Kama umeamua kuipumzisha gari izime kabisa. Usiweke silence. Gari ukiiweka silence (idle) hujaipumzisha bado, engine bado inaendelea kuwa moto na tena kama umepiga nayo safari ndio kabisa inaendelea kuwa moto haipoi. Kumbuka, unapokuwa njiani, sio maji tu ndio yanapoza mashine, ule upepo unaopiga kwenye radiator na engine kwa ujumla unasaidia sana tena sana kupoza mashine ndio maana ukikaa silence mda mrefu unaona feni zinazunguka. ila kama upo kwenye mwendo, hutozisikia zikizunguka kwa sababu tayari upepo wa kutosha upo