Dar: Hali ya Soko la 'Magunia' yahatarisha Afya za Wananchi

Dar: Hali ya Soko la 'Magunia' yahatarisha Afya za Wananchi

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Hali ya Soko la 'Magunia' Msasani bonde la Mpunga linavyoonekana pichani, ambapo soko hilo hutumiwa na Wakazi wa maeneo mbalimbali ikiwemo Masaki na Oysterbay kujipatia Mahitaji yao ya kila siku

Pamoja na umuhimu wa Soko hilo kwa maeneo hayo, suala la usafi wa Mazingira na Miundombinu yake imekuwa ni changamoto kwa muda mrefu, hali inayohatarisha Afya ya Wakazi hao na hata kusababisha Magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu, licha ya ushuru kukusanywa Kila siku Sokoni hapo

60BD0117-4AC3-4640-8807-E815EE22EF93.jpeg

Chanzo: Michuzi
 
Tuna kazi za msingi kwanza za Kitaifa hilo soko ni jambo dogo litashughulikiwa na serikali ya mtaa.
 
Mbona lipo kwenye hali ya kawaida hasa kwa kipindi hiki cha masika ?
 
Aaah,
Hapo pazuri kabisaaaa,
We hujaona uchafu nini? Tembelea hata kariakoo uone shida na uchafu na vurugu zinavyosababisha maradhi ya miripuko
 
Hali ya Soko la 'Magunia' Msasani bonde la Mpunga linavyoonekana pichani, ambapo soko hilo hutumiwa na Wakazi wa maeneo mbalimbali ikiwemo Masaki na Oysterbay kujipatia Mahitaji yao ya kila siku

Pamoja na umuhimu wa Soko hilo kwa maeneo hayo, suala la usafi wa Mazingira na Miundombinu yake imekuwa ni changamoto kwa muda mrefu, hali inayohatarisha Afya ya Wakazi hao na hata kusababisha Magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu, licha ya ushuru kukusanywa Kila siku Sokoni hapo

View attachment 2205955

Chanzo: Michuzi
Masoko yote ya Dsm,ukipita pale soko la ndizi mabibo utashangaa......Kuna watu wanakodisha mabuti kabisa.......na huko ndani tope linafika kwenye ugoko kabisa halafu kuna watu wanachukua Kodi
 
Back
Top Bottom