Uchaguzi 2020 Dar: Helkopta ya Kampeni ya Tundu Lissu, yanyimwa kibali cha kutumia anga, ni baada ya kuomba kibali hapo jana

Leo nitawalaumu kidogo CHADEMA na mnivumilie kwani nina tatizo moja la kutovumilia 'Upuuzi' ambao nauona hata kama nitakaowasema ni Marafiki zangu. Kama ninavyowasema CCM ( Chama chagu Shabiki ) nanyi pia 'nawalaumu' kwani hakuna asiyejua kuwa 'hampendwi' na Mamlaka / Dola hivyo nilitegemea muwe na 'anticipations' kwa mambo mengi tu ili mje na 'alternatives' zenu za 'Kukabiliana' nazo lakini cha 'Kusikitisha' CHADEMA 'mmewekeza' mno katika Kukimbilia kutoa 'Lawama' pale mnapokuwa 'mnabinywa' na hao 'mnaowalaumu' 24/7. Badilikeni haraka.
 
Kwahiyo hawakuzuiwa? Sometimes msiwe wapuuzi kupita kiasi
Ile ndege yaliyotumia Mwanzo alipewa ruhusa na Kenya nadhani. Kama sio Somaliland.
Weka barua ya zuio huwezi kuzuiwa vebrally tu, ili Serkali tuisute
 
Walioweka zuio ndio watoe sababu
 
Mbona sababu za kuzuiliwa Hiyo helikopta Hawakuweka?

Chadema waongo helikopta hata Gwajima anayo yaweza kukufuata ulipo kukubeba huhitaji kwenda airport sababu ile sio ndege kuwa kuruka na kutua ni airport!

Diamond mbona huenda maonyesho kibao na helikopta na huwa hapandii airport?

Chadema acheni usanii sisi ndege tunapanda sana Kwa hilo la helikopta ni fix waongo nyie
Wanaenda kupanda hell copta airport tena terminal 3? Waongo
 
Nimegundua sasa kwanini moyo wangu ulikuwa mzito tangu asubuhi kuhusiana na huu usafiri..nilikuwa nimeshanusa hujuma japo sikujua ni hujuma gani
Hawakupata watu bagamoyo. Msilete visingizio. Hujuma gani wanaweza kufanyiwa? Amekimbia tu aibu ya kuhutubia uwanja mtupu.

2015 Lowassa alishindwa kufika Tunduma lakini kwenye Mkutano watu walikua wamejaa toka saa 1 asubuhi wanamsubiria. Nanyinyi tuonesheni watu waliokua wanamsubiria Tundu Lissu ili tujue kweli kuna hujuma zimefanywa.
 
Msilaumu bure kwani pengine kulikuwa na shari imeepukwa!!! Everything happens for a reason!
 
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA

Ratiba ya mikutano 5 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mhe. Tundu Lissu, iliyopangwa kufanyika leo mkoani Pwani, imevurugika baada ya helkopta aliyokuwa aitumie kufika katika maeneo hayo, kuzuiliwa kwa kunyimwa kibali na Mamlaka ya Anga nchini, muda mfupi kabla ya kuruka.

Taarifa za kukataliwa kwa helkopta hiyo kuruka zilitolewa kwa Ofisa Mnadhimu wa Kampeni, Amani Golugwa, wakati msafara wa Mhe. Lissu ukielekea kupanda ndege baada ya kumaliza taratibu zote za ukaguzi wa kiusalama Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) terminal I.

Ofisa wa Mamlaka ya Anga aliyewasilisha taarifa hiyo wakati msafara wa Mhe. Lissu umeshatoka nje ya jengo la abiria, ametoa sababu zisizoeleweka kuzuia helkopta hiyo kuruka kutoka Uwanja wa JNIA kuelekea Bagamoyo, Chalinze, Mlandizi na Kibaha, wakati kibali chake kiliombwa tangu jana.

Kutokana na hatua hiyo, Chadema imelazimika kutafuta njia mbadala ili Mgombea Urais Mhe. Lissu na msafara wake, aweze kuendelea na ratiba ya mikutano kwa kadri inavyowezekana. Mbali ya Mhe. Lissu, abiria wengine waliokuwa watumie usafiri huo ni watu 3, akiwemo Ofisa Mnadhimu wa Msafara Amani Golugwa, Katibu wa Mgombea, David Jumbe, msaidizi wa masuala ya ulinzi pamoja na rubani wa ndege hiyo.

Imetolewa leo, Alhamis, Septemba 10, 2020 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano

Wapiga kura wako barabarani, yeye anapaaa, hataki tumpungie mkono? Awe siliazi kidogo lissu
 
Huu ni upumbavu uliotukuka.
 
Hawakupata watu bagamoyo. Msilete visingizio. Hujuma gani wanaweza kufanyiwa? Amekimbia tu aibu ya kuhutubia uwanja mtupu.

2015 Lowassa alishindwa kufika Tunduma lakini kwenye Mkutano watu walikua wamejaa toka saa 1 asubuhi wanamsubiria. Nanyinyi tuonesheni watu waliokua wanamsubiria Tundu Lissu ili tujue kweli kuna hujuma zimefanywa.
Kwahiyo 2015 lowassa alishinda?
 
Back
Top Bottom