Uchaguzi 2020 Dar: Helkopta ya Kampeni ya Tundu Lissu, yanyimwa kibali cha kutumia anga, ni baada ya kuomba kibali hapo jana

Uchaguzi 2020 Dar: Helkopta ya Kampeni ya Tundu Lissu, yanyimwa kibali cha kutumia anga, ni baada ya kuomba kibali hapo jana

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA

Ratiba ya mikutano 5 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mhe. Tundu Lissu, iliyopangwa kufanyika leo mkoani Pwani, imevurugika baada ya helkopta aliyokuwa aitumie kufika katika maeneo hayo, kuzuiliwa kwa kunyimwa kibali na Mamlaka ya Anga nchini, muda mfupi kabla ya kuruka.

Taarifa za kukataliwa kwa helkopta hiyo kuruka zilitolewa kwa Ofisa Mnadhimu wa Kampeni, Amani Golugwa, wakati msafara wa Mhe. Lissu ukielekea kupanda ndege baada ya kumaliza taratibu zote za ukaguzi wa kiusalama Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) terminal I.

Ofisa wa Mamlaka ya Anga aliyewasilisha taarifa hiyo wakati msafara wa Mhe. Lissu umeshatoka nje ya jengo la abiria, ametoa sababu zisizoeleweka kuzuia helkopta hiyo kuruka kutoka Uwanja wa JNIA kuelekea Bagamoyo, Chalinze, Mlandizi na Kibaha, wakati kibali chake kiliombwa tangu jana.

Kutokana na hatua hiyo, Chadema imelazimika kutafuta njia mbadala ili Mgombea Urais Mhe. Lissu na msafara wake, aweze kuendelea na ratiba ya mikutano kwa kadri inavyowezekana. Mbali ya Mhe. Lissu, abiria wengine waliokuwa watumie usafiri huo ni watu 3, akiwemo Ofisa Mnadhimu wa Msafara Amani Golugwa, Katibu wa Mgombea, David Jumbe, msaidizi wa masuala ya ulinzi pamoja na rubani wa ndege hiyo.

Imetolewa leo, Alhamis, Septemba 10, 2020 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano


Tena hiyo chopper isiruhusiwe kabisa kwenda huko. Apande magari aende zake.
 
Maana TMA jana walitoa tahadhari ya upepo mkali, isijekuwa Tundu lissu analindwa dhidi ya ajali ya helkopta inayoweza kusababishwa na upepo!
 
Kuna wakati unashindwa kuelewa hawa watu wana roho mbaya ama Wana wivu.

Inakuwaje Lissu aogopwe namna hii ilhali walio madarakani wana kila kitu kinachowahakikishia ushindi?

Tume, mahakama, polisi na jeshi vyote vipo upande wao.

Kuwaachia wananchi wapate furaha ya moyo mara moja katika miaka mitano iliyopita napo imekuwa nongwa.

Watawala nia yao ni kuishi peke yao bila shaka.

Inachosha!
 
Poleni sana.. Unaonaje ukaziweka sababu hizo unazosema hazieleweki ili tuzijue huenda zikawa zinaeleweka ila wewe ndio hujazielewa, hapa kuna wadau wabobezi wa hizo mambo wanaweza kuchanganua ili mjipange vizuri baadae ktk harakati zenu.. Alaf punguza malalamiko kua tayari kujifunza kila cku.
Asante

Sent from my SM-J260F using JamiiForums mobile app
Barafu Yuko wapi sikuhizi? Angetupa habari za jikoni
 
Watumie barabara, kwa kuwa ni Nzuri na zinapitika, hamna haja ya kelele za ma helcopter.
Mwishoe limdondoshe waanze kisingizio.
Mpuuzi wewe !!. Yaani umpangie mpinzani wako namna ya campaign ?!.
 
Hawakupata watu bagamoyo. Msilete visingizio. Hujuma gani wanaweza kufanyiwa? Amekimbia tu aibu ya kuhutubia uwanja mtupu.

