Dar: Mfanyabiashara Mohamed Dewji(Mo Dewji) atekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay

Hii sio taarifa nzuri sana kwa Collosium gym itapoteza watu maarufu wateja, pia kwa wawekezaji, huyu MTU amegusa maisha ya watu wengi sio kitu cha kuchekea , Mh Rais hawezi kulifumbia macho hili hatari kubwa.
Wajiandae kisaikoloji kwenye hili Colloseum.. Huwezi ukaweka mlinzi anaekimbia silaha sehemu wanayoenda wafanyabiasha Na watu wenye hela.
 
Lakini inasemekana watu wamemnukuu vibaya RC. Hajapatikana bado Mo
 
Matukio kama haya tumeyafumbia macho muda mrefu bila kuwakamata wahusika... Tunaishia kuwatumbua mawaziri wakishakamilisha mission zao kama hizi.
Angalia mfano_: Alphonce mawazo,
Ben saanane
Tundu lissu
Roma
Azory... n.k
Sasa umekuwa kama mchezo kwenye maisha ya watu, huu ni ujinga tena mkubwa...
Imefikia wakati sasa kila tukin la namna hii serikali inatajwa kuhusika.. Kama hawatoi maelezo mazuri, hakuna upelelezi, watuhumiwa hawakamatwi kwa nn tusiseme wahusika ni serikali eti wasiojulikana.
Acheni ushamba na uadui wa kijinga.
 
Mmmh! sasa mbwa kaaza kutufuata hadi madhabahuni. Lazima tujiulize kama wengine tunasema wanatekwa kwa sababu za kisiasa Mo katekwa kwa sababu zipi?

Za kibiashara? kwamba amedhulumiana, ameingilia, ameshindana na wenzake visivyo halali? wivu? ndani au nje ya nchi?
Za kimaskini, kwamba maskni wamemteka?
Za kisiasa!!?
Za kimpira?
Au.

Kama tusipozifahamu sababu ni vigumu kutafuta wahalifu wake.
 
Bado hajapatikana
 
Unajua kujiongeza japo inaweza isiwe kweli lakini kwa akili za DAB naweza kubet nikaweka mkwanja mrefu hapa kwamba ni 'kweli'.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…