Dar Kuna fursa nyingi za biashara na kupiga pesa, ni kuamua na kutokuwa na aibu tu

Mwaka juzi alikua ndugu yangu mmoja Dar akahangaika wee maisha yakawa magumu ikabidi aje kwangu kuomba hifadhi na kumsaidia kupata kazi
Mwamba ni darasa la 4 tu

Nikakumbuka kuna jamaa aliwahi kuniambia kama ukiwa unakwenda Vingunguti machinjioni unakwenda kununua nyama kisha ukatafuta kijiwe kilicho changamka na ukaweka jiko lako pale kuanzia jioni ukawa unauza nyama za kuchoma utapiga hela kimasihara

Basi nikampa humo mchongo dogo akakubali, tukatafuta jiko kwa 120,000 na wavu kisha machinjioni unakwenda kununua nyama mchanganyiko, kule haununui kwa kilo, utakuta wale wachunaji na wachinjaji wananyama zao wamepiga bao kwa kukata kidogo kidogo kisha wanakusanya na mnakubaliana bei tu kulingana na wingi na aina ya nyama

Mwanzo ilikua changamoto lakini alipokujuja kujua namna ya kuoatana bei na namna ya kukata nyama alianza kupiga hela hatari
Yaani ukichukua gharama kuanzia nauli ya kuamka saa 10 kwenda na kurudi machinjioni, ikachukua ná gharama za ununuzi wa nyama, viungo vya pilipili ya maji, chunvi, mkaa nk kwa siku faida ilikua inachez 20,000 hadi 50,000 kwa nyama za vipande vya buku2, buku, na jero jero utumbo

Baada ya miezi 6 tu dogo akatafuta chumba na hivi sasa ana mke na watoto kwa biashara hiyo na yuko vizuri kabisa anendesha maisha yake
 
Sawa Dogo Muuza NyamA.
 
Sio kweli Dar maisha ni cheap sana

Ugali wa buk unashiba kabisa
Nauli ya 10000 unaenda Morogoro au
Kwa bachela Dar maisha ni rahisi mmno
Dar hapa kuna ugali hadi mia 500, mboga dagaa tembele na mchuzi wa utumbo 😂

Pilau la buku au wali harage la buku na maji ya 50 unashiba na usingizi hapa hapo 😂

Dar ukitaka kuiona ngumu basi ishi kwenye level sio zako za kujifanya unachagua hotel na sehemu za hadhi kwenda kula

Hapa posta wali nyama ipo kuanzia buku jero hadi sahani 5000
Ni wewe tu
 
Dar pesa ipo
Ni ubunifu tu kukomaa
Unaweza ona mtu unadharau kazi yake kumbe pesa anayopata ni Siri yake
 
Nadhani hajazingatia kwanza competition ilioko kwenye hizo biashara ambazo kila mtu anaweza fanya sababu mtaji ni mdogo.

Kisha jua lilivyo kali mjini hapa 🤣inahitaji moyo sana kuanza hizo mishe.
Hakuna biashara hapo inakosa wateja
Utatoa mzigo wote uuze na hakika utamaliza
 
Mkuu si rahisi as you think mkuu! Najuta nilipoteza 5 milioni kwa hizo biashara za kuambiwa pumbavu zako
 
Lakini siku hizi kila mtu anajua kusajili line ni bure, line za siku hizi sio kama za zamani zinakuja zimeshakatwa, siku hizi watu wengi hawanunui vocha bali wananunua vifurushi kupitia mobile money.
Huyu kwao Ngara anajua Dar napo kuna mabwege wakupigwa kusajili laini kwa kulipia. Alafu anadai ukishasajili unakata laini unamlipisha mteja, mara ya mwisho kuona laini haijakatwa ni 2019.

Sanasana Dar mtu atanunua vocha ya buku baada ya kusajili.
 
Huyu kwao Ngara anajua Dar napo kuna mabwege wakupigwa kusajili laini kwa kulipia. Alafu anadai ukishasajili unakata laini unamlipisha mteja, mara ya mwisho kuona laini haijakatwa ni 2019.

Sanasana Dar mtu atanunua vocha ya buku baada ya kusajili.
Laiti mngejua kazi ya kusajili laini inavyolipa wote mngekuwa freelancer
 
Laiti mngejua kazi ya kusajili laini inavyolipa wote mngekuwa freelancer
Hawa madogo wenyewe wanajua ubishi tu
Me nawapa uzoefu wanasema kwetu Ngara, haya me mhangaza sijui mambo ya mjini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…