Offshore Seamen
JF-Expert Member
- Mar 9, 2018
- 5,489
- 14,091
Bandari Ina changamoto sana kiutendaji kuanzia storage facility, handling equipment, parking na system.Kabisa mkuu nimeingiza Trucks tokea ijumaa kupakia Plant tokea jumatatu nikuzungushana tu machine mbovu wanakosa hata betri za ku boost machne kweli? aibu sana mtu akiwa nnje hawezi kuamini tukisemacho.
Halafu wanakwambia Bagamoyo ni mradi wa kishenzi, Kuna watu tutakufa tutaacha nchi bila kuwa na bandari kama ya Durban au hata Lamu ya 254Bandari Ina changamoto sana kiutendaji kuanzia storage facility, handling equipment, parking na system.
Humu Kuna raia Wana thubutu kulinganisha Dar Port na Durban Port
Kwa umbumbumbu wako unadhani ukubwa unaanzia mita ngapi na unaishia mita ngapi?Kwahiyo kwa akili zako unadhani meli ya mita 200 ndio kubwa sana?
Mombasa Port wametuacha parefu kwenye port productivity, sisi Bado tunafurahia size na ukubwa wa meli wenzetu wanapambana kila mwezi kuvunja rekodi za meli kukaa muda mfupi ikiwa imehudumiwa na bandari yao.Kwahiyo kuja kwa hiyo meli ndo inaonesha Bandari ya Dar ina uwezo wa kushindana na Bandari ya Mombasa, au?!!
Au kwavile umeambiwa bandari imepokea "bonge la mmeli" ndo maana umefikia kusema hayo!!!
FYI, ile meli wamesema ina urefu wa almost 200M, wakati Megaships zinafikia hadi 400M; and it's matter of time kabla hazijitengenezwa zenye urefu wa hata 500M!!
Meli kama hizo nilizotaja hapo juu haziwezi kuingia Dar Port!!
Na kama unadhani kuingia meli yenye urefu wa 200M ndo inaonesha mbavu zetu dhidi ya Mombasa, hebu soma hapa chini:-
Hiyo ndo meli ambayo ilifunga gati Mombasa way back in 2018!!
Na hapa chini, ni idadi ya meli zilizofunga gati, na zinazotarajiwa kuingia kwenye bandari hizo mbili kama inavyoripitiwa na Marine Traffic---
Sasa endeleeni kuleta mizaa kwenye mambo serious, lakini nikukumbushe tu kwamba, Firs Phase ya Lamu Port imeshakamilika!!
Hata hizo unazoziita kubwa kwa sasa inawezekana baada ya miaka ishirini zikatengenezwa kubwa zaidi ya hizo.Kwahiyo kuja kwa hiyo meli ndo inaonesha Bandari ya Dar ina uwezo wa kushindana na Bandari ya Mombasa, au?!!
Au kwavile umeambiwa bandari imepokea "bonge la mmeli" ndo maana umefikia kusema hayo!!!
FYI, ile meli wamesema ina urefu wa almost 200M, wakati Megaships zinafikia hadi 400M; and it's matter of time kabla hazijitengenezwa zenye urefu wa hata 500M!!
Meli kama hizo nilizotaja hapo juu haziwezi kuingia Dar Port!!
Na kama unadhani kuingia meli yenye urefu wa 200M ndo inaonesha mbavu zetu dhidi ya Mombasa, hebu soma hapa chini:-
Hiyo ndo meli ambayo ilifunga gati Mombasa way back in 2018!!
Na hapa chini, ni idadi ya meli zilizofunga gati, na zinazotarajiwa kuingia kwenye bandari hizo mbili kama inavyoripitiwa na Marine Traffic---
Sasa endeleeni kuleta mizaa kwenye mambo serious, lakini nikukumbushe tu kwamba, Firs Phase ya Lamu Port imeshakamilika!!
Siamin.! Magar 2000 sio mchezo.!View attachment 1887764
View attachment 1887765
Bandari ya Dar es Salaam imeendelea kuzivutia kampuni kubwa za usafirishaji duniani, baada ya meli kubwa ya kisasa ikiwa na shehena kubwa zaidi ya magari kuwahi kutia nanga bandarini hapo.
