shirika la Maendeleo la nchi hiyo (JICA) likichangia Sh bilioni 26. Jina la Mfugale limetokana na jina la Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Barabara (Tanroads), Patrick Mfugale, ambaye Rais Magufuli alisema amekuwa na mchango mkubwa katika ujenzi wa miundombinu nchini na kumpa heshima ya kulitunuku daraja hilo jina lake.
Mkataba wa ujenzi wa daraja hilo, ulisainiwa Oktoba 15, mwaka 20 1 5 kati ya Wakala wa Taifa wa Barabara (Tanroads) na Kampuni ya Sumitomo Mitsui Construction Co. Ltd. Juzi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika kuanzia saa 2 asubuhi huku akiwataka wananchi, viongozi wa siasa kutoka vyama mbalimbali kujitokeza kwa ajili ya kushuhudia uzinduzi huo wenye historia ya kipekee nchini.
View attachment 879144
Rais Magufuli amewasili katika eneo hilo zinapokutana barabara za Mandela na Nyerere na amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda
RC Makonda
Makonda wakati anamkaribisha Rais amemsifu na kumwambia kuwa ujenzi wa fly-over hiyo utaondoa usumbufu wa msongamano wa barabarani na kusaidia watu kuwahi maofisini, majumbani na hata Airport
"Tumewaalika wabunge wote wa Dar katika Uzinduzi wa ‘Flyover’ ya Mfugale ila Wabunge wa Kawe, Ubungo na Kibamba hawajaja... aaah!
Ndoa za wengi zilitetereka kutokana na foleni ya TAZARA, wengine walidanganya kumbe walikuwa ‘guest’ tu
Daraja la Nyerere la Kigamboni kwa sasa linaingiza takribani Tsh. Milioni 800 kwa mwezi"
Pia amemuomba Rais afanye ziara katika Mkoa wa Dar kwani wanahitaji sana ziara hiyo na wanaona wivu anapokuwa katika mikoa mingine na kupiga picha na wananchi
Mkurugenzi Mtendaji TANROADs
Mwaka 2008, Tanzania iliandaa ‘Master Plan’ ya kupunguza msongamano jijini Dar. 2013 Japan wakajitokeza kuwa watatusaidia kujenga daraja hili; 2014 ilitangazwa tenda! Wazabuni walikuja na gharama kubwa
Japan iliongeza ufadhili hadi Bilioni 103 mwaka 2015 Machi, Mkandarasi mmoja alikuja lakini gharama zake zilikuwa mara mbili zaidi. Tulifanya ‘Selective Tendering’ ambapo mkandarasi aliyejenga daraja hili alipatikana
Daraja hili limejengwa kwa nguzo kubwa 26; zimekaa juu ya Piles 133. Daraja lina urefu wa zaidi ya km 1. Linaweza kubeba tani 180 kwa wakati mmoja. Daraja hili linaweza kutumika kwa zaidi ya miaka 100. Limejengwa kwa jumla ya Sh. Bilioni 92
Tunao mkakati wa kujenga BRT ya kutoka mjini(CBD) hadi Gongo la Mboto katika awamu ya 3
Balozi wa Japan
Naamini watanzania wote wamefurahi kuona Flyover ya kwanza nchini Tanzania. Daraja hili litapunguza msongamano jijini Dar. Nafarijika kuwa nikiwa narudi Japan nitatumia ‘Mfugale Flyover’
Eng. Ninatubu Lema(ERB)
Mhandisi Patrick Aaron Lipilima Mfugale ametumikia taaluma ya Uhandisi kwa miaka 41
- Alizaliwa Ifunda, Iringa na alikamaliza Sekondari mwaka 1975. Alipata 1st Degree nchini India, Masters nchini Uingereza
- Aliajiriwa Wizara ya Ujenzi 1977
Mfugale ametumia muda wake mwingi wa kazi kama Mtaalamu wa Madaraja. Alibuni daraja la Malagarasi; ameshiriki ktk ujenzi wa madaraja ya Mkapa, Umoja, Rusumo, Kikwete, Nyerere, Mto Sibiti, Kilombero na mengine mengi (zaidi ya 1,400 nchini)
Mhandisi Patrick Mfugale ni Mtendaji Mkuu wa TANROADS; leo atapata heshima kubwa sana kwa Flyover ya kwanza Tanzania kupewa jina lake!
