Dar: Inasemekana tukio hili la utekaji limetokea Kiluvya, kutokana na uzito wa jamaa walishindwa kumchukua. Hakuna aliyetoka kumsaidia

Nani atamfunga paka kengele?. Unaweza ukajipeleka kusaidia afu ukajikuta uko peke Yako wamekuachia msala,

Kila mtu huipigania nafsi yake ni ngumu sana mtu aende kusaidia peke yake vipi akipigwa risasi?

Muwalaumu hao wanaoteka , sasa raia wa kawaida ajipeleke afu akutane na watu Wana bunduki
 
Fisiem imeleta laana katika nchi hii,watu wanashindwa kuandamana wanashindwa kusaidiana basi hata huruma tuoneane unamuona mwenzako anafanyiwa hivi unashindwa hata kuuliza?

Basi hata kelele unaogopa kupiga? Why watu wanakuwa hivi?

Ukiona haya ujui nchi imeoza haya mambo pale ukifanya pale bububu (Zanzibar) hao wote wangekuwa maiti sasa hivi.
 
Hao polisi kama wapo serious kukamata hilo kundi la wahuni na wauwaji sijui wapewe ushahidi gani tena maana mpaka sura za wahusika safari hii wanazo kwenye camera.

Ngoja siku ya briefing usikie mikwara ya makamanda halafu baada ya week mbili kimya, kama kwenye sakata la marehemu mzee Kibao.

Mtuhumiwa mmoja unaambiwa alipanda basi toka linaanza safari, marehemu kachukuliwa kwenye basi lililojaa abiria na mpaka leo hakuna hata updates wamefikia wapi.

Haya mambo ya kutaka kuchukua maisha ya watu kirahisi rahisi kwakweli yanasikitisha sana.
 
Hivi Bastola ni tsh ngapi...kibali ntapambana nacho nikipate...kwa hali ya sasa Bastola ni Basic need kama mbwai iwe mbwai tufee wote maninaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…