Meli hiyo ya TRANQUAIL ACE (IMO: 9561253) inayomilikiwa na Kampuni ya Mitsui ikitokea moja kwa moja nchini Japan, imetia nanga ikiwa na magari 3,743 ambayo ni mengi zaidi kuwahi kusafirishwa kuja nchini kwa mara moja.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Eric Hamissi amesema kuwa meli hiyo imeandika historia mpya kutokana na kubeba shehena kubwa ya magari.
Meli hiyo iliyotengenezwa mwaka 2009 ina urefu wa mita 199.9 na upana mita 32.2 kwenda chini, ambapo imetia nanga chini ya nahodha, Diardado Garate.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 10, 2021 katika Bandari ya Dar es Salaam, Hamissi amesema kuwa meli hiyo imetia nanga Agosti 9, 2021 na kuanza shughuli ya ushushaji ambao unatarajiwa kumalizika kesho jioni.
Meli kubwa kuwahi kutia nanga nchini na ailiyokuwa imebeba shehena kubwa ya magari ilitia nanga bandarini hapo mwaka 2018 ikiwa na magari 2600.
"Leo ni siku nzuri sana katika historia ya TPA kwa kuweka rekodi mpya kwa kupokea meli kubwa na iliyobeba shehena kubwa zaidi kuja nchini. Hii haijawahi kutokea katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na kubwa zaidi meli hii imetoka moja kwa moja Japan kuja nchini bila kupitia bandari nyingine.
View attachment 1887766
"Kwa hiyo ni jambo jema dunia inakafahamu kwamba, Tanzania tuna bandari bora na ya kisasa yenye uwezo wa kupokea meli zote na ikazihudumia kwa wakati,” amesema Hamissi na kuongeza: “Katika inayoendelea kushushwa, magari yatasafirishwa kwa njia ya barabara kwenda nchi jirani na mengine 798 yanabaki hapa nchini.
"Mtaona ni jinsi gani sasa nchi zetu za jirani zinazotuzunguuka zimeenza kutuamini, kati ya magari yaliyoingia asilimia 65 yanakwenda kwenye nchi hizo."
Meneja Kampuni ya Inchcape Shipping Services, John Massawe amesema meli hiyo ina uwezo wa kubeba magari 5,200 na kwamba imetumia siku 20 ikiwa safari hadi kuwasili.
"Tumekuwa tukihudumia kampuni ya magari kwa miaka zaidi ya 20, na hii ni meli ya kwanza hivyo tunatarajia huu ni mwanzo wa kuleta meli nyingine kubwa zaidi," amesema Massawe.
Thanks, na hilo nimelisema jana kwamba hizi mega-ships zinaweza kuchukua mzigo mkuuubwa, labda kutoka Far East kwenda Pwani ya Bahari ya Hindi ya Afrika, kisha ikaenda kufunga gati kwenye nearest port yenye uwezo wa kupokea meli kama hizo, na hizi meli za kawaida zikaenda kuchukulia mzigo hapo na kusafirisha hadi kwenye hivi vibandari vyetu!Hata hizo unazoziita kubwa kwa sasa inawezekana baada ya miaka ishirini zikatengenezwa kubwa zaidi ya hizo.
Hizo meli zinzzoitwa kubwa hazibebi mzigo mmoja mkubwq bali mizigo midogo midogo mingi hivyo sio kwamba ili bandari fulani ifanye kazi basi lazima iwe na uwezo wa kupokea meli kubwa tu. Pia kuwa na bandari yenye kupokea meli kubwa sio gaarantii kuwa bandari hiyo itafanya kazi to the maximum capacity, ndio maana hiyo meli imetia nanga Dar badala ya Mombasa.
kazi iendelee!!Bandari ya Bagamoyo itaweza kupokea hayo madude hata nane kwa wakati mmoja, mbali na hapo wenzetu Durban, Beira, Lamu ndio watakuwa wenyeji wa hayo ma Megaship East South Africa
kazi iendelee!!Bandari ya Bagamoyo itaweza kupokea hayo madude hata nane kwa wakati mmoja, mbali na hapo wenzetu Durban, Beira, Lamu ndio watakuwa wenyeji wa hayo ma Megaship East South Africa
Unajua Wabongo tunapenda sana kujipa matumaini!! Yaani leo meli yenye urefu wa 200m, kutia nanga Dar Port ndo tayari tumeshaona a milestone! Na kama ulivyosema, ni kweli nimesoma jinsi KPA hivi sasa wanavyokazania suala la efficiency manake wenzetu wanajua suala la time inayotumika kutoa mzigo bandarini ni factor kubwa sana ya kupima efficiency ya bandari!!Mombasa Port wametuacha parefu kwenye port productivity, sisi Bado tunafurahia size na ukubwa wa meli wenzetu wanapambana kila mwezi kuvunja rekodi za meli kukaa muda mfupi ikiwa imehudumiwa na bandari yao.
Hata ukitembelea Kenya Port Authority website yao utaona wakifanikiwa kuhudumia meli kwa muda mfupi wanaweka rekodi zake.
Hili kwa kweli, wala halina mjadala, haidhuru hata kama tutaenda kule Kenyan Forum na kuwaambia "Hiyo SafariCom yenyewe ni ya Wazungu 🤣 🤣 🤣 ili mradi tu!!Ukweli mchungu, jamaa wametuacha inabidi tupambane.
Za bandari ni mali ya chama hazihusiki na ujenzi wa nchi, za ujenzi wa barabara na mambo menginemengine bajeti yake ipo kwenye tozo za miamala!!Hapo kila gari kodi sio chini ya 5m zidisha mara 1000 tu uone ni bara bara ngapi zitajengwa na huo ushuru wa bandari
Mkuu Bongo yetu kuna uongo mwingi tu.Wapo waliowahi kusema kuwa hatuwezi kuongozwa na mwanamke,lkn leo Mama ameishikilia usukani.Mnaosema bandari ya Dar haiwezi himili meli kubwa uongo wenu umeanza kuonekana
Hakuna lisilowezekana chini ya juaSiku moja nitaenda kutalii bandarini, nione hizo meli zinavyofanana, kwa kweli sikuwahi kufikiri kama meli inaweza kubeba magari mengi kiasi hicho
Itabidi maza ashughulike hiyo kero kwa kuwawajibisha wahusika.Ujinga tu tunajisifia kupokea meli kubwa lakini huduma bandarini mbovu kabisa, hao vijana wanaoshusha hayo magari utazania vichaa wanaendesha hovyo wanakwangua magari ya watu na hawaadhibiwi kabisa, kwakweli utendaji wa bandari yetu unashangaza sana, unakaa siku 3 unahitaji GOT WARD yakupalia Machine ya mteja siku 2 kila siku mbovu mara betri mara system basi ilimradi ucheweleshwaji tu na hakuna msamaha wa Storeg walio isababisha wao.
C.r.a.p....Kwa umbumbumbu wako unadhani ukubwa unaanzia mita ngapi na unaishia mita ngapi?
Mkuu sisi time na efficiency hatujaweka kipaumbele.Unajua Wabongo tunapenda sana kujipa matumaini!! Yaani leo meli yenye urefu wa 200m, kutia nanga Dar Port ndo tayari tumeshaona a milestone! Na kama ulivyosema, ni kweli nimesoma jinsi KPA hivi sasa wanavyokazania suala la efficiency manake wenzetu wanajua suala la time inayotumika kutoa mzigo bandarini ni factor kubwa sana ya kupima efficiency ya bandari!!
Mkuu kulinganisha Dar Port na Durban Port ni mbingu na nchi. Wenzetu wapo mbali sana kuanzia terminal facilities, railway network na idadi ya berth. Ili tuanze kulinganisha na Durban labda uwekezaji mkubwa ufanyike Bagamoyo si kwa Dar Port.