2015 Lowassa alishindwa kufika Tunduma lakini kwenye Mkutano watu walikua wamejaa toka saa 1 asubuhi wanamsubiria. Nanyinyi tuonesheni watu waliokua wanamsubiria Tundu Lissu ili tujue kweli kuna hujuma zimefanywa.
Sasa nakubaliana na Sirro kuwa kuna mtu anataka afe, polisi chukueni jukumu la kumlinda asije jinyonga akasingizia kauwawa
 
Helicopter ya kwenda kupandia airport ??
Hawakupata watu bagamoyo. Msilete visingizio. Hujuma gani wanaweza kufanyiwa? Amekimbia tu aibu ya kuhutubia uwanja mtupu.

2015 Lowassa alishindwa kufika Tunduma lakini kwenye Mkutano watu walikua wamejaa toka saa 1 asubuhi wanamsubiria. Nanyinyi tuonesheni watu waliokua wanamsubiria Tundu Lissu ili tujue kweli kuna hujuma zimefanywa.
 
Hii habari imetolewa na afisa habari wa chama cha Chadema kweli?

Kwanini asiweke hizo sababu zisizoeleweka kwenye hilo bandiko? Na badala yake anaelezea mambo ya kutafuta sijui usafiri

Kwangu mimi hii imekaa kijanjajanja zaidi kama vile wanatafuta excuses

Ushauri waache kulalama watafute mbadala, wananchi wanawasubiri na muda unasonga hausubiri
Mkuu maana ya kuleta habari kwa fumo hii ni kwamba ili sisi hapa jukwaani tujadili tukiegemea upande mmoja tu kuwapa haki chadema huku tukiwa hatujui ya upande wapili ambapo inawezekana hawakufuata taratibu husika.

Fikiria kibali kimeombwa jana kwa mujibu wa hiyo taarifa hapo na huwezi jua hiyo jana ni saa ngapi ( kwa siku moja wanataka mamlaka ya anga itoe kibali Cha kurusha ndege)

Wakati huo kumbuka kesho toa tamko kuwa Kuna njama ovu dhidi yake kwenye hiyo ndege ili apate ajali ,hapo unadhani mamlaka itaruhusu kirahisi? ( Mdomo wake ndio unamponza)

Alafu mtu hujapewa kibali bado lakini tayari usha andaa safari unataka kurusha ndege.
 
Kweli sasa huu ni zaidi ya ushetani! hata shetani hawezi kufanya huu unyama!
Hivi ccm wanafikiri hii nchi ni yao peke yao?
Hivi hawa watu watatutesa hivi hadi lini?
 
Kuna wakati unashindwa kuelewa hawa watu wana roho mbaya ama Wana wivu.

Inakuwaje Lissu aogopwe namna hii ilhali walio madarakani wana kila kitu kinachowahakikishia ushindi?

Tume, mahakama, polisi na jeshi vyote vipo upande wao.

Kuwaachia wananchi wapate furaha ya moyo mara moja katika miaka mitano iliyopita napo imekuwa nongwa.

Watawala nia yao ni kuishi peke yao bila shaka.

Inachosha!

Kamanda twambie ameambiwa amezuiwa kwa sababu zipi?
 
Hai ni chadema ndo wanalialia baada ya kuona hawana mwelekeo. Kwani Salum Mwalimu yuko wapi angeenda hata yeye kuokoa jahazi.
Chadema hata mipango ya mikutano imewashinda, nMnyika anawahujumu. Agalia ccm Mgombea mwenza yuko kivyake anasaka kura, Waziri mkuu yupo kivyake anasaka kura, shida ya chadema wanaye mgombea ambaye hawezi kusimama peke yake, ni kunguru asiyefugika.juzi kati kaachwa peke yake kule Pemba akachafua hali ya hewa kwa kumtosa mgombea wa Chadema Zanzibar.Mwaka huu mnalo inabidi muandamane na mgombea kama kumbikumbi,KAAAAZI KWELI
 
Back
Top Bottom