Kutekwa kwa raia yeyote yule ni ishara mbaya...haijalishi huyo mtu ni maarufu au mtu wa kawaida kama mimi.
Tanzania sio nchi ya kwanza dunia tukio kama hili kutokea...haya mambo yanatokea sana hata ulaya na marekani.
Halafu usipende kuhukumu moja kwa moja kana kwamba unafahamu nani kamteka na ni kwanini.
Muhimu ni kuonesha ushirikiano kwa jeshi la polisi.
ASANTE
Nitajie nchi moja tu, yoyote ile ambayo tajiri wake mkubwa kuliko wote aliwahi kutekwa na saa 24 kupita bila vyombo vya dola kuwa na clue!
Kwamba, eti "haijalishi huyo mtu ni maarufu au kama mimi" hiyo ni kujaribu ku-justify uozo uliopo kwenye mfumo wetu wa ulinzi na usalama! Endelea kujidanganya kwamba akina eti sie tupo sawa tu na akina Reginald Mengi na kwamba, utekwaji wa yeyote miongoni mwetu hiyo ni ishara mbaya! Ni kweli, ni ishara mbaya lakini anapotekwa mtu kama Mo Dewji, hiyo sio tu ni ishara mbata bali ni ishara mbaya zaidi na zaidi!
Sie wengine miaka kadhaa iliyopita tulishuhudia Mzee Reginald Mengi akipewa ulinzi wa polisi nyumbani kwake Oysterbay baada ya kutishiwa kuuawa! Kama unaamini wewe na Mzee Mengi ni sawa, basi nenda kwenye kituo cha karibu ukaripoti kwamba unatishiwa kifo na kisha wathibitishe kwamba kweli unatishiwa kifo halafu uone kama unapewa askari polisi wa kuja kukulinda hapo unapoishi!!!
Mtu kama mimi, nitaenda viwanja gani kama sio Tandale, Mwananyamala, Manzese, Temeke n.k! Huko haitashangaza nikitekwa kwa sababu mfumo wetu wa ulinzi haujafika kisawasawa hadi Uswahilini!!! Lakini inapotokea mtu anatekwa maeneo kama ya Colleseum na kupita 24 hours bila vyombo vya dola kuwa na clue, hapo akina sie hatutaacha kujiuliza ikiwa maeneo kama yale na mtu kama yule anaweza kutekwa na watekaji kutokomea kusikojulikana! Maeneo ambayo angalau yana mifumo mizuri ya mitaa ambayo ingewezesha kuwa na street cams; vipi akina sie tunaoishi Kwa Mtogole! Huku kwetu watu si wanaweza kuingia hadi na vifaru na wasionekane!!
Ikiwa maeneo kama yake hayana hata Patrol inayoweza ku-respond kwa haraka anapotekwa mtu kama Mo Dewji, vipi huku kwetu?Ikiwa Richest Person anaweza kutekwa na polisi wasiwe na clue hata baada ya saa 24 kupita huku tukifahamu wamewekeza nguvu zao zote katika kufanya msako! Vipi ninapotekwa mtu kama mimi ambae polisi haitaweza kutoa japo askari mmoja kutafuta nipo wapi!!!
Kwa wale wanaoamini katika siku ya huku, mimi na Mo Dewji ni sawa lakini ni sawa mbele ya mwenye kiti cha enzi lakini hatuna usawa wowote mbele ya viti vya akina Magu!!
No wonder tunapotekwa akina sie wala hakuna anayejishughulisha! Endelea kuhangaika ku-justify ujinga!