Dar: Grace Mushi ambaye alimchomea ndani Mpenzi wake, akamatwa na Polisi

Dar: Grace Mushi ambaye alimchomea ndani Mpenzi wake, akamatwa na Polisi

MULIROOO.jpg

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ACP Muliro Jumanne,

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linamshikilia Grace Mushi (25) kwa tuhuma za kumuua aliyekuwa mpenzi wake Khamis Abdallah (25), mkazi wa Mbezi Makabe baada ya kumfungia ndani ya nyumba na kuimwagia mafuta ya petroli na kisha kuichoma moto nyumba hiyo.

Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo Muliro Jumanne, na kusema kuwa tukio hilo limetokea Julai 16, 2021, majira ya saa 8:30 usiku na uchunguzi umebaini kwamba wapenzi hao walikuwa na mgogoro mkubwa wa mapenzi.

"Baada ya tukio hilo mtuhumiwa alijaribu kutoroka lakini kwa kushirikiana na wananchi alikamatwa na uchunguzi wa awali umeonesha kwamba ulikuwepo mgogoro mkubwa wa kimpenzi kabla ya kufanyika kwa tukio hili la mauaji ya kikatili," ameeleza Kamanda Muliro.
 
I know, ukumbuke ukiandika hivyo kwenye usajili ni watu wawili tofauti, mfano; wengine huandika Margreth - Margrate, Matthew - Mathew, Mushi - Mushy, Emmanuel - Immanuel etc hayo majina ni tofauti Mkuu
Wachana nao. Jina halina tafsiri kwenye kuandika. Ukiitwa Mnazi Mmoja huwezi sema akija mzungu utamwambia naitwa One coconut. Grace na Neema ni majina mawili tofauti kabisa.
 
Isome hii comment ya cariha vizuri ina madini ya kutosha, hii siri sikutaka kuisema ila huyu cariha kaitaja hapa

Wanaume wengi sana wanauliwa kwa sumu ya pole pole, kimya kimya..

Wamama wa Sinza ndo vinara wa huu mchezo[emoji22][emoji848]

Ni balaa
Aiseee.. Umeongea kitu akili yangu ikashtuka na kufanya utafiti wa dakika tano nikapata majibu.
Kuna ukweli fulani nimeuona.. miji kumi na mbili (ninayoifahamu) hapo Sinza wamebaki wanawake wajane wanadunda tu mitaani.
 
Duh ongezea nyama kidogo sinza kubwa ujue
 
Dah..Noma sana Mapenzi yanaua,
Pumzika kwa Amani Mwana.
 
Tatizo hamna hata basic ya Elimu ya moto kila ukitokea mnauchukulia poa wangapi sio walevi na wameungua na familia nzima ndani moto wa petrol na gesi ni hatari sana...Mungu amlaze mahali pema Mwamba
Mkuu ni watoto hawa. Wasamehe bure. Moto umeua wenye makomandoo wenye mafunzo maalum. Moto ni kuomba usitokee. Hauna ujanja.
 
Aiseee.. Umeongea kitu akili yangu ikashtuka na kufanya utafiti wa dakika tano nikapata majibu.
Kuna ukweli fulani nimeuona.. miji kumi na mbili (ninayoifahamu) hapo Sinza wamebaki wanawake wajane wanadunda tu mitaani.
Ndo hivo mkuu

Na wanaume hawajui hii kitu kabisa[emoji848]
 
Kweli kabisa[emoji848]

Ukiona mwanaume anakunyima hela ujue hakupendi kabisa

Chapa lapaa
Vp na sisi tukiona wanawake hawatufanyii majukumu kama kufua, kupiga deki na kupika kipind Cha uchumba tuje na conclusion gan hapo [emoji2577]
 
Naskia wachaga wa old Moshi kiasili ni watu wa marangu ..kule old Moshi walienda kufata Maeneo ..

Ni kama wameru ..kiasili ni wachaga wa machame
Yes dear. Ni waanjo wote. Kilema, kirua, marangu huko. Old moshi etc. Wengine wanahamiaga eneo kwasababu ya ugomvi. Wote wanawekwa kundi moja la waanjo
 
Back
Top Bottom