Dar: Mchina adaiwa kumuua mwenzake na kumjeruhi mwingine kwa risasi, chanzo ugomvi wa mapenzi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamtafuta mtuhumiwa ZHENG s/o LINGYAO, 42, raia wa China Mkazi wa Dar es Salaam kwa tuhuma za kumuua FU s/o NANNAN, 26, Raia wa China, mfanyabiashara na mkazi wa Kalenga Ilala Dar es salaam.

Tukio hilo limetokea tarehe 11/06/2022, Mtaa wa Kalenga Ilala kwenye ghorofa ya tatu ya wapangaji majira ya saa tano na dakika arobaini na tano usiku, ambapo mtuhumiwa anayetafutwa alifika eneo hilo na kumjeruhi kwa risasi tumboni NIE d/o MNQIN, 32, raia wa China na baadaye alimfyatulia risasi FU s/o NANNAN Raia wa China ambaye alipoteza maisha.

NIE d/o MNQIN anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Taifa Muhimbili.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne amesema uchunguzi wa awali wa tukio hili umebaini kuwepo kwa tatizo la kutoelewana lililotokana na masuala ya kimapenzi.
 
Utakuta yalikuwa yanamgombania demu wakibongo aliyejaziajazia kwasababu yakwao ni fleti aliyekuwa akiwagawia beki. Huu ugonjwa wa mrangi utawaua wengi.
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamtafuta mtuhumiwa ZHENG s/o LINGYAO, 42, raia wa China Mkazi wa Dar es Salaam kwa tuhuma za kumuua FU s/o NANNAN, 26, Raia wa China, mfanyabiashara na mkazi wa Kalenga Ilala Dar es salaam.

Tukio hilo limetokea tarehe 11/06/2022, Mtaa wa Kalenga Ilala kwenye ghorofa ya tatu ya wapangaji majira ya saa tano na dakika arobaini na tano usiku, ambapo mtuhumiwa anayetafutwa alifika eneo hilo na kumjeruhi kwa risasi tumboni NIE d/o MNQIN, 32, raia wa China na baadaye alimfyatulia risasi FU s/o NANNAN Raia wa China ambaye alipoteza maisha.

NIE d/o MNQIN anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Taifa Muhimbili.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne amesema uchunguzi wa awali wa tukio hili umebaini kuwepo kwa tatizo la kutoelewana lililotokana na masuala ya kimapenzi.
ASHURA kafanya Mambo yake

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Kuuwa kwa sababu ya mapenzi ni ujinga na ushamba uliokubuhu. Hata kama ni mke wangu, ninamfungisha ndoa na huyo mchepuko ila kisheria nirudishiwe pesa zangu (mahari)
 
Screenshot_20220612-173808_Edge.jpg
 
Back
Top Bottom