Elias J. Kwandikwa
Mradi huu jumla umegharimu Bilioni 106. Serikali ya Tanzania imegharimia kodi zote. Daraja hili litapunguza msongamano jijini Dar. Toka Flyover imeanza kutumika, msongamano eneo la TAZARA umepungua kwa kiwango kikubwa
Miradi inayotarajiwa jijini Dar kwa kushirikiana na JICA:
> Upanuzi wa barabara ya Morocco - Mwenge
> Ujenzi wa Daraja la Gerezani (Kariakoo)
Rais Magufuli
Natoa pole kwa familia zilizoondokewa na wapendwa wao kufuatia ajali ya #MVNyerere na kuwaombea majeruhi uponyaji wa haraka. Nawashukuru watanzania kwa mshikamano walioonyesha
Ajali hii ya #MVNyerere iwe funzo kwetu. Ajali kama hizi zinaepukika, na zikitokea basi madhara yake yanaweza kuwa madogo kama tukipata funzo kwa kilichotokea
Nawapongeza Wizara ya Ujenzi, TANROADS na Wahandisi washauri kwa kusimamia ujenzi wa #MfugaleFlyover. Daraja limegharimu Bilioni 106.65; Japan wamechangia kiwango kikubwa cha pesa hii, ni marafiki wa kweli kwenye masuala ya maendeleo
Nampongeza Mbarawa ambaye alikuwa Waziri wa Ujenzi wakati ujenzi wa #MfugaleFlyover unaanza
Nakumbuka wakati Daraja la Umoja linaandaliwa kujengwa, nilimwita Mfugale anisaidie design ya Daraja hilo; nilipoipeleka kwa marais wa Tanzania na Msumbiji, ikapitishwa. Wakati wa uzinduzi wala hakutambulishwa
Mwaka 2008 Mfugale na mwenzake walipewa maagizo wakayakataa, Katibu Mkuu wa wakati huo aliwaokoa; mwenzake (marehemu Mjungi) alijiua kwa kujipiga risasi lakini Mfugale alivumilia. Ndo gharama ya kusimamia maadili
Ujenzi wa Flyover ya Ubungo itagharimu Bilioni 247. Itakuwa flyover ya aina yake kwa hapa Dar es Salaam! Wazaramo watasema ‘Ina ghorofa 3’
Tunajenga barabara ya njia 6 kutoka Kimara kwenda Kibaha kwa Sh. Bilioni 140 na fedha zote zinatolewa na Serikali ya Tanzania. Kutakuwa pia na njia ndogo 2 (service road). Bomoabomoa ya Kimara ilizingatia sheria!
Katika #MfugaleFlyover, nataka zifungwe kamera kote! Kazi hii ianze mara moja. Hatutaki watu wajiue hapa. Na madaraja mengine yote yatakayojengwa yawekewe kamera
Kwa kazi alizozifanya Eng. Mfugale, Flyover hii ilistahili kuitwa jina lake. Hakupendelewa, ni haki yake. Wataalamu wengine wamuige!
Gharama za umeme hapa nchini ni kubwa mno. Ni kikwazo katika ushindani wa viwanda. Bila umeme wa uhakika, viwanda ni ndoto!
Naomba flyover ya Gerezani ifanyiwe kazi ambayo tayari hadi tenda yake imeshatangazwa
Nawaomba Japan pia waikumbuke barabara ya Morocco-Mwenge waliyoahidi, imechukua muda mrefu!
