Uchaguzi 2020 Dar: Helkopta ya Kampeni ya Tundu Lissu, yanyimwa kibali cha kutumia anga, ni baada ya kuomba kibali hapo jana

Tena hiyo chopper isiruhusiwe kabisa kwenda huko. Apande magari aende zake.
 
Maana TMA jana walitoa tahadhari ya upepo mkali, isijekuwa Tundu lissu analindwa dhidi ya ajali ya helkopta inayoweza kusababishwa na upepo!
 
Kuna wakati unashindwa kuelewa hawa watu wana roho mbaya ama Wana wivu.

Inakuwaje Lissu aogopwe namna hii ilhali walio madarakani wana kila kitu kinachowahakikishia ushindi?

Tume, mahakama, polisi na jeshi vyote vipo upande wao.

Kuwaachia wananchi wapate furaha ya moyo mara moja katika miaka mitano iliyopita napo imekuwa nongwa.

Watawala nia yao ni kuishi peke yao bila shaka.

Inachosha!
 
Barafu Yuko wapi sikuhizi? Angetupa habari za jikoni
 
Watumie barabara, kwa kuwa ni Nzuri na zinapitika, hamna haja ya kelele za ma helcopter.
Mwishoe limdondoshe waanze kisingizio.
Mpuuzi wewe !!. Yaani umpangie mpinzani wako namna ya campaign ?!.
 
Sasa nakubaliana na Sirro kuwa kuna mtu anataka afe, polisi chukueni jukumu la kumlinda asije jinyonga akasingizia kauwawa
 
Helicopter ya kwenda kupandia airport ??
 
Mkuu maana ya kuleta habari kwa fumo hii ni kwamba ili sisi hapa jukwaani tujadili tukiegemea upande mmoja tu kuwapa haki chadema huku tukiwa hatujui ya upande wapili ambapo inawezekana hawakufuata taratibu husika.

Fikiria kibali kimeombwa jana kwa mujibu wa hiyo taarifa hapo na huwezi jua hiyo jana ni saa ngapi ( kwa siku moja wanataka mamlaka ya anga itoe kibali Cha kurusha ndege)

Wakati huo kumbuka kesho toa tamko kuwa Kuna njama ovu dhidi yake kwenye hiyo ndege ili apate ajali ,hapo unadhani mamlaka itaruhusu kirahisi? ( Mdomo wake ndio unamponza)

Alafu mtu hujapewa kibali bado lakini tayari usha andaa safari unataka kurusha ndege.
 
Kweli sasa huu ni zaidi ya ushetani! hata shetani hawezi kufanya huu unyama!
Hivi ccm wanafikiri hii nchi ni yao peke yao?
Hivi hawa watu watatutesa hivi hadi lini?
 

Kamanda twambie ameambiwa amezuiwa kwa sababu zipi?
 
Hai ni chadema ndo wanalialia baada ya kuona hawana mwelekeo. Kwani Salum Mwalimu yuko wapi angeenda hata yeye kuokoa jahazi.
Chadema hata mipango ya mikutano imewashinda, nMnyika anawahujumu. Agalia ccm Mgombea mwenza yuko kivyake anasaka kura, Waziri mkuu yupo kivyake anasaka kura, shida ya chadema wanaye mgombea ambaye hawezi kusimama peke yake, ni kunguru asiyefugika.juzi kati kaachwa peke yake kule Pemba akachafua hali ya hewa kwa kumtosa mgombea wa Chadema Zanzibar.Mwaka huu mnalo inabidi muandamane na mgombea kama kumbikumbi,KAAAAZI KWELI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…