Dar: Inasemekana tukio hili la utekaji limetokea Kiluvya, kutokana na uzito wa jamaa walishindwa kumchukua. Hakuna aliyetoka kumsaidia

Dar: Inasemekana tukio hili la utekaji limetokea Kiluvya, kutokana na uzito wa jamaa walishindwa kumchukua. Hakuna aliyetoka kumsaidia

ile ya eti mteka mtu mzima anaepiga mayowe ya kuomba msaada huku anaerekodi video na mashuhuda wengine wakikodoa macho na kushuhudia action movie hiyo kwa umakini mkubwa 🐒
Movie eeh au siyo vipi Ile ya Zakaria Tarime ilikuwa Bonge moja la movie. Mnarudi lini kwa jamaa kumalizia movie?
 
Hawa jamaa ipo siku watakufa wamebong'oka wataingia kwenye 18 moja miili ya itakuwa sehemu ya kunolea panga muraa
 
hebu share kipande cha video kwa faida ya wadau gentleman 🐒
Kakifate kwa Zakaria si yupo au aliondoka nacho jamaa kutibiwa south Africa. Na alipopiga nduru mkakimbilia sheli kwake huku mkisema sisi ni maafisa wa usalama wa serikali na mzee Zakaria akaanza kutuliza wakurya pale msitembezewe panga. Mkawa mnatamani msaada uje chapu. Na kukosa Zakaria mwenyewe kutuliza watu mlikuwa mnachezea panga vizuri sana mura
 
Wakuu,​

Nimekutana na video hii duniani huko, pamoja na kujaribu kupiga kelele watu waliuchuna. Angalu video hii imepatikana, kama ni tukio la kweli wasiyojulikana wataanza kujulikana.

=====

Kumbusho Dawson kaandika haya kupitia ukurasa wake akisindikiza video hiyo;

"Tukio hili la utekaji limetokea jana Rovvenpec Resort, Kiluvya madukani, kutokana na nguvu za mwamba aliwashinda watekaji.
"Inasikitisha Sana kwamba hakuna pamoja Na kwamba kulikuwa na watu wanashuhudia hakuna mtu aliejitokeza kutoa msaada inasikitisha.

Pia soma: Kupambana na watu wasiojulikana: Ukija kukamatwa na polisi bila uniform na hajaambatana na kiongozi wa eneo husika piga firimbi, kusanya nzi

"Mstari unaotofautisha akili za nyumbu na Watanzania ni ndogo kama punje ya haradali. Mtu anakamatwa watu wanashangàa kama kundi la nyumbu porini. Shame be upon you."

Kupata matukio ya nyuma kuhusu watu wasiyojulikana ingia hapa: Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana
 
Attachments

  • IMG-20241113-WA0005.jpg
    IMG-20241113-WA0005.jpg
    128.1 KB · Views: 2
hao watekaji wanaonekana kabisa. ndio maana marekani trump alisema kila mtu amiliki silaha, ila kama zinapigwa muwe kwenye level sawa.

Hao wanaringa kwa sababu wana silaha, ila wangejua jamaa naye ana silaha wasingemuonea hivyo. nchi imefika pabaya sana.
Mbona kama picha mbili hazina watu wanaofanana?
 
Kakifate kwa Zakaria si yupo au aliondoka nacho jamaa kutibiwa south Africa. Na alipopiga nduru mkakimbilia sheli kwake huku mkisema sisi ni maafisa wa usalama wa serikali na mzee Zakaria akaanza kutuliza wakurya pale msitembezewe panga. Mkawa mnatamani msaada uje chapu. Na kukosa Zakaria mwenyewe kutuliza watu mlikuwa mnachezea panga vizuri sana mura
kwahiyo umeamua kusimulia wadau watakuelewa kweli gentleman 🐒
 
Siku nikikuta mtu anakamatwa kwa nguvu, kama kuna gari nitahakikisha nawaponda mawe ya kutosha na vioo nashusha vyote, hiyo siku nitakufa mimi au mtekaji au wote kwa pamoja.

Na wakifanikiwa kukimbia nikawafahamu, familia zao zitateseka sana.

Si tunaishi nao mitaani?

Nitakua nimekufa kishujaa. Nimejiskia vibaya sana.
 
Tofautisha, chama, serikali na wahuni?.
P
Unaanza na wahuni, unakuja na chama na baadae chama chaunda serikali...

Magenge yaliyoko mexico na nchi nyingine yalianza hivihivi na wahuni. Logically huwezi niambia kuna wahuni polisi au serikali isiowajua, sawa itawezekana swali litakuja je usalama kazi yao nini hizi vuguvugu za wahuni hawazijui na hawapati fununu zozote..

Ni rahisi kumdanganya mzee kwa trick zakitoto, huku mzee kwa busara na hekima zake kukubali kudanganyika, lakini anakuona huna akili kwakuwa yote alikwisha piti enzi za ujanani.
 
Siku nikikuta mtu anakamatwa kwa nguvu, kama kuna gari nitahakikisha nawaponda mawe ya kutosha na vioo nashusha vyote, hiyo siku nitakufa mimi au mtekaji au wote kwa pamoja.

Na wakifanikiwa kukimbia nikawafahamu, familia zao zitateseka sana.

Si tunaishi nao mitaani?

Nitakua nimekufa kishujaa. Nimejiskia vibaya sana.
Haka ka video kamenifanya nitamani kuwa na ka pistol kangu kwa ajili ya usalama wangu binafsi
 
Back
Top Bottom