Dar: Kuanzia Novemba 30 Mbezi Luis Terminal itaanza kutumika rasmi

Dar: Kuanzia Novemba 30 Mbezi Luis Terminal itaanza kutumika rasmi

Baadae sijui itahamishiwa Kiluvya sijui, au itapelekwa Kibaha kabisa. Matokeo ya poor planning haya, toka Mnazi Mmoja, Kisutu, Ubungo na sasa Mbezi Louis. Kwa nini tusiwaze 100yrs?

Japo naamini hii itaishi kidogo coz of massive road reserve na nafikiri njia ya kuingia/kutoka itakuwa rafiki kwa mwingiliano wa Morogoro road, again inlets na outlet ya Mbezi iwe designed vizuri kupunguza msongamano.

Kwa sisi mgeni akiingia jijini namwambia ukishuka stand vuta bodaboda buku uje home, nice!!!
 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam anawatangazia wananchi wote kuwa kutakuwa na mabadiliko ya kituo cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani.

Kuanzia Novemba 30, 2020 mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani yataanza kutumia kituo cha Mbezi Luis na sio Ubungo kama ilivyo sasa.

Aidha wadau wote wanakaribisha kutuma maombi ili kupata maeneo mbalimbali ya biashara katika kituo hicho.

View attachment 1621185
Watakuwa wameshamaliza ujenzi?
 
Kuna sehemu hapa Dar kufika ubungo tu ilikuwa changamoto,je hapo mbezi unadhani itakuwaje.
Mf.mbagala,g/mboto n.k
Kwa sasa ni rahisi mno hiyo route unayosema, ni lami tupu kupitia Kinyerezi unatokea Ukonga na hakuna foleni popote
 
Daaah...aisee. Ndiyo maana ulikua unaona manyota nyota tu hapa na kila ukijaribu kupiga Picha Stand ya mkoa inakaaje Kisutu na Mnazi mmoja haikuingii akilini😀😀😀.
Tanzania imetoka mbali, miaka yetu bango la karibu Dar es Salaam likikua pale Fire.
Baadaye likasigezwa mbele ya Mbezi huku Mizani na geti la Maliasili vikiwa pale Ubongo fyry over/mataa
🤣🤣🤣 Et bango la karibu Dar Es Salaam lilikuwa Fire
 
Kwa sasa ni rahisi mno hiyo route unayosema, ni lami tupu kupitia Kinyerezi unatokea Ukonga na hakuna foleni popote
Baada ya stand kuanza magari yatakuwa mengi kutakuwa na msongamano mkubwa. Hiyo barabara ni nyembamba sana, hata sasa muda wa jioni na asubuhi msongamano upo.
Inapaswa njia ya Pugu Station ijengwe kwa lami. Mabasi ya kutoka Goms, Pugu na Chanika yapite njia ya Station.
Majumba sita yapite ya kutoka Temeke, Mbagala.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mtu anaekaa Mbagala na ana safari ya kwenda Morogoro, itamgharimu pesa nyngi zaidi kutoka Mbagala kwenda stand kuu endapo atatumia bodaboda ili awahi kuliko hata kutoka Dar kwenda Moro.
Kwanini atumie bodaboda wakati daladala za Mbagala zipo 24 hours?
 
Hivi haiwezekani kila sehemu kukawa na stendi ya mabasi ya kwenda mikoani maana kila saaa ni kuhamisha tu [emoji2303][emoji2303][emoji2303]
 
Stand iko mbali Sana lol, ila tutazoea taratibu tyuuuh
 
Zitajengwa nyumba za kulala wageni ili wale wa mbali wapate pa kulala kabla ya safari
 
Stand iko mbali Sana lol, ila tutazoea taratibu tyuuuh
In five or more years hapo ndio patakuwa Centre ya Dar kwasababu kuanzia Mlandizi hadi hapo kati patakuwa pamejengeka vya kutosha, ni mtazamo wangu inaweza isiwe sahihi sana kwasababu kwa mfano chukulia waliofanya feasibility study ya karakana ya BRT iwekwe Jangwani si ni engineers (Yawezekana honored ones) lakin angalia kinachotokea leo mvua ikipiga.
 
Imagine unatoka mbagala kwenda mbez dhaaa
Hii nchi sijawahi kujua hawa maafisa mipango miji huwa wana kazi gani. Miaka ya 1980s kituo cha ma Bus ya mikoani kilikuwa Kisutu na kingine Mnazi mmoja. Ubungo Bus terminal ilikuwa ni yard kubwa tuu ya UDA enzi za Icarus. Enzi za Mwaibula na Keenja ndiyo Walahamishia kituo kwenda pale terminal, na pia UDA walishaiua kiaina. Sasa eti badala ya kuwa na plan ya kutanua pale Ubungo Terminal enzi pana nafasi ya kutosha ili wajenge kituo cha kudumu, cha ghorofa ili kutoa nafasi ya kutosha kwa ma Bus, wao wakalala usingizi. Sasa Wanawapeleka watu hukooo mbali... Hii pia nimeikuta Iringa, kituo kipo about 20km or so from town center.....
 
Nakumbuka wakati Stand inahamishwa kutoka Mnazi Mmoja na Kisutu kwenda Ubungo watu walilalamika na kulia sana, ilikua bado kidogo waandamane.
Wakapiga sana simu redio Tumaini kulalamikia hatua hiyo wakidai Ubungo ni Mbali sana[emoji2][emoji2][emoji28].
Sasa hivi Jiji limefunguka sana, kikubwa ni kuwepo kwa utaratibu mzuri wa usafiri kutoka pande hizo hadi Mbezi.
Huko tuendako Stand itahamishiea Moro na Dodoma na bado watu watawahi na kusafiri kama kawaida.
Si kweli, kwa jiografia ya Dsm watu wanaokaa jirani na Kisutu wengi wao ni wahindi, Waswahili wengi wako kuanzia Magomeni kushuka nyuma kwenda pande zote. Infact wengi walifurahia sana huo uamuzi wa akina Keenja Akiwa jiji na yule Mwaibula (sijui wako wapi hawa jamaa maana wana mchango mkubwa sana kwa jinsi walivyojitahidi kulipanga jiji enzi zao)
 
Hii nchi sijawahi kujua hawa maafisa mipango miji huwa wana kazi gani. Miaka ya 1980s kituo cha ma Bus ya mikoani kilikuwa Kisutu na kingine Mnazi mmoja. Ubungo Bus terminal ilikuwa ni yard kubwa tuu ya UDA enzi za Icarus. Enzi za Mwaibula na Keenja ndiyo Walahamishia kituo kwenda pale terminal, na pia UDA walishaiua kiaina. Sasa eti badala ya kuwa na plan ya kutanua pale Ubungo Terminal enzi pana nafasi ya kutosha ili wajenge kituo cha kudumu, cha ghorofa ili kutoa nafasi ya kutosha kwa ma Bus, wao wakalala usingizi. Sasa Wanawapeleka watu hukooo mbali... Hii pia nimeikuta Iringa, kituo kipo about 20km or so from town center.....
Changamoto hii!
 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam anawatangazia wananchi wote kuwa kutakuwa na mabadiliko ya kituo cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani.

Kuanzia Novemba 30, 2020 mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani yataanza kutumia kituo cha Mbezi Luis na sio Ubungo kama ilivyo sasa.

Aidha wadau wote wanakaribisha kutuma maombi ili kupata maeneo mbalimbali ya biashara katika kituo hicho.

View attachment 1621185
Daaa!!! Sasa sisi watu wa Mbagala tutakoma!
 
Back
Top Bottom