Dar: Mfanyabiashara Mohamed Dewji(Mo Dewji) atekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay

Dar: Mfanyabiashara Mohamed Dewji(Mo Dewji) atekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay

Duh!Watu wasioujulikana hao bila shaka!

Hii nchi sasa!!

Walitekwa na kupotea watu wa kawaida, tukaona ni mambo madogo.Leo wanatekwa matajjri na watu maarufu labda sasa ndio tutashituka.

Nakumbuka pia yaliompata Lissu na mfanyabiashara wa Tarime bwana Zakaria.

Wacha tusubiri tuone nini kinaendelea tutapata picha kamili.

Kwa sasa wanaweza kuwa wanapima upepo.Pressure ikiwa kubwa,wanaweza kumwachia ikiwa mpaka sasa bado yuko salama.

Hii update kuwa katekwa na wazungu,inanipa maswali mengi sana na mojawapo ni wazungu gani hao wa kumteka mtu tajiri kama huyo tena wakiwa katika nchi ya watu?

Wanajiamini nini?
Sasa kama katekwa na wazungu kumbe wanajulikana
 
Keshaanza kujichanganya
Na usikute hapa ni kupotezea ku fail kwa mradi wa Mwendokasi aliojisifia sana Jiwe na wenzake.
Nimeangalia mateso wanayopata wana wa Dar na eti kuna mtu anayewakilisha wana Dasalama ANAUNGA MKONO JUHUDI? kweli hii hali ya Dar mbona nchi nyingine ingesha tishia kuangusha serikali?
Wasiojulikana wanatumika wakati mwingine kupoteza maboya watu, dawa yao ni Zakaria style tuu. Mwaga utumbo na fyekelea mbali!
 
Kuna hizi habari kwamba Mfanyabiashara Mohamed Dewji ametekwa leo asubuhi maeneo ya Collosium Gym , Oysterbay alipokuwa ameenda kufanya mazoezi..

Mwenye habari kamili atujuze.

======

UPDATES:

Mfanyabiashara maarufu nchini, ambaye pia ni mwekezaji wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji (Mo Dewji), anadaiwa kutekwa na watu wasiojulikana waliokuwa na silaha za moto, saa 11 alfajiri wakati akiingia kufanya mazoezi katika gym ya Colosseum, Oysterbay jijini Dar leo Oktoba 11. Kamanda wa Polisi Kinondoni, Jumanne Muliro athibitisha.

RPC Lazaro Mambosasa amesema Polisi Dar inafuatilia madai ya kutekwa kwa mfanyabiashara huyo maarufu nchini

UPDATE 1:

Dereva wa Uber amesema aliona watu 4 wakishuka kwenye gari dogo, wakiwa wamejifunika usoni, wakapiga risasi moja juu na kumchukua Mohammed Dewji

UPDATE 2:

RPC Lazaro Mambosasa amesema waliomteka mfanyabiashara Mohamed Dewji (Mo) ni wazungu wawili. Aidha, amesema msako mkubwa unafanywa kwa raia wa kigeni wote waliopo nchini kufuatia kutekwa kwa Mo Dewji

UPDATE 3:

RPC Lazaro Mambosasa amesema watu watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano kuhusu kutekwa kwa mfanyabiashara Mo Dewji

jamaani watu wabaaya kosa gan asaa/ au kik
 
Ukiwa na hela shida, ukiwa masikini shida... Sasa sijui hata mtu uweje.. Ukiunga mkono juhudi shida , usipounga mkono juhudi shida pia.. Daaah
Kwa utawala huu ukiwa na pesa ndio shida kabisa
 
Wasiojulikana wamerudiii tena.....
 
Kuna hizi habari kwamba Mfanyabiashara Mohamed Dewji ametekwa leo asubuhi maeneo ya Collosium Gym , Oysterbay alipokuwa ameenda kufanya mazoezi..

Mwenye habari kamili atujuze.

======

UPDATES:

Mfanyabiashara maarufu nchini, ambaye pia ni mwekezaji wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji (Mo Dewji), anadaiwa kutekwa na watu wasiojulikana waliokuwa na silaha za moto, saa 11 alfajiri wakati akiingia kufanya mazoezi katika gym ya Colosseum, Oysterbay jijini Dar leo Oktoba 11. Kamanda wa Polisi Kinondoni, Jumanne Muliro athibitisha.

RPC Lazaro Mambosasa amesema Polisi Dar inafuatilia madai ya kutekwa kwa mfanyabiashara huyo maarufu nchini

UPDATE 1:

Dereva wa Uber amesema aliona watu 4 wakishuka kwenye gari dogo, wakiwa wamejifunika usoni, wakapiga risasi moja juu na kumchukua Mohammed Dewji

UPDATE 2:

RPC Lazaro Mambosasa amesema waliomteka mfanyabiashara Mohamed Dewji (Mo) ni wazungu wawili. Aidha, amesema msako mkubwa unafanywa kwa raia wa kigeni wote waliopo nchini kufuatia kutekwa kwa Mo Dewji

UPDATE 3:

RPC Lazaro Mambosasa amesema watu watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano kuhusu kutekwa kwa mfanyabiashara Mo Dewji

Walomteka ni ma professional hawajadhuru mtu mwingine wameafata kilichowapeleka tu kwa 100% sio wabongo hawa
 
Kumbe ni wazungu
IMG-20181011-WA0002.jpg
 
Back
Top Bottom