Baadhi ya mikwamo hapa nchini imeletwa na wataalam ambao ni watanzania wenzetu! Wataalam wetu walipendekeza vyoo vya mradi wa Stiegler's Gorge vijengwe kilomita 10 toka eneo la mradi...
Miradi hii inaumiza baadhi ya watu. Tusitumike kukwamisha maendeleo ya watanzania. Yapo mengi tunayaweza kwa fedha zetu. Fedha za kujenga Stiegler's Gorge zipo!
Hatuwezi kuingia Uchumi wa Kati wakati tuna umeme unaokatikakatika. Hatuwezi kwenda huko bila kuwa na Flyovers, miundombinu ya Reli n.k. Maendeleo hayana chama!
Sijasema wapinzani wote waje, ila wale wanaoelemewa na mizigo. Wakija tutawapokea kwa mikono miwili (akimtolea mfano Waitara)
Nawapongeza sana wana Dar es Salaam kwa mshikamano wenu. RC Makonda ameomba nifanye ziara. Nitafanya hivyo, msiwe na wasiwasi nitawatembelea
Rais Magufuli kuzindua Flyover ya TAZARA. Yamaliza Foleni iliyokuwa ikisababisha hasara ya Tsh. Bilioni 400 kwa Mwezi - JamiiForums
Barabara ya Njia sita yaiva: Baada ya bomoabomoa, ujenzi waanza kwa kasi Kimara - JamiiForums
He is intelligent politicianMakonda anajua kucheza na saikolojia ya bosi wake ni kusifia mwanzo mwisho na kutaja idadi ya barabara anajua ugonjwa wake
Hata yule msaliti wa nchi yetu angekuwepo nadhani angeenda. Augue pole.Ingejengwa moja wapo ya hivi si nchi nzima ingelikusanyika Dar! Kinjia kidogo wamekusanyika serikali, viongozi wa dini zoteeeeeeeeeeeeeee (kama kweli tuna viongozi wa dini)
View attachment 879233
8 of the World's Most Amazing Flyovers You Need to See to Believe
Uongo wakati mi nimeona kwa macho yangu, umepita saa ngapi hapo leo? Nenda pale sasa hivi uone kwa macho yako, na usisahau kutupigia pichaAcha uongoo
Kwa waliokuwepo karibu na eneo la tukio, tunaomba picha
Duuu, kumbe hadi uhasibu? Mi nadhani ule wizi unaosemwa ni CAG ni wizi wa ajabu sana, maana kadri walivyoiba ndio miundombinu zinakuwa bora, waongeze tu kasi ya kuiba kwa kweliSio chang'ombe tu hapa uhasibu zegelina mwagika muda simrefu itakuwa kama tazara.
Nikijenga kwa 700m nikala 500m..bado nimeiba acha upompoma wewe.Duuu, kumbe hadi uhasibu? Mi nadhani ule wizi unaosemwa ni CAG ni wizi wa ajabu sana, maana kadri walivyoiba ndio miundombinu zinakuwa bora, waongeze tu kasi ya kuiba kwa kweli
Sasa si bora anaekula 500m katika 700m, kuliko anaekula 700m yote!!!Nikijenga kwa 700m nikala 500m..bado nimeiba acha upompoma wewe.
#MaendeleoHayanaChama
Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna usemi unasema uongo una panda lift, ukweli una tembea kwa miguu.Duuu, kumbe hadi uhasibu? Mi nadhani ule wizi unaosemwa ni CAG ni wizi wa ajabu sana, maana kadri walivyoiba ndio miundombinu zinakuwa bora, waongeze tu kasi ya kuiba kwa kweli
Sasa punguani ni mimi au wewe unaebisha bila hoja, kwamba sijaona picha ya makalio yako means huna makalio?Nimekuja speed nikifikiri kuwa nitakutana na picha kumbe punguani ndiye kaleta uzi.
Acha ushabiki maandazi.Mbona ni kama baadhi ya MATAGA mmeanzisha uzi na kujijibu wenyewe.