Dar: Kuanzia Novemba 30 Mbezi Luis Terminal itaanza kutumika rasmi

Hivi haiwezekani kila sehemu kukawa na stendi ya mabasi ya kwenda mikoani maana kila saaa ni kuhamisha tu [emoji2303][emoji2303][emoji2303]
Sijui hawa wanaosimamia nchi wanatumia masaburi gani kufikiria. Mambo ya kuhamisha stand kila siku ni uzwazwa.

~Temeke kuwe na stand ya gari za kusini, iwe ya kisasa na kimataifa kabisa.

~Mbezi Louis kuwe na stand ya kisasa na kimataifa kabisa kwa gari za kanda ya ziwa, Morogoro na huko Iringa-Mbeya.

~Tegeta kuwe na stand nzuri ya kisasa kabisa kwa ajili ya gari za kaskazini huko.

~Reli ya kisasa toka jijini isambae nyanda zote dadeq.

~Trams za ndani ya jiji, za ukweli....

...aaah nimejiwazia tu Mama Sabrina!
 
🙆🏽‍♂️🙆🏽‍♂️🙆🏽‍♂️🙆🏽‍♂️🙆🏽‍♂️ Unajitafutia ban naona
 
Hakuna gharama itakayoongezeka.

Route mpya zitaanzishwa. Kama ulikuwa unapanda mbagala - ubungo. Kutakuwa na gari za mbagala - mbezi zinapita maramba mawili.

Tena naona mbezi ni karibu zaidi kuliko ubungo. Kwa watu wanaotokea maeneo ya airport, mbagala, temeke, chanika n.k.
 
Hata stand ihamishiwe kibaha, foleni haikosekan.
 
Huko malamba mawili n mbali afu mabonde tyuuuh, barabara mbovu lol
Mkuu kwa Dar hakuna mbali nakumbuka Ahmed Jongo akitangaza mpira RTD alikuwa akitamka wale wa Gongolambota wanaanza kuondoka akimaanisha ni mbali lakini leo kumejaa na watu wamefika Chanika mwano mgumu. Ngoja tuwaache mlioozea milimba na mabonde ya kutengeza. Nasikia siku hizi mnapanda mlima wa Ubungo flyover
 
Kweni hilo daraja la juu kama unatoka mikoani limeisha jengwa?. Kama bado hicho kizaazaa kitakacho kuwepo hapo wakati mabasi hayo yakijaribu kukata kushoto yakitokea mikoani kitakuwa siyo cha mchezo.
Haraka hii ya kufungua kituo ambacho bado mambo mengi tu hayajakamilika itakuwa na gharama yake. Yetu macho tu.
 
Mlionicheka kuwa naishi nje ya mji sasa niwaone mkija kulala kusubiria safari ya Mwanza
 
Duuuuh hatareeeeeh sanaah
 
Uwiiiiiiiih afu hapana bhanaah lol
 
Songea pia stand iko mbali saba, yaan 20 km toka town center.
 
ingefanyika hivi
magari ya kwenda moro dodoma mbeya mwanza kigoma yawe mbezi

tanga arusha na mikoa ya kaskazini yajengewe stand bunju

mikoa ya lindi mtwara ijengwe mbagala au chamazi


maduka ya bidhaa za nguo bunju

bidhaa za samaki na vyakula mabibo na ferry

vifaa vya electronics mbezi

vyombo vya nyumbani na ujenzi kariakoo

mashine mbagala
 
True mkuu, Watu wa temeke, gomz, segerea, tabata, makumbusho, kawe gari moja. bunju, mbweni, chanika, mbagala et gari mbili, sidhani kama Kuna sehemu itahitaji zaidi ya gari mbili ili ufike mbezi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…