Dar: Meli yenye magari 3,743 yawasili bandarini ikitokea Japan

Dar: Meli yenye magari 3,743 yawasili bandarini ikitokea Japan

Magu huyu huyu ambae maelezo yake ni kama alikuwa anashindwa hata kutofautisha kati ya Contract na Framework Agreement ambayo hata hivyo ilisha-expire?!
Naam ni jambo la afya kuwa na fikra huru za kufikiria juu ya jambo, kitu, ama mtu kadri Mungu anavyokuwezesha.

Hata hivyo, kwa kuanza kumkosoa Hayati Dr John Pombe Joseph Magufuli, aliyekuwa rais wa nchi yetu Tanzania, tena kwa kebehi huku ukijua kabisa hawezi kuja hapa kufafanua utofauti wa contracts na framework agreement, inatoa taswira ya ama kwa makusudi unataka kubadili mjadala ama kuna ukweli kuna nguvu za 'ziada' zinakuweka kwenye utetezi wa mradi (sentensi ndefu, nivumilie).

Binafsi, sikutilii shaka lakini unatengeza mazingira ya kunikatisha tamaa mimi mwanafunzi wako kindakidanki nisiendelee na somo.🙂🙂🙂
 
Ni haki yako kama binadamu kuwa na maamuzi hay. Nashukuru na kufurahi kwa kuwa ulifanya utafiti na kukusanya taarifa ( Nikiwa na imani kulifuata Taratibu zote zinazoelezwa na sheria ya nchi ya Takwimu). Kwa hiyo tupe taarifa rasmi juu ya ukweli kuhusu mradi wa Bagomoyo. Taarifa yako itasaidia sana kumaliza mjadala huu ili tuendelee kujadili mambo mengine muhimu kwa ajili ya taifa letu.

Karibu.
Kiongozi Mkuu anaweza kuwa misinformed kwenye suala la Bandari kama alivyokuwa misinformed kwenye suala la Covid-19.

Sina utaalamu sana kwenye masusla ya kodi lakini niliangalia faida za ziada na kodi vyanzo vya mapato vitavyotengenezwa na mradi.

Tukumbuke fedha ya mradi huu sio mkopo, bali nu fedha karibia trillions 23 mtu anakuja kuwekeza hivyo anahitaji muda kurudisha fedha yake na faida juu.

Pia suala la kijiografia, tumezungukwa na nchi 8 ambazo 6 hazina bandari zimekuwa zikitegemea bandari yetu ya Dsm. Ambayo pia imekuwa ikipata ushindani wa kibiashara kutoka kwenye bandari za Lamu, Beira na Durban kutokana na ufanisi wa hizo bandari.

Pia bandari yetu kuu bado ni ndogo kwa Dunia ya sasa na technology ilivyokuwa ndio maana tumeshangaa meli kubeba gari 3700 wakati kuna bandari zinauwezo wa kupokea meli za kubeba gari 8000 kwa wakati mmoja. Tulipokea meli ya kontena 5000 na yenyewe ikawekwa kwenye font fod wakati huko Duniani Kuna meli zinabeba kontena 20000.

Pia hatukujenga SGR kwa ajili ya kutumia Kama tunavyotumia MGR. Uwezo wa SGR ni kubeba mzigo mkubwa na kwa haraka zaidi. Tunaboresha reli kwa matrilion lakini Mlango (Bandari) wa kupokea na kutolea Mzigo bado na mwembamba moja moja utaweza ona faida ya SGR ni bora tubaki na MGR kulilo kuteketeza Kodi za watanzania hapo kwe SGR.

Pia mradi ulikuwa unakuja na viwanda karibia 190 kwenye eneo la Bagamoyo na Pwani, sijajua vingetoa ajira kiasi gani na mapato kiasi gani kwa serikali ya mkoa na serikali kuu.

 
MWAKA 2018 MELI KUBWA ZAIDI KWA HAPA TZ ILITIA NANGA BANDARI YA MTWARA IKIWA IMEBEBA MALORI 600 YA DANGOTE. MELI HIYO ILIKUWA NA UREFU WA 210 M. Hivyo sishangai sana.
 
Hivi Kimantiki tunatakiwa tusifie Ufanisi na Mapato ya Bandari zetu au tusifie tu Ukubwa wa Bandari zetu kwa kupokea Meli Kubwa kama Viwanja vya Mpira?
Corona ipo Moshi na Arusha kwa sababu ya laana ya kushangilia kifo cha Magufuli
 
Ushuru upandushwe haraka.kwa ahadi ya barabara ya changakawe sijui tutaendeshaje magari.
 
Watetezi wa bandari ya Bagamoyo waone aibu. Maana tulikuwa tunaambiwa kuwa bandari ya Dar haiwezi kushindana na bandari ya Mombasa hivyo tukitaka kushindana basi tujenge bandari ya Bagamoyo; leo wamesutwa.

Narudia hakuna haja ya bandari ya Bagamoyo.
 
Bandari ya Dar ishaingiza meli ya urefu wa zaidi ya 250M. Hii ya kusema kwamba hii ya 200m ndo kubwa zaidi kuwahi kuingia bandari ya Dar sijui wameitoa wapi.
 
Watetezi wa bandari ya Bagamoyo waone aibu. Maana tulikuwa tunaambiwa kuwa bandari ya Dar haiwezi kushindana na bandari ya Mombasa hivyo tukitaka kushindana basi tujenge bandari ya Bagamoyo; leo wamesutwa.

Narudia hakuna haja ya bandari ya Bagamoyo.
Kwahiyo kwa akili zako unadhani meli ya mita 200 ndio kubwa sana?
 
Naam ni jambo la afya kuwa na fikra huru za kufikiria juu ya jambo, kitu, ama mtu kadri Mungu anavyokuwezesha.

Hata hivyo, kwa kuanza kumkosoa Hayati Dr John Pombe Joseph Magufuli, aliyekuwa rais wa nchi yetu Tanzania, tena kwa kebehi huku ukijua kabisa hawezi kuja hapa kufafanua utofauti wa contracts na framework agreement, inatoa taswira ya ama kwa makusudi unataka kubadili mjadala ama kuna ukweli kuna nguvu za 'ziada' zinakuweka kwenye utetezi wa mradi (sentensi ndefu, nivumilie).

Binafsi, sikutilii shaka lakini unatengeza mazingira ya kunikatisha tamaa mimi mwanafunzi wako kindakidanki nisiendelee na somo.🙂🙂🙂
Ndugu yangu inakuwa hunitendei haki ukisema kwamba namkebehi Magu...

Btw, kwani wakati yupo hai alishawahi kuja JF kujibu chochote hadi ionekane kusema hivi sasa itakuwa ni kutomtendea haki?!! Halafu hili la Magu unatakiwa kulizoea...

Mwalimu amefariki zaidi ya miaka 20 iliyopita, lakini bado anasemwa, na ataendelea kusemwa!

Karume amefariki takribani miaka 50 iliyopita lakini bado anasemwa na ataendelea kusemwa!!!

Kwahiyo unatakiwa kuzoea na hilo la Magu....

Ndugu yangu TUJITEGEMEE hebu tafakari peke yako....

Ulishawahi kuona au kusikia pande mbili zinasaini mkataba, halafu hapo hapo wanatangaza wanaendelea na majadiliano kwa sababu hawajafikia makubaliano?! Hushawahi kusikia kitu kama hicho?!

Sina shaka wewe ni mfuatiliaji wa mambo yanayoendelea nchini! Je, ipo siku yoyote uliyowahi kusikia kwamba SERIKALI IMEVUNJA MKATABA wa Ujenzi wa Bandari?

Ukitafakari kwa makini, utaona wazi kwamba hapakuwa na mkataba na ndo maana majadiliano yalikuwa yanaendelea!! Sasa kama hapakuwa na mkataba, ni mkataba upi ambao Magu na Serikali yake walikuwa wanatutangazia kwamba ni wa Kinyonyaji, ni upi?!

Sasa hapo uki-doubt credibility ya Magu sio kwamba ni kumkebehi bali ndo uhalisia wenyewe!!! Na ukizingatia kauli zingine kwenye mambo mengine, hapo inatoa nguvu zaidi ya ku-doubt credibility yake!!

Lakini tatizo lingine la Magu, inawezekana ni kama lile ambalo niliwahi kusema kuhusu Kakoko, kwamba Kakoko ni Engineer kwahiyo inawezekana hana uelewa mkubwa kuhusu mambo ya kodi!!

Matokeo yake, akaenda kwenye media na kutangaza "Mchina ametaka asamehewe kodi" bila kutaja ni kodi ipi! Ilikuwa ni muhimu kutaja kwa sababu, sheria zetu zinaruhusu kusamehe baadhi ya kodi ili kuvutia wawekezaji!!

Lakini unapotoka tu mbele na kusema "Mchina anataka asamehewe kodi" ni rahisi sana wananchi kuamini kwamba kumbe zile VAT, Import Tax, Excise Duty n.k zote hizo zinaenda kwa Mchina; jambo ambalo si kweli!!
 
Mbona hii meli imewahi kuja Bandari ya hapo hapo Dar es Salaam kipindi cha nyuma ?

Nini kimebadilika mpaka iwe habari ?

Naomba ufafanuzi tafadhali !

Hizo huwa ni RoRo kama hiyo, zinakuja mara kibao kuleta magari

Huenda hapo kabla ndio hakujawahi kuwa na RoRo yenye ukubwa kama huo kutia nanga hapo bandari ya Dar...
 
Back
Top